TAMISEMI wekeni vizuri mfumo wenu wa kuomba ajira za ualimu

scolastika

JF-Expert Member
Jan 26, 2019
3,771
5,541
TAMISEMI wekeni vizuri system yenu ya kuomba ajira za ualimu, yaani karibia wiki inaisha system inasumbua tu, kila siku tunapanda gari kwenda mjini, tunakaa asubuhi mpaka jioni ila system haikubali.

Tufanyeje jamani hela zinaishia kwenye nauli na kazi yenyewe watu nyomi wanataka, emu acheni ubabaishaji.
 
Wapo baadhi kwa mbindeee usiku hatulali ila mambo ni magumu nimeamkia internet cafe ngoja nisubiri mpaka usiku.
Ni lazima uende internet cafe? Maana kama unainternet hapo kijijini unaweza kumaliza hapohapo unless kama kuna utaratibu mwingine
 
Internet cafe ndo afadhali na so zote na zinazojitahd ni kwa shda sana pc haikubali wala smu
 
Itakua overloaded kipindi cha mchana. Jaribu usiku.

Je kuna aliyefanikiwa? Hebu fanya utafiti kidogo
Hakuna kitu kama hicho(overloaded) kwani haifunguki kabisa, hadi nawaonea huruma, wanavyohangaika!! Isije kuwa ni usanii kwani hata mazingira yenyewe ya hizo, ajira ni kama ya kisiasa siasa hivi!!! Unakuja shangaa dead line, inafika unaambiwa waliotuma maombi ni wengi sana, wasubiri kupangiwa kazi wale waliochaguliwa, ndio kimyaaaa!!!
 
Kabisaaa
 
Jmani msaada wa hili tatizo now naandikiwa servise temporarily unavailable
Screenshot_20200910-202613_Chrome.jpg
 
Poleni sana! Ingekua enzi zile za JK, hakuna kutuma maombi wala nini!! Unashangaa tu jina limetoka. Unaenda kuripoti, ukiona mazingira ni magumu, unasepa zako!

Shikamoo JK!!
Dah!...kweli kila kitabu kina kurasa zake...Sasa hivi mambo yamebadilika Sana.
 
Poleni sana! Ingekua enzi zile za JK, hakuna kutuma maombi wala nini!! Unashangaa tu jina limetoka. Unaenda kuripoti, ukiona mazingira ni magumu, unasepa zako!

Shikamoo JK!!
Nakumbuka kipindi kile cha JK ndio ziliposhamiri Shule Za kata ambazo zilianza 2004 kipindi cha Mkapa.
Shule nyingi zilikua Hazina walimu kabisa na walimu wengine waliazimwa primary kwenda kusaidia Sekondari.
Kulikua na uhaba mkubwa sana wa walimu wa Sekondari nakumbuka mpaka walitafutwa walimu wa Voda fasta lakini bado uhaba uliendelea.
Vyuo vyote vikuu isipokua vya udaktari wa binadamu vilielekezwa kufundisha pia masomo ya ualimu.
Sasa walimu wakajaa kwa vyuo kutoa graduate wengi wa ualimu, tatizo la walimu wa Art likaisha. Mjini kuna shule zikawa na walimu wengi mpaka wanakosa masomo wanagawana mada tu. Tatizo jingine ikaonekana walimu wote wakipangwa vijijini ama wanakimbia ama wanahama nalo bado linasumbua.
Tatizo kubwa kabisa lililobaki ni la walimu wasayansi ambalo nalo litaisha sio muda mrefu.
Kama walimu wote wanaomaliza Chuo wakipangwa mashuleni kunauwezekano baadae wanafunzi wakazidiwa na walimu, walimu wakawa wengi mno kupita mahitaji.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom