Tambwe Hizza amekuwa msemaji wa TAMISEMI?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Nimemsikiliza mwisho mwisho Tambwe Hizza katika bulletin ya Ch 10 usiku huu akitoa ufafanuzi kuhusu uchaguzi wa Meya Arusha kuwa ulifanyika kihalali na nonsense nyingine kuhusu yule Mbunge wa viti Maalum wa Tanga aliyepiga kura Arusha.

Nauliza, tangu lini Hizza amekuwa msemaji wa TAMISEMI? Ufafanuzi ulitakiwa utolewe na Mkuchika au bosi wake Pinda,
 
Mzee wa kuchumia tumbo huyo.
 
Mimi simlaumu Tambwe hata kidogo maana yeye hajui atendalo na kila mara hudhani ana majibu ya kuitetea CCM. Amekuwa akifanya juhudi kubwa sana kuitetea CCM lakini kila analoongea linachangia pakubwa kuibomoa na kuiaibisha CCM ambayo ina makada mahiri ambao wangetumika aibu hii isingejitokeza. Wa kulaumiwa ni yule aliyeruhusu Tambwe awe anaendesha diorrhea ya mdomo kama anavyofanya na kisha akabaki huru na kuendelea kupokea mshahara huku chama kikishuka hadhi yake.
 
Ataendelea kuchujwa kwenye nafasi ya kugombea ubunge hadi azeeke. Jamaa ameutafuta sana ubunge lakini CCM hawana fadhila na mdomo wake, wanamchakachua kama kawaida!
 
Back
Top Bottom