Tambwe hiza, ahusisha migomo ya tanzania na chadema

Mimi sifahamu lakini nahisi ni STD VII na ana certificate of attendance ya kozi ya computer kwenye chuo kilichopo maeneo ya kariakoo. Ni mtanzania pekee aliyegombea ubunge mara tano na kushindwa. Kwa sasa ni msaidizi wa mkuu wa kitengo cha porojo na uropokaji cha sisiem. Kazi hiyo ameimudu sana tangu akabidhiwe na inasemekana muda wowote anaweza kupandishwa cheo kuwa full boss wa hicho kitengo.
 
namjua dereva wa daladala posta-mwenge
Huyu jamaa hawezi hata kuwa dereva kwa jinsi asivojua wapi au wakati gani aseme au afanye nini a.k.a hana busara.... anaweza kupiga honi mahakamani au hospitalini!!:suspicious:
 
Nimeitafut cv yake muda mrefu bila mafanikio, huyu bwana kwenye net huwezipata cv yake. Sidhani kama cv yake ni nzuri ndo maana hawezi ipachika mtandaoni!
 
Tambwe Hiza ni kijana aliyekulia Temeke Wailes nina uhakika alimaliza darasa la saba sina kumbukumbu kama alimaliza form two. Na kazi yake kubwa ilikuwa ilikuwa kuUza stationaries kwenye ki box pale posta club, nje ya Bilicanas au Break point, ame uza makaratasi na toners inc hewa saana CCM mkoa na wizara za serikali kabla ya kujiunga na vyama vya upinzani yaani NCCR or CUF.
Anafaa kuwa CCM lakini si katika Chama makini
INAWEZEKANA MUNGU AMERUHUSU HIZA TAMBWE NA BOSS WAKE MAKAMBA WAENDELEE KUWEPO CCM NA KUFANYA WANAYO YAFANYA ILI CCM IJIKAANGE KWA MAFUTA YAKE MWENYEWE, KWANI HAWA WATU NI MIZIGO MNO
 
huyu jamaa ni kilaza mwanzo mwisho...ana elimu ya darasa la saba kupitia mmekwa baada ya kuhitimu ..akajiunga upinzani kabla ya CCM kumwona akiungana na vilaza walionao...watatengeneza timu nzuri ya pumba:)
 
Hana CV, si kila mtu ana CV, hajasoma sasa CV ataandika nini?
he is useless, even defn.. ya katiba hajui, unategemea nini?
 
Hana CV, si kila mtu ana CV, hajasoma sasa CV ataandika nini?
he is useless, even defn.. ya katiba hajui, unategemea nini?

Duuu, kweli bwana!! Siyo kila mtu lazima awe na CV. Hivi kama alipomaliza shule ya msingi temeke then akaanza kuuza stationery kabla kujiunga na siasa, kuna haja ya kuwa na CV? Sidhani kama ni sahihi.
 
Wandugu,
Lazima kuna mwanachama wa JF aliyewahi kukutana na kuongea kidogo na mropokaji wa sisiem. Hivi huyo jamaa ana business cards?? Kama anazo, ameandika nini kuhusu elimu na cheo chake??
 
Si mpaka awe nayo basi hiyo business card. Kwa kweli Tambwe muuza mitumba wa soko la Tandika leo kuwa msemaji wa CCM ni dharau na matusi ambayo hayasameheki kamwe!
 
I am just curious wakuu.....i am trying to connect things he was saying kipama jotoni na elimu yake

Huyu jamaa hana "formal CV" lakini maelezo ya ukweli mafupi kabisa kama nimjuavyo mimi ni haya (miaka sikumbuki):

1. Amemaliza darasa la saba shule ya msingi Wailes Temeke Mwisho
2. Alikuwa akiishi Temeke Mwisho Wailes mtaaa wa Mombo
3. Alikuwa "Meter Reader" (msoma mita AKA Kishoka) wa Tanesco
4. Alijaribu kuanzisha kampuni yake akijifanya contractor wa mambo ya umeme ikamshinda, akakimbilia Zanzibar nako akashindwa na hicho kikampuni chake.
5. Alirudi bara na kujiingiza kwenye siasa.
6. Aligombea ubunge katika jimbo la Temeke kupitia CUF kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 na kushindwa vibaya.
7. Kaimu mkurugenzi wa umbeya wa chama cha majambazi (mwanzoni cheo hicho hakikuwepo sasa sijui anakaimu nini)

Hayo ndiyo niyajuayo mimi kuhusu huyu mmbea.
 
Hicho cheo cha Mkurugenzi wa Propaganda mhhh!! Katika watu amabao wanatumika CCM mmojawapo ni huyu huwa hafikiri anayoyaongea ili mradi mkono uende kinywani na afurahishe mafisadi
 
Nani asiyejua Tambwe Hizza mganga njaa na nyemelezi anayeweza kurukia chama chochote ili mkono uende kinywani ni mgumu wa kujifunza, sijui ni kutokuwa na uelewa na elimu ndogo au kuzidi kujipendekeza ili aongezewe malipo yatokanayo na mabaki ya ufisadi??

