TAMISEMI mnamkwamisha Mkandarasi kwa cheap popularity

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Ni aibu kwa wasomi wa nchi yetu kutetea au kuunga mkono kinachofanywa na TAMISEMI katika jengo linaloendelea kujengwa.

Kwanza, KWENDA eneo la ujenzi wakati wewe siyo fundi au muhusika wa ujenzi Ni hatari kwa usalama wako na ndio maana maeneo ya ujenzi uzungushwa fensi kuzuia movement za watu. Yamkini watumishi hawa usalama wao siyo kipaumbele.

Pili, kuishi kwenye jengo linaloendelea kujengwa ni kumkwamisha mjenzi.

Tatu, hoja siyo kuripoti kazini Bali hoja ni kufanya kazi..kwa mazingira yaliyoonyeshwa huko dodoma inatupa picha kwamba watu hawaendi kufanya kazi Bali wanaripoti maeneo yao ya kazi na kurejea nyumbani hivyo wanalipwa bure.

Nne, waziri anapaswa kutumbuliwa kwa kuwadanganya wananchi kwamba amehamia kwenye jengo linaloendelea kujengwa. Huwezi kwenda shambani bila jembe the ukatuaminisha kuwa unalima.Niombe waandishi wa habari watuonyeshe wazi ni kazi gani za kiofisi zinafanywa katika eneo hilo. Watuonyeshe computers zilipofungwa na watuonyeshe namna utekelezaji wa majukumu unavyoendelea.

Tano, hii Ni aina ya viongoz au watendaji wasiohitajika serikalini. Rais ni binadamu na anaweza akatamka Jambo baadaye akafuata akaombwa msamaha au akeleweshwa na kuelewa, tulitegemea Waziri amweleweshe Rais. Ni Bora ukafukuzwa kazi kwa kueleza ukweli kuliko kuwepo kazini huku ukitenda kwa kujidanganya na kumdanganya aliyekupa kazi.

Sita, Tujenge kujihamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali hii imejaa wakina "Yes Sir" wengi mno, karibia wote tu.

Na hii inatudhihirishia wazi kuwa Huko kwenye Vikao vya Baraza la mawaziri hakuna discussions,ni orders tu.

Tumepatwa awamu hii, dah!
 
Na wao walikua wapi wasimalize jengo kwa wakati?????... adhabu yao wahamie hivyo hivyo.. na ole wao wasifanye kazi.. watajuta..
 
Na wao walikua wapi wasimalize jengo kwa wakati?????... adhabu yao wahamie hivyo hivyo.. na ole wao wasifanye kazi.. watajuta..
Kwani wote wanaohamia walikuwa wanahusika kumalizia hilo jengo mkuu? Kwanini uite adhabu yao!
 
Back
Top Bottom