TAMISEMI Kuweni na huruma na sisi,sisi ni binadamu wenzenu!

NAMBOGO

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
244
56
Hivi nyie watu wa Tamisemi mnaohusika na elimu,walimu walishawakosea nini,inakuwaje MTU adai malimbikizo ya mshahara kwa miaka minne bila mafanikio?wakati viambata vyote ameleta?kila mwaka mnasema fedha zimetengwa bado mnahakiki,ni taarifa gani za kuhakiki miaka4?Natamani Siku moja niwaone kwa sura nione wanavyofanana hawa watu,mnaboa,mnaudhi mnaleta hasira,kama kuna Mwl Mhanga wa hili hasa huku Katavi au popote aje hapa tushauriane!
 
Mtumbua jipu Wizara ya elimu ina mijipu kuanzia Wilayani hadi Wizarani fedha hizo zinatoka ila wanalipa kwa kuangalia usoni niliwahi kufuatilia Halmashauri ktk orodha ni mtu wa 46 ktk madai fedha imeletwa nilirukwa wakalipwa wanaowajua wao pale Halmashauri madai toka 2013 najuta kuingia sekta hii bora ningekimbilia TRA au Bandarini hata kama ningetumbuliwa wanangu wangenisifu ila huku Ualimuni nitalaumiwa tu na wanangu.
 
Hivi nyie watu wa Tamisemi mnaohusika na elimu,walimu walishawakosea nini,inakuwaje MTU adai malimbikizo ya mshahara kwa miaka minne bila mafanikio?wakati viambata vyote ameleta?kila mwaka mnasema fedha zimetengwa bado mnahakiki,ni taarifa gani za kuhakiki miaka4?Natamani Siku moja niwaone kwa sura nione wanavyofanana hawa watu,mnaboa,mnaudhi mnaleta hasira,kama kuna Mwl Mhanga wa hili hasa huku Katavi au popote aje hapa tushauriane!

Halmashauri ndio chanzo cha hayo yote mwl kapewa barua ya kupanda daraja mshahara haujabadilika huu mwezi wa 3.
 
Back
Top Bottom