TAMISEMI itazame upya mgawanyo wa Gairo na Kilosa

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
¤ TAMISEMI itazame upya mgawanyo wa Gairo na Kilosa kwani Wilaya ya Kilosa kabla ya kugawanywa ilikuwa na kilomita za mraba 14,245. Ilipogawanywa Gairo ikapewa kilomita za mraba 1,851.34 tu sawa na asilimia 13 huku Kilosa ikibakiwa na kilomita za mraba 12,393.66 sawa na asilimia 87.

¤ Tarafa ya Magole ambayo ilitakiwa kuja Gairo kwenye maandishi, mihtasari na makubaliano tangu mikutano ya Vijiji, Baraza la Madiwani, DCC na RCC bado ipo Kilosa mpaka leo.

¤ Gairo kukatengenezwa Kata ndogondogo kama Kijiji ili iwe Wilaya. Leo hali ni tete hata kuendesha Halmashauri ni changamoto kubwa sana. Ukija kwenye mapato ndiyo usiseme.

¤ Sababu zinazosemwa za kuzuia Tarafa ya Magole isije Gairo hazipo kwenye maandishi mahali popote.

¤ Poa kwenye mgawanyo kuna fedha Gairo inadai Kilosa mpaka leo bila kulipwa!!

Hivyo ni Wananchi kwa ujumla wanaiomba Wizara ya OR-TAMISEMI kutazama upya mgawanyo huu. Pia wanaipongeza na kuishukuru kwa kazi nzuri wanayoifanya.
 
Back
Top Bottom