TAMISEMI: Watakaoshindwa kukamilisha zoezi la kupandisha watumishi madaraja kuchukuliwa hatua

Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
3,387
3,574
Update from OR TAMISEMI

Watakaoshindwa kukamilisha zoezi la kupandisha watumishi madaraja kuchukuliwa hatua - Prof Shemdoe

Na Raphael Kilapilo - Dar es Salaam

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Profesa Riziki Shemdoe amesema atachukua hatua kwa viongozi watakaoshindwa kusimamia zoezi la ubadilishwaji wa kada na upandishwaji wa vyeo kwa watumishi wote walio chini ya OR-TAMISEMI, na kuagiza zoezi hilo kukamilika ndani ya siku moja ya ziada.

Profesa Shemdoe alitoa agizo hilo leo Juni 17, 2021 alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo ambapo pamoja na mambo mengine aliwasisitiza wale wote waliopewa dhamana ya kufanikisha suala hilo kukamilisha haraka, ikiwa ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Sintokuwa tayari nipoteze kazi kwa sababu ya uzembe wa mtu, kila halmashauri inapaswa kukamilisha kazi hiyo ifikapo kesho, nasisitiza kuwa wale ambao bado hawajakamilisha kazi hiyo hadi hivi sasa kuhakikisha wanaliza kabla ya hatua zingine,” alisisitiza Profesa Shemdoe.

Alieleza kuwa hadi kufikia jana Juni 16, 2021 asilimia 80 ya watumishi 239,000 kutoka mamalaka zote za Serikali za Mitaa walikuwa tayari wameshaingizwa katika mfumo huo huku asilimia 20 iliyobaki ikitarajiwa kukamilishwa Juni 16-17, 2020 tayari kwa utekelezaji wa agizo hilo la Rais Samia.

Aidha alizipongeza Halmashuri zote zilizopambana kwa kujitoa usiku na mchana kufanikisha zoezi hilo, na zaidi pongezi hizo akizielekeza kwa uongozi na timu ya maafisa utumishi wa Jiji hilo la Dar es Salaam kwa ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa jukumu hilo.

Kwa mujibu wa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo Bernadetha Mwaikambo, hadi kufikia jana watumishi 2555 kati ya 2625 walikuwa tayari wameshaingizwa katika mfumo huo wa upandishwaji vyeo na kwamba idadi ya watumishi 70 waliosalia kutokuingia kwao kumetokana na changamoto mbalimbali ambazo Katibu Mkuu huyo wa Tamisemi amesema atazifanyia kazi.

Pia Profesa Shemdoe alisema kuwa awali zoezi la utekelezaji wa mfumo huo lilipaswa kukamilika Juni 12, 2021 lakini kutokana na uwepo wa changamoto mbalimbali walifanya mazungumzo na Wizara ya Utumishi, hatua iliyosaidia kuongezewa muda kidogo ili kulikamilisha.

Alitoa msisitizo kwa maafisa hao kuhakikisha wanapaswa kuitumia fursa hiyo ya ziada iliyotolewa ipasavyo ili kukamilisha suala hilo vinginevyo watachukuliwa hatua za kitumishi.

Kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa umma Na 8 ya mwaka 2002, pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003 na taratibu za uendeshaji za mwaka 2003, pamoja na miongozo na nyaraka mbalimbali zilizotolewa na Serikali, Mamlaka ya kupandisha vyeo watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa isipokuwa Walimu kwa mujibu wa Kanuni ya D. (f) na (g) ya Kudumu ya mwaka 2009 ni Halmashauri yenyewe.
 
Ngonjera zimeanza tena.
Zoezi limekamilika Juni 12.
Siku za nyongeza ni Juni 16-17
Then tunaambiwa siku ya nyongeza ni moja tu.
Kwahiyo tarehe 16-17 ni siku moja?
 
Profesa Shemdoe alitoa agizo hilo leo Juni 17, 2021 alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo ambapo pamoja na mambo mengine aliwasisitiza wale wote waliopewa dhamana ya kufanikisha suala hilo kukamilisha haraka
Ameshindwa kusemea Dodoma
 
niulize swali nje kdg ya mada'Rais alisem nyongeza ya mshahar hadi mwakan'
je kwa mwaka huu ile annual increment nayo hadi mwakan ama vp?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Update from OR TAMISEMI

Watakaoshindwa kukamilisha zoezi la kupandisha watumishi madaraja kuchukuliwa hatua - Prof Shemdoe

Na Raphael Kilapilo - Dar es Salaam

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Profesa Riziki Shemdoe amesema atachukua hatua kwa viongozi watakaoshindwa kusimamia zoezi la ubadilishwaji wa kada na upandishwaji wa vyeo kwa watumishi wote walio chini ya OR-TAMISEMI, na kuagiza zoezi hilo kukamilika ndani ya siku moja ya ziada.

