TAMISEMI: Sheria ya serikali za mtaa, the urban planning act 2007 zimepitwa na wakati

Maze runner

Member
Dec 7, 2021
32
39
Kumekuwa na claim nyingi juu ya kupandishwa hadhi kwa vijijj, mitaa, na halmashauri kadhaa kutokana na kutimiza vigezo vya kupanda kadhi vilivoekwa na Sheria na kanuni zetu.

Suala hili limechangiwa na kupitwa na wakati kwa Sheria mbalimbali zinazoongoza sekta hiyo. Hivyo Kuna uhitaji was wizara husika kufanya mabadiliko ya Sheria na kanuni ili kuleta maboresho yenye tija. Kwa mfano;
1. Mbagala na mbunge wao ametaka mbagala iwe jiji na rais alikubaliana na ombi Hilo. Ukweli Ni kwamba kwa vigezo vya Sasa mbagala wanna uhalali wa kuwa wilaya. Ila kiuhalisia mbagala haina hadhi ya kuwa jiji.
2. Geita mjini nayo wanataka kupanda hadhi vile vile wakati hakuna haja kiuhalisia.
3. Chato kutaka kuwa mkoa.
4. Dar es salaam kuwa mkoa na wilaya tano nk.

Mapendekezo ya kubadili baadhi ya Sheria na kanuni;

VIGEZO VYA KUANZISHA HALMASHAURI ZA MANISPAA
"Kuwa na watu wasiopungua milioni 1."

VIGEZO VYA KUANZISHA HALMASHAURI ZA JIJI
"Kuwa na watu wasiopungua milioni 3-4."

VIGEZO VYA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA.....
" Eneo la mita mraba pamoja na idadi ya watu na mengineyo yaboreshwe"

Tukifanya hivyo, serekali yetu na nchi yetu itaweza kwenda na muda na kuokoa fedha zinazopotea pamoja na kuongeza usimamizi mzuri was miradi na mapato. Baadhi ya mafanikio tutakayo pata baada ya kuchukua hatua hizo Ni pamoja na;
1. Dar es salaam yote isipokuwa kigamboni kuwa wilaya yenye hadhi ya jiji
2. Kigamboni kubaki na hadhi yake wilaya-halmashauri ya manispaa
3. Dar na kigamboni kuwa ndani ya mkoa wa pwani hivo kupunguza gharama za kuwa na wakuu was MIA 2, wakuu was WILAYA 4 kwa dar gharama zao zitaondoka na kubaki mmoja tu ambae atakjwa DC wa dar es salaam.
4. Claim za kijinga za kupanda madaraja pasi na umuhimu Wala tija
 

Attachments

  • 5a17e034314be844048999.pdf
    32.8 KB · Views: 7
Back
Top Bottom