TAMISEMI: Serikali kuifanyia mapitio Sera ya Zahanati kila Kijiji na Kituo cha Afya kila Kata

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange amesema Serikali imeamua kuifanyia mapitio Sera ya Zahanati katika Vijiji na Vituo vya Afya katika Kata.

Ameeleza, "Tumeamua hivyo ili tuwe na ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya kimkakati zaidi badala ya kuwa kila Kijiji na kila Kata"

Kauli yake ni baada ya Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Dkt. David Mathayo David kuhoji ni lini Serikali itapeleka Watumishi wa Afya katika Zahanati Jimboni kwake ili zisifungwe kwani Sera ya Serikali ni kuwa na Zahanati kila Kijiji na Kituo cha Afya katika kila Kata.

1624867468239.png

 
Huyu ni mjinga. Huduma za muhimu kama hizo inatakiwa ziwafikie wananchi wote. Aliyeandaa hiyo sera aliona mbali sana.

Sijui tunaongozwa na mambumbumbu gani?
 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange amesema Serikali imeamua kuifanyia mapitio Sera ya Zahanati katika Vijiji na Vituo vya Afya katika Kata

Ameeleza, "Tumeamua hivyo ili tuwe na ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya kimkakati zaidi badala ya kuwa kila Kijiji na kila Kata"

Kauli yake ni baada ya Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Dkt. David Mathayo David kuhoji ni lini Serikali itapeleka Watumishi wa Afya katika Zahanati Jimboni kwake ili zisifungwe kwani Sera ya Serikali ni kuwa na Zahanati kila Kijiji na Kituo cha Afya katika kila Kata
Kuwa na zahanati kila kijiji siyo kiashiria cha maboresho ya sekta ya Afya, bali ni kiashiria cha kuzorota kwa uwekezaji kwenye sekta ya Afya ya msingi (Primary Health care).
Serikali kwa kushauriwa vibaya na wataalamu, emejikita zaidi kwenye tiba(curative services) kwa sababu huko ndiko maslahi hasa kwenye manunuzi ya madawa na vifaa tiba kwa magonjwa yanayoweza kuzuilika.
Ghalama za uwekezaji kwenye Afya ya msingi ni ndogo sana ukilinganisha na huduma ya tiba. Lakini matokea yake ni makubwa zaidi.
Kinachitakiwa ni kuwa na kituo cha huduma ya Afya kila kijiji, chenye watumishi wasiopungua watatu. 1.Afisa
Afya, ambae jukumu lake ni kuelimisha jamii na kukagua hali ya usafi na mzingira kila kaya kwa mujibu sheria ya Afya na mazingira.
2.Muuguzi mkunga msaidizi, jukumu lake ni huduma ya kwanza kwa wagonjwa, huduma ya kliniki ya mama na mtoto narufaa kwenda kwenye zahanati ya kata.3 Mlinzi wa kituo.
Jamii ikiwezeshwa kupata huduma hii ya Afya ya msingi idadi ya wagonjwa wanaolazimika kutaka tiba watapungua.(Health needs) Tukishindwa kuwekeza kwenye Afya ya msingi,tutegemee wagonjwa kuendelea kumiminika kwenye vituo vya tiba(Health demands) na kupelekea nchi kutumia fedha nyingi
pasipo sababu.
Kwa kifupi ni kwamba Serikali iangalie namna ya kuwekeza zaidi kwenye Afya ya msingi ( PRIMARY HEALTH CARE) ili kuokoa fedha na nguvu kazi ya Watanzania.
 
Yale mambo aliyaweza magu tu, huyu mama tutamuonea tu na kibarua kizito cha kulea watoto watukutu(mafisad)
 
Back
Top Bottom