Tamisemi kuweni makini na yanayoendelea kwenye mgawanyo fedha za ujenzi za kujengea Hospitali na Shule

Komando tamimy

Senior Member
Nov 18, 2020
108
121
Habari wanajukwaaa.

Mimi ni mdau wa elimu na pia wa maendeleo ya wananchi kwa nimekuwa mfatiliaji mzuri wa maswala ya ujenzi hasa kipindi hiki ambacho tamisemi kupitia Rais wetu Samia Suluhu wamezamilia wanafunzi wote watakaoanza kidato cha kwanza mwakani waripoti wote.Lakini nimegundua kuna mambo ambayo tamisemi nadhani hawakuyaweka sawa kwani baada ya kuweka fedha kwenye akaunti za halmashauri tamisemi ilitakiwa itoe miongozo ifuatayo.

1. itoe ramani ya majengo ambayo yanatakiwa kujengwa.
2. Materials ambayo yatakayotumika.
3. Wakandarasi wa Halmashauri ambao wameajiriwa na serikali wahusishwe.
4. Pesa ziwe chini ya bodi ya shule zisiwe chini ya DMO/RMO/MKUU WA SHULE/MWALIMU MKUU.
5. Tamisemi iunde Task force ya kufutilia utekelezaji wa miradi yao nawapite kila zone ambayo pesa ilipelekwa na serikali.
Ikumbukwe ujenzi ambao uko chini ya kiwango uigharimu sana serikali kwani uhitaji ukarabati wa mara kwa mara pia ikumbukwe hospitali na madarasa tunayojenga ni kwa ajili ya jamii yetu na vizazi vijavyo.

Kwanini nimeshauri hayo ni kutokana nimepita baadhi ya sehemu nimeoa yafuatayo.
Msingi wa jengo futi 1. Yaaani futi1 na wametandaza tofali jengo la serikali? Halafu linajengwa kwa tope!? Tena tofali zenyewe za kuchoma?!

Kuna sekondari ambazo zilijengwa na wakoloni mpaka leo ziko imara sasa sijui wakoloni walikuwa wazalendo kuliko sisi.?
Pia nimewaona baadhi ya wakuu wa shule/Dmo/Rmo/ wakilipa pesa bila kushirikisha bodi ya shule au vikao vya maamuzi sasa sijajua umakini wao katika mambo ya hela. Halafu itasababisha upotevu mwingi wa pesa. Kwani most of them are legalized bandits.

Kuna wengine nimeskia wabane pesa zitakazobakia watazipangia matumizi. Na hapo ndo shida kubwa ipo pia wengine wanadai badala ya kujenga madarasa ma2 wajenge ma3 sasa sijajua tamisemi imejipangaje nakumbuka nilikuwa kwenye ziara mkuu wa wilaya Songwe tukaenda shule siikumbuki tukakuta mtendaji mmoja anadai ameibiwa pesa yote ambayo ilitakiwa imalizie nyumba ya mwalimu tafsiri yake ni kwamba mtendaji huyo aliikabidhiwa pesa yote matokeo yake kaibiwa ila kama ni kweli.

Pia nikabahatika kuwa kwenye ziara ya nadhani peramiho daaaah tulioyakuta huko ni zaidi ya kilio bwalo la chakula la wanafunzi zaidi ya 700 linajengwa kwa tofali za tope hela na wakati huo pesa yote imeliwa.

Tamisemi njooo ni na mifumo na utaratibu sahihi wa kufanya kazi najua wizara ni kubwa lakini pia watendaji ni wengi.
Kuna taarifa ambazo ambazo nimepenyezewa na mmoja watu ambao ni reliable source kwamba wakuu wa shule wanatakiwa kutafuta mafundi naiona hatari na ubora hafifu wa majengo yatakayojengwa kwa sababu wengi wao watatafuta mafundi wenye kiwango cha chini.
 
Hii nchi ni ngumu sana.nimependa huo mstari ulioandika kwamba wakoloni ni wazalendo kuliko sisi.ni kweli kabisa nimesoma songea boys hiyo shule imejengwa na mkoloni mpaka leo ipo imara.lkn nikianglia shule ya kata imejengwa miaka ya 2000 leo hii ni choka mbaya.
 
Umeandika na kutoa maelekezo kizalendo sana,nami kwa upande wangu nahisi kutakuwa na matatizo makubwa kwenye huo mfumo wa ujenzi holela.

Ilitakiwa kuwe tathmini iliyotoa mpango na ramani elekezi kwa kila mkoa au kwa kila wilaya unaofanana kwenye vifaa vifaa vitakavyotumika na ubora wake na si kuachiwa kila alielipwa afanye kile ambacho ataona yeye kinafaa kwa utashi wake na familia yake

Tusije tukajuta na kulaumiana baadae kuwa pesa zilizotoka hazikutenda kulingana na matarajio yetu Kama taifa
 
Kilichopatikana huko wilayani MULEBA mkoani Kagera Ni zaidi ya kituko.

1.mkurugenzi mtendaji ndiyo msambazaji wa saruji.Kawaagiza watu watafute saruji ya kujengea msingi Kisha ya kumalizia atawauzia baada ya kuitoa kiwandani.

2.DC ndiyo muuzaji wa tofali kupitia SUMA JKT,eti kawaeleza wakuu wa Taasisi kuwa tofali zitatengenezwa na SUMA JKT.

3.bado hawajaelezwa bati zitaletwa na Nani ,je DAS ndiyo atakuwa msambazaji?

4.kila mkuu wa Taasisi Ni lazima atoe taarifa ya Kila Siku kwa katibu muunezi wa CCM.

Huu ujenzi inaonekana umeingiliwa na wanasiasa ,tumuombee waziri UMMY afuatilie kwa kina yanayojili huko muleba mkoani Kagera.

Hizi fedha si za wanaccm Bali Ni mkopo utakaolipwa na watanzania wote.
 
Mkuu madudu ni mengi mnoo ukija huku kwenye pesa za fidia za ada na ruzuku UTALIA MCHOZI UKUTOKE, wakuu wanapiga hizi hela vibaya sana.

Ila tatizo linaanzia UONGOZI wa juu kabisa, Watanzania tuna shida sana kwenye UAMINIFU.
 
Tatizo ni kuwa nchi imebaki ya kutegeana, badala ya kufuatilia, wakubwa wabasubiria nani atakayeharibu ili tumtumbue.
 
Kama nilivyosema most of the head of School are legalized bandits sasa kwenye Captation za ada wanaiba ? Je kwenye mamilioni haya ya ujenzi si ndio balaaa maanake mafundi waliotafuta upande wa ujenzi ni walevi kupindukia kwa sababu ya cheap price na chajuu tunahitaji kujenga shule ambazo zitadumi kwa miaka 50 ijayo.
Mkuu madudu ni mengi mnoo ukija huku kwenye pesa za fidia za ada na ruzuku UTALIA MCHOZI UKUTOKE, wakuu wanapiga hizi hela vibaya sana.

Ila tatizo linaanzia UONGOZI wa juu kabisa, Watanzania tuna shida sana kwenye UAMINIFU.
 
Back
Top Bottom