msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 839
- 1,472
Naibu waziri-Tamisemi, mhe. David silinde akiongea na kituo kimoja cha redio huko Lindi ametoa agizo kwa walimu wakuu kuorodhesha majina ya walimu wanaojitolea kwenye shule zao ili wapatiwe kipaumbele cha ajira kila zinapotangazwa na serikali. In fact ni agizo ambalo linahitaji tafakuri ya kina kabla ya kufanyiwa utekelezaji kwa sababu,
Kutoa kipaumbele kwa walimu waliojitolea ni ubaguzi wa wazi katika utoaji wa ajira za walimu kwa sababu kitendo hicho kinachochea rushwa,undugu na kujuana.
Kwa maana kinatoa mwanya kwa wakuu wa shule na maafisa elimu kata kuchomeka watu kwa hongo au ndugu zao kwa lengo la kuwasaidia kupata ajira serikalini kwa haraka.
Secondly, walimu wanaojitolea sio kwamba wanafundisha bure bila malipo yoyote isipokuwa wanalipwa,hivyo wana uhakika wa kupata chochote kitu kila mwisho wa mwezi.
Kwahiyo malipo wanayopata ingetosha kuwa motisha kwao lakini kwenye ajira washindane kwa usawa na walimu wengine bila kupewa upendeleo.
Thirdly, kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuwalipa, shule nyingi zinapokea walimu wachache sana kati ya mwalimu mmoja hadi watatu jambo linalopelekea walimu wengine kukosa nafasi za kujitolea japo Nia wanakuwa nayo.
Fourthly, ni ukweli usiopingika kwamba vijana wengi wanapitia kipindi kigumu cha ukali wa maisha kiasi cha mavazi waliyonunua wakiwa vyuoni kuchoka au kuchanika kabisa hivyo inawawia vigumu kwenda kujitolea kwa sababu hata viwalo vya kuvaa hawana.
Kufuatia ukweli huo, ndio maana Rais alitoa tamko vijana wote waajiriwe kwa usawa bila upendeleo kwa sababu anajua magumu wanayopitia, iweje leo tamisemi mtake kukinzana na agizo hili la mheshimiwa Rais?
Fifth, suala la kujitolea linawezekana kwa kijana anayeishi nyumbani na kuhudumiwa na wazazi wake lakini kwa kijana aliyeanza maisha ya kujitegemea na kulea familia mathalani watoto au wazazi wake ni gumu kwa kiasi chake.
Ni gumu kwa sababu nyuma yake kuna familia inamtegemea sasa akisema aache kibarua chake cha kujiegesha ili akajitolee kufundisha hamuoni kama anakuwa anaiweka familia yake rehani?
Kadhalika, kijana aliyepanga kama akienda kujitolea atalipaje kodi ya pango achilia mbali kumudu gharama za maisha?....Tamisemi kuweni na huruma toeni ajira kwa haki na usawa