Hivi karibuni alikaririwa akimshambulia Katibu wa CHADEMA Slaa (PhD) akisema 'ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba kiongozi huyo (Slaa) amepandwa na wazimu, alichobakiza ni kuvua nguo...amechanganyikiwa na ndiyo maana anatapatapa kutafuta lolote la kusema'

Tuwe wakweli jamani, hivi kati ya Dk Slaa aliyemtingisha hata bosi wake Jakaya Kikwete na KIDAMPA kama Hizza nani anakaribia kuvua nguo?? Nani hajui kuwa Hizza alijivua nguo alipojiunga na CUF na kutimua baada ya kushindwa ubunge??

Kwanza sijui kama maneno hayo ni ya Hizza au Martin Shhigella au Salva Rweyemamu ambao sawa na Hizza wameonyesha uhuni haumtoki mtu ukishamuingia....maana uhuni ni uhuni hata kama anayefanya anatetea ikulu au chama tawala.

Kuna haja ya kujiuliza ni kwa nini Hizza anatetea madaraka Chamani. Nadhani ingawa CCM imekuwa ikishutumu vyama vingine ukabila, Hizza anafanya hivi kutokana na kuwekwa alipo na mtu wa kabila lake Yusuf Makamba ambaye baada ya kumpachika mwanaye serikalini na chamani ameonyesha wazi anavyotumia madaraka yake kwa ajili ya familia na hata kabila lake.

Niliwahi kumtaka Hizza na Makamba wanipe vigezo vitatu tu vya kufungua ofisi ambayohata kwenye katiba ya CCM haimo, ya propaganda, bahati mbaya kutokana na ukweli na uzito wa hoja yenyewe waliingia mitini na kunywea.

.........Ndio, Mbwa ili alipwe lazima awinde au hata kubweka kama afanyavyo Hizza. Ila kwa umri wake huku ni kuchelewa kukomaa kiakili na kisifa kama mwanaume.

kwa nini Hiza haoni ukichaa wa mjomba wake aliyechekelea mauaji ya Arusha asijue kila mtu atakufa? MBONA CHADEMA HAWAKUCHEKELEA KUANGUKA ANGUKA HOVYO KWA MWENYEKITI WAKE?

Laiti angekuwa na elimu lau akatumia busara kujua hata mambo madogo ya kisheria lakini hakuna haja ya kumshangaa au kumwonea Hiza kutokana na SHULE KUMPIGA CHENGA na hii ndio maana hata hiyo ofisi ya propaganda na zile za wilaya zimejaa vihiyo wasio na usomi wala busara.


Hivi kati ya bosi wake Hiza na Slaa nani anakaribia kuokota makopo? Arejee anavyosakamwa kukisambaratisha chama kutokana na kupayuka hovyo huku huku akiwatumia wahuni na vihiyo kama Hizaza kuchafua hewa chamani.

Hizza amesahau kuwa kampeni zimeisha hata waganga njaa wenzake akiwemo yule MTABIRI MWONGO na mashehe wengine njaa bila kusahau maaskofu njaa wamejua kuwa wakati wa kugeuzana mradi umepitwa na wanachoongea kinafuatiliwa kwa makini!

Je! Kwanini CCM wanapenda kumtumia Hizza na si watu wenye akili angalau na mashiko hata kama ni mafisadi?

Wengi wanajua Hizza baada ya kuukosa Ubunge na kuwa na kisomo kidogo kiasi cha kutoweza kuajiriwa alijirejesha CCM kama mbwa koko afanyavyo baada ya kudokoa kwa aliyemfuga? Siku zote nimekuwa nikitahadharisha kuhusiana na siasa za ukuku, ufisi na umbwa, Kuku hula asicho zalisha na hUZALISHA ASICHOKULA, HIZZA ANAKULA PESA YA WALIPA KODI NA ANAZALISHA MIGONGANO.

Kama tungekuwa hatuna adabu kama Hiza basi tungemshambulia mwenyekiti wake kutokana na kuishiwa hadi hata umoja wa watoto wa chama chake kuanza kutoa matamko makali baada ya mumwona kimya na hafai hata kidogo.

Kwa nini Hizza hashupalii Dowans? Kwa sababu hawezi kukata mkono unaomlisha yeye na bosi wake na yule mhuni mwenzie wa Ikulu.

Bwana Hizza kama propaganda zimewkushinda si uende kwenu Lushoto kujifunza lau uganga kuliko huo uganga njaa?Hivi siku mjomba wako akitimuliwa utaondoka naye kama mwana wa kufikia au utadandia chama gani?

Watanzania mdharau Hizza ...............isitoshe angekuwa amekwenda jando kichwani na si kukeketwa basi tungemchukulia kwa uzito wa ziada............


NKWAZI MHANGO

DIRA YA MTANZANIA TOLEO NAMBA 070 UK 17

 
Back
Top Bottom