Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,370
- 3,148
Habari ya mwisho wa wiki wanajukwaa
Sikutatu zilizopita niliandika habari yenye kichwa cha habari mkuu wa shule aliyeshindikana katika jiji la ,Jafo njoo umng'oe.
Wadau waliowengi wamekua na mtazamo ambao sio sahihi kwangu kwakuona kama vile ninamajungu,chuki au roho mbaya. Naomba niwaambie sinachuki na mkuu huyo wa shule ya sekondari Maweni iliyopo jijini Tanga
Mkuu huyo mbali na mambo mengine mengi ambayo alilalamikiwa kwa Afisa elimu jiji tangu mwaka jana na walimu wa shule hiyo na akawaahidi kuchukua hatua,hadi sasa hajachukua hatua ni matatizo kama lugha mbaya,kejeli,matusi na ubabe kazini na bado vimekua kama sehemu ya maisha yake shuleni
Msukumo wa kuandika mada hii umekuja pale ambapo mkuu huyu wa shule anafanya ubadhirifu wa waziwazi wa fedha za serikali na bado analindwa na wateule wake.
Amekua mkorofi kiasi kwamba hata fedha za fundi ambazo alitakiwa amlipe kupitia utaratibu wa force account pia amezila na amegoma kulipa. Tena anasema haogopi maana yeye ni usalama wa taifa.
Fundi alipoona hakuna msaada atakaoupata kwa afisa elimu huyo,aliamua kwenda PCCB hivyo ngoja tusikilizie hao jamaa maana hawana mambo ya kumpendeza mtu,niwatenda haki
Kibaya zaidi nikwamba Afisa elimu jiji amewaambia walimu wa shule hiyo hawatapata fursa kwakua eti hawamtaki mkuu huyu wa shule, hapa kuna maswali mengi
Tetesi za kuhamishwa baadhi ya walimu
Inasemekana kwamba walimu waliothubutu kumkatalia mkuu huyo wa shule kuandaa taarifa za udanganyifu juu ya namna alivyotumia fedha hizo, wameonekana kama kikwazo hivyo upo mpango wa kuwaondoa walimu hao shuleni hapo.
Hata Afisa elimu amewatishia walimu na kuwaambia wasije wakamlaumu kwa maamuzi atakayochukua juu yao. Swali ni je,kama ameiba mkuu wa shule,walimu wengine waliopigia kelele wizi huo wanahamishwa kwanini?
Au kauli hiyo ilikua ya kuwatishia walimu hao wasipaze sauti zao? Afisa elimu hapo ninadhani uliteleza ila angalia usije ukaamua ukiwa na hasira maana mchelea mwana,hulia mwenyewe
Ninawaahidi kuendelea kuwapa mrejesho wa kitakacho jiri,hasa aina yoyote ya ubabe na uonevu dhidi ya fundi na walimu hao
Kupitia jukwaa hili wadau wengi wataona na haki itatendeka