Tamisemi na Utumishi kwanini mnamkwamisha Rais Samia

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
478
962
Habar zenyu mabibi na mababu..

Inasemekana kuwa kauli ya Rais ni sheria tena yapaswa kutekelezwa mara moja, Rais anapotoa order usipotekeleza ni kama unapingana na maagizo ya bosi wa nchi.

Mhe Rais Samia suluhu hassan alitoa maagizo katika wizara mbili wizara ya tamisemi na wizara ya utumishi ambazo zote ziko chini ya ofisi ya Rais ya kuwa watoe ajira za ualimu 6000 mara moja haraka iwezekanavyo ili kufanya replacement ya waliostaafu, waliokufa na kutumbuliwa, na alisisitiza kuwa hizo sio ajira mpya.

Katika hali ya kustaajabisha mpaka leo hii hakuna jipya lolote hakuna tamko wala ata tangazo la ajira kuwa vijana waombe ajira, je mawaziri hawa wameamua kumkwamisha rais.

Mbaya zaidi kuna vijana wametoka mashambani wamekuja maeneo ya mjini kwa shemeji zao walau waweze kufanya applications ila mpaka sasa holaa.

Waziri wangu Ummy Mwalimu wewe ni mchapakazi sana nashangaa hili la ajira ambalo mh rais ameshatoa kibali chake linakushindaje wewe??? Embu kuweni na huruma na watoto wa kimaskini, wakisema wasahau ajira waende wakalime nyanya mnakuja mnawatamanisha kuwa ajira zipo afu mnawaacha kwenye mataa.
 
Waziri alisema bungeni ajira hizo zitatoka tarehe 30 July 2021 kwahiyo mkuu kuwa na subra
 
Vipi jamani na hii iliyosema na waziri wa utumishi ,mbona Mambo hayaeleweki
Screenshot_20210503-194643.jpg
 
Wizara inabidi imulikwe aisee, watu wanateseka
Ummy hamna kazi kabisa. Anatakiwa awepo mtu anaemuendesha kama kipindi cha covid ilivyokua.
Anajichekesha chekesha anadhani watu wanakazi na mimeno yake.
Badilika wewe,Jafo pamemshinda hapo wewe hutoboi.
Ummy jimbo limemshinda.
Halmashauri yake imeoza. Jiji linaongozwa kizembe mno
 
Okay
 
Ummy hata kampeni ndio hivyo tena,jimboni anabwabwaja halmashauri inakufa. Wananchi wananyanyaswa DED na Afisa aedhi aitwae Tony. Ummy anawasifia eti hawagombani.
Aibu yake.
Ngoja hao jamaa zake waliwe vichwa muda sio mrefu sijui ataishije jimboni,sijui ataringa na hao wapambe chawa wenyeviti wa mitaa na walimu uchwara.
 
Umenigusa Sana mtoa maada ruwasa walitangaza nafasi za kujitolea mwez wa pili tukatuma maombi.mpk Sasa kimya
 
Hizo ajira mchakato unaendelea wanachukua majina ya walimu wanaojitolea.
 
Habar zenyu mabibi na mababu..

Inasemekana kuwa kauli ya Rais ni sheria tena yapaswa kutekelezwa mara moja, Rais anapotoa order usipotekeleza ni kama unapingana na maagizo ya bosi wa nchi.

Mhe Rais Samia suluhu hassan alitoa maagizo katika wizara mbili wizara ya tamisemi na wizara ya utumishi ambazo zote ziko chini ya ofisi ya Rais ya kuwa watoe ajira za ualimu 6000 mara moja haraka iwezekanavyo ili kufanya replacement ya waliostaafu, waliokufa na kutumbuliwa, na alisisitiza kuwa hizo sio ajira mpya.

Katika hali ya kustaajabisha mpaka leo hii hakuna jipya lolote hakuna tamko wala ata tangazo la ajira kuwa vijana waombe ajira, je mawaziri hawa wameamua kumkwamisha rais.

Mbaya zaidi kuna vijana wametoka mashambani wamekuja maeneo ya mjini kwa shemeji zao walau waweze kufanya applications ila mpaka sasa holaa.

Waziri wangu Ummy Mwalimu wewe ni mchapakazi sana nashangaa hili la ajira ambalo mh rais ameshatoa kibali chake linakushindaje wewe??? Embu kuweni na huruma na watoto wa kimaskini, wakisema wasahau ajira waende wakalime nyanya mnakuja mnawatamanisha kuwa ajira zipo afu mnawaacha kwenye mataa.
SIASA IMESHATAFUNA HII NCHI TUENDELEENI KUPAMBANA KITAAA
 
Back
Top Bottom