TAMISEMI sasa ni ya wananchi, Waziri Ummy Mwalimu anastahili pongezi

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
71
75
Leo nimemskiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na amesisitiza Ujenzi wa Vituo vya Afya katika Tarafa 207 utatumia utaratibu wa FORCE ACCOUNT sio KANDARASI. Na ameagiza watumie Mafundi Ujenzi waliopo ktk eneo husika ili kutoa ajira na kuchochea mzunguko wa fedha kwa wananchi kwenye maeneo ambayo mradi unatekelezwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI pia amesema Wizara imepokea Sh 22.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 90. Fedha hizo zimetokana na tozo za miamala ya simu.

TAMISEMI kupokes Shiling. Bil 7 za Tozo ya Mawasiliano kukamilisha maboma ya madarasa 560

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa @ortamisemitz wiki ya tarehe 23-29/08/2021 itapokea kiasi cha shilingi bilioni 7 kitakamilisha maboma ya madarasa 560 ili kupunguza uhaba wa madarasa na maandalizi ya kuwapokea wananfunzi wa kidato cha kwanza wa Elimu bila ada mwaka 2022.

Kutokana na utekelezaji wa Sera ya elimu msingi bila ada kutakuwepo na ongezeko la wananfunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 na kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwa sasa wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza darasa la saba mwaka 2021 ni takribani wanafunzi 1,129,129 .

Kati ya hao wanaotegemewa kufaulu ni 944,855 sawa na asilimia 84; Ongezeko ni wanafunzi 522,452 ukilinganisha na wanaomaliza Kidato cha nne mwaka 2021 ambao ni 422,403.

kutokana na ongezeko la wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 kunauhitaji wa madarasa 10,447, hivyo fedha ambazo wananchi wamechangia kupitia tozo za mawasiliano zitasaidia ujenzi wa madarasa hayo.

Ujenzi wa Darasa moja hugharimu kiasi cha shilingi milioni 20 lakini lakini maeneo mengi wananchi wamejitoa na kuchangia, wameanza ujenzi madarasa na kuyafikisha kwenye lenta kwa hiyo Serikali itapeleka kiasi cha shilingi milioni 12.5 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa darasa moja , hivyo shilingi bilioni 7 zitakamilisha takribani madarasa 560.

Kwa muda mrefu Wizara hii ilikosa Waziri Mchapakazi aina ya Ummy Mwalimu ambaye kwa muda mfupi amefanya ziara mikoa mbalimbali, vijijini, amekutana na changamoto, amezitolea maelekezo na sasa matokeo yanaanza kuonekana. Ummy Mwalimu anastahili Pongezi.

IMG-20210820-WA0034.jpg
 
Kwanza ile kusema Eti mafundi watoke kijijini pale pale mradi utakapojengwa naona nia ni njema lakini changamoto zake ni pamoja na kukosa mafundi mahiri wakisasa wanaokwenda na wakati.

Kijijini kwenyewe nyumba za matofali zinahesabika!

Na mara nyingi mafundi huwa wanatolewa mbali labda Wilayani!

Lakini kwa vyovyote vile watajua wenyewe!
 
Hauishi Tanzania mkuu?
Kwanza ile kusema Eti mafundi watoke kijijini pale pale mradi utakapojengwa naona nia ni njema lakini changamoto zake ni pamoja na kukosa mafundi mahiri wakisasa wanaokwenda na wakati.

Kijijini kwenyewe nyumba za matofali zinahesabika!

Na mara nyingi mafundi huwa wanatolewa mbali labda Wilayani!

Lakini kwa vyovyote vile watajua wenyewe!
 
Tunatakiwa tujenge shule sio vyumba vya madarasa kwa sababu shule sio madarasa peke yake. Ni yale yale ya matundu ya vyoo. Nashauri wangeongeza shule na wangewekeza zaidi kwenye makazi bora ya walimu.

Amandla...
 
Ujenzi wa mabweni kwenye Shule za kata yanapaswa kupewa kipaumbele lakini sijasikia akizungumzia.

Shule ziko mbali sana na ndio chanzo cha mimba za utotoni na wengine kuacha Shule kwa kuishia njia. Nani atembee kwa miguu zaidi ya kilometers 50 kwenda na kurudi kila siku
 
Ujenzi wa mabweni kwenye Shule za kata yanapaswa kupewa kipaumbele lakini sijasikia akizungumzia.

Shule ziko mbali sana na ndio chanzo cha mimba za utotoni na wengine kuacha Shule kwa kuishia njia. Nani atembee kwa miguu zaidi ya kilometers 50 kwenda na kurudi kila siku
Au zijengwe shule karibu na wanakoishi.
Amandla...
 
1. Ushauri: Hayo madarasa na zahanati ziandikwe "jengo hili limejengwa kwa fedha za tozo za miamala ya simu za watanzania".

2. Ucheshi: Watakaofuja pesa za tozo wahamishiwe Burundi kwa lazima.
 
Back
Top Bottom