TAMISEMI: Halmashauri 90 CCM ishapita bila kupingwa, hakutakuwa na kampeni na mikoa mitatu tayari CCM ishashinda

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imetangaza kuwa mikoa mitatu haitafanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwa wagombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupingwa.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwita Waitara amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa, kati ya halmashauri za wilaya 184 nchini, 90 kati ya hizo hazifanyi uchaguzi huo Novemba 24 mwaka huu kwa kuwa wagombea wamepita bila kupingwa.

“Katika mikoa 26 ya hapa bara, kwa taarifa ambazo tumeshapokea mpaka leo asubuhi mikoa mitatu inaonekana kwamba wagombea wa Chama Cha Mapinduzi wamepita bila kupingwa kwa hiyo kuanzia siku ya uteuzi wao ni viongozi halali na wasimamizi wameshawateua, hakuna haja ya kampeni katika eneo hilo” ameyasema hayo wakati anazungumza kwenye kipindi cha Asubuhi Hii kinachorushwa na kituo cha redio cha TBC Taifa cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Wakati akizungumza na Habarileo leo mchana Waitara ameitaja mikoa ambayo haitafanya uchaguzi kabisa kuwa ni Katavi, Tanga, na Ruvuma.

“Mahalali ambako mgombea alikuwa peke yake na amepita bila kupingwa kazi ya msimamizi ni kumtangaza na baada ya hapo atasubiri baada ya tarehe 24 ataapishwa na ataanza majukumu yake kwa hiyo hakuna habari ya kampeni lakini mikoa 23 itakuwa na mchakato wa uchaguzi”amesema.
 
safi sana wapinzani wameweka mpira kwapani hawana uwezo wa ushindani na ccm
 
Kaeni tayari maana saa yaja maana siku hizo mzazi atamkimbia mwana aliyeko shamba abaki huko maana itakuwa kilio na kusaga meno. Mwenye masikio na asikie mwenye macho na aone. Tutubu tumrudie mungu muumba wetu
Una maana gani mbona unaweweseka?
 
Kama mna ogopa kampeni hadi mna wafanyia wapinzani figusi kwanini msipite bila kupingwa. Chama kikongwe kinacho ogopa uchaguzi. Halafu mnasema maendeleo mmeleta.
 
God bless my lovely country
tapatalk_jpeg_1573847648740.jpeg
 
Back
Top Bottom