Tambwe Hiza Kukaangwa Kwa Mafuta Yake Mwenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tambwe Hiza Kukaangwa Kwa Mafuta Yake Mwenyewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kada wa Chama Cha Mapinduzi, Richard Hiza Tambwe Tuesday, May 04, 2010 2:11 AM
  MIKANDA ya video inayoonyesha mikutano iliyokuwa ikihutubiwa na kada wa Chama Cha Mapinduzi, Richard Hiza Tambwe wakati akiwa CUF akiiponda CCM huku akidai atafia CUF imeandaliwa kwa lengo la kummaliza kwenye harakati zake za kuwania ubunge wa Temeke Tambwe ametangaza nia yake ya kulitaka jimbo hilo la Temeke linaloongozwa na Mbunge Abbas Mtemvu kupitia CCM na wapinzani wake wamepanga kumkaanga kwa mafuta yake mwenyewe.

  Mwandishi wa Nifahamishe aliyepata kushuhudia mikanda hiyo, alielezwa na mtu aliyeomba jina lake lihifadhiwe kwamba mikanda hiyo baadaye itatumika kwa ajili ya kampeni ili kumuonyesha mwanasiasa huyo alivyokuwa kigeugeu.

  Baadhi ya mikanda hiyo inaonyesha kundi la wafuasi wa CUF wakisikiliza katika moja ya mikutano ya kampeni ambayo Tambwe alikuwa akielezea jinsi CCM inavyotumia hila za kuwarubuni wanasiasa wanaoona ni kikwazo kwao na kuwahamishia kwenye chama chao.

  Katika mikanda hiyo, Tambwe anaapa kutokuwa mmoja wa watu hao aliowaita 'waroho wa madaraka' na kusisitiza yeye atafia CUF ikiwa ni dhamira yake ya kuwatetea Watanzania.

  Imebainika kuwa kazi hiyo inafanywa kwa umakini kwa ushirikiano kati ya wanachama wa CUF na CCM, tayari mikanda hiyo ya video ipo tayari kutumiwa iwapo Tambwe Hiza atachaguliwa kuiwakilisha CCM.

  Hata hivyo kazi hiyo ya kudurufu haikufahamika mara moja endapo inafadhiliwa na chama cha CUF alichokikimbia na kuhamia CCM.

  Kwa mujibu wa habari hizo, katika kampeni za ubunge na madiwani zinazotarajiwa kuanza mwezi Oktoba, mikanda hiyo itakuwa ikionyeshwa katika 'Projekta' kubwa za vitambaa itakayokuwa ikionyeshwa usiku baada ya yeye kufanya kampeni zake mchana.

  'Projekta' hizo zitakuwa zikifungwa katika ofisi ndogo zitakazoanzishwa na vyama mbalimbali vitakavyosimamisha wagombea jimboni humo ili kuepuka dhana ya kuonekana kufanya kampeni katika muda usioruhusiwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

  Hivi karibuni, akitangaza nia yake ya kugombea ubunge jimboni Temeke, Tambwe alisema anafahamu kuwepo kwa watu wanaompinga, wanaopita kumtangaza vibaya na hata kumtukana na akaahidi yupo tayari kupambana nao.

  Tambwe aliyeanza kugombea ubunge jimboni humo kwa tiketi ya NCCR Mageuzi mwaka 1995, na baadaye kuhamia CUF alikogombea mara tatu na kisha kujiunga na CCM, anakabiliwa na makundi matatu yanayompinga katika jimbo la Temeke.

  Kwa mujibu wa wakazi wa jimbo hilo walioongea na Nifahamishe kwa nyakati tofauti wamebainisha kwamba, mwanasiasa huyo kwanza anapingwa na wanachama na wapenzi wengi wa vyama vya upinzani.

  Zimebainisha zaidi habari hizo kwamba makundi mengine ni pamoja na chama cha CUF alichokitosa na kuhamia CCM pamoja na mbunge wa wa sasa wa Jimbo hilo Abass Mtemvu anayeonyesha nia ya kulitetea jimbo lake.

  Hata hivyo Tambwe Hiza anaonyesha kukubalika zaidi kwa wakazi wa jimbo hilo wa kada ya kati ambao ni pamoja na vijana wengi waliofikia umri wa kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=4430546&&Cat=1
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hawa CCM bana huyu wangemwacha tu akafa kifo cha kawaida kama akina Jidulamabambasi na Danny Makanga...akimaliza ulaji Makamba, Tambwe atarudi kuwa konda wa dala dala haina haja ya kuumiza kichwa saaana.
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Waganga njaa AKA MAKANJANJA
   
 4. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,036
  Trophy Points: 280
  Hivi yuko wapi huyu bwana....Amani Nzugile Jidulamabambasi.....Ndo kafulia kimoja ama??
   
 5. Bright

  Bright Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo bwana hana msimamo kabisa na hafai kuwa kiongozi kwa kupitia chama chochote kile. Huyu ni mmoja wa wazee watarajiwa wa DSM watakaokuwa wanaongea na marais wanatarajiwa kama Ridhiwan.
   
 6. Mswahilina

  Mswahilina Senior Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Apr 7, 2008
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni mkuu wa wilaya ya "Mwanza Mjini"
   
 7. N

  Nanu JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndo wanasiasa uchwara hao, wanahangaika wanasema chama hakina sera kumbe yeye ndiye hakuwa na malengo!
   
 8. F

  Froida JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kwa mbinu za CCM safari hii atapita,ukweli akiondoka Baba yake Yusuf Makamba Ukatibu mkuu lazima na yeye ataondoka kakalia kuti kavu,sidhani kama walitoka jasho kuijenga CCM kwa tabu na raha wanafurahia jinsi alivyopewa ujiko eti yuko kitengo cha propaganda,
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,420
  Trophy Points: 280
  kama ridhiwani anataka kuwa rais kwa kigezo cha utoto wa rais ...asubiri kwanza ...capt[mst]makongoro nyerere awe rais[siku hizi katulia..na alipelekwa master na mkapa uk baada ya baba yake kufa..and he talk sense and of ana uchungu na nchi]..,then apewe urais ..hussein mwinyi[naye msomi huyu daktari],...then apewe urais..nico merinyo mkapa[naye msomi mwansheria ..ana llm] them ndio aje yeye riziwani[msomi pia ana llb]...

  yes namaanisha kuwa kama kuzaliwa na rais ni kigezo cha kugombea basi waanze hao.....
   
 10. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mkuu nimeipenda sana hii.Nadhani laiti wengi wetu tungekuwa na mtizamo kama huu (wa kuangalia miaka kadhaa mbele yetu) huenda leo tusingekuwa na mwana mipasho hapo Ikulu.
   
Loading...