Profesa Shemdoe alitoa agizo hilo leo Juni 17, 2021 alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo ambapo pamoja na mambo mengine aliwasisitiza wale wote waliopewa dhamana ya kufanikisha suala hilo kukamilisha haraka, ikiwa ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Sintokuwa tayari nipoteze kazi kwa sababu ya uzembe wa mtu, kila halmashauri inapaswa kukamilisha kazi hiyo ifikapo kesho, nasisitiza kuwa wale ambao bado hawajakamilisha kazi hiyo hadi hivi sasa kuhakikisha wanaliza kabla ya hatua zingine,” alisisitiza Profesa Shemdoe.

Alieleza kuwa hadi kufikia jana Juni 16, 2021 asilimia 80 ya watumishi 239,000 kutoka mamalaka zote za Serikali za Mitaa walikuwa tayari wameshaingizwa katika mfumo huo huku asilimia 20 iliyobaki ikitarajiwa kukamilishwa Juni 16-17, 2020 tayari kwa utekelezaji wa agizo hilo la Rais Samia.

Aidha alizipongeza Halmashuri zote zilizopambana kwa kujitoa usiku na mchana kufanikisha zoezi hilo, na zaidi pongezi hizo akizielekeza kwa uongozi na timu ya maafisa utumishi wa Jiji hilo la Dar es Salaam kwa ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa jukumu hilo.

Kwa mujibu wa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo Bernadetha Mwaikambo, hadi kufikia jana watumishi 2555 kati ya 2625 walikuwa tayari wameshaingizwa katika mfumo huo wa upandishwaji vyeo na kwamba idadi ya watumishi 70 waliosalia kutokuingia kwao kumetokana na changamoto mbalimbali ambazo Katibu Mkuu huyo wa Tamisemi amesema atazifanyia kazi.

Pia Profesa Shemdoe alisema kuwa awali zoezi la utekelezaji wa mfumo huo lilipaswa kukamilika Juni 12, 2021 lakini kutokana na uwepo wa changamoto mbalimbali walifanya mazungumzo na Wizara ya Utumishi, hatua iliyosaidia kuongezewa muda kidogo ili kulikamilisha.

Alitoa msisitizo kwa maafisa hao kuhakikisha wanapaswa kuitumia fursa hiyo ya ziada iliyotolewa ipasavyo ili kukamilisha suala hilo vinginevyo watachukuliwa hatua za kitumishi.

Kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa umma Na 8 ya mwaka 2002, pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003 na taratibu za uendeshaji za mwaka 2003, pamoja na miongozo na nyaraka mbalimbali zilizotolewa na Serikali, Mamlaka ya kupandisha vyeo watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa isipokuwa Walimu kwa mujibu wa Kanuni ya D. (f) na (g) ya Kudumu ya mwaka 2009 ni Halmashauri yenyewe.
Eti siko tayari kupoteza kazi yangu
Means Jamaa asingetishiwa watumishi ingekula kwao
 
Siku nikiiona hiyo hela nitakaa chini niliee kwa uchungu nikikumbuka jinsi safari ya jangwani ilivokua ngumu
 
tatizo la watumishi wa umma hampendani, kila idara mnaumizana nyinyi kwa nyinyi, mnabaniana, unafiki na majungu ndio mtindo wa maisha yenu, kusemana vibaya kuharibiana n.k, unakuta kiongozi anapiga pini aliye chini asipande, roho mbaya!! utadhani hela inayo lipwa ni ya kampuni yake binafsi kumbe ni serikali ya watanzania wote.
Jirekebisheni, badilikeni, pendaneni ndipo hata sisi wananchi tutakuwa na imani kwenu.
 
Umenena kweli tupu ubarikiwe mkuu.
 
Yani sijui tu hii ngozi tuna tatizo gani katika hivi vichwa yani uliyoandika ndiyo uhalisia ulivyo.
 
Back
Top Bottom