Tambua wakati mzuri wa kutafuta mwanamke wa maisha!

Sio zama hz aisee, unamkubali mwanaume hana kitu, unamsaport kwa kila hali, hela za nauli za kwenda kwny interview unamtafutia hata kwa kukopa, unamsaidia kutafuta matangazo ya kazi, kuaply, kusaka vibarua huku na huku, lkn akishainuka na kupata ajira na hela basi wewe unaonekana screpa!!! Anaanza kushoboka na wavaa mawigi wanaojua kujichubua na kutumia hela wasizozitafuta!!!! Mwisho wa siku anakubwaga kweupe na kashfa juu ati wewe sio hadhi yangu...wasengerema kweli hawa viumbe.
ayaaaaaaaa! wewe
 
Wanaume hamna maana mtu anakukubalia ukiwa na hali ngumu lakini pindi mkahangaika wote mkapata, mnaanzaga kutafuta anaejua matumizi. Yule wa shida anawekwa pemben kwanza fedha zinatumika na yule aliekuta zipo tayari. Sasa ya nini kuvumilia tabu za m'ume, aiseee ajipange tu kwanza. Na mwanaume usipokuwa vizur una asilimia 80% ya kuchapiwa...
 
Ntakuvumilia wakati wa shida ....tutasota hatimae utafanikiwa.....ukifanikiwa unaanza kuniona mi si lolote si chochote ...unaanza kuniona nimefanana na mbuzi unaanza kuhangaika na wanawake wengine ....my dear brother pambana usake mahela tukutane juu kwa juu hakuna MTU anapenda stress za baadae
 
Wapo lakini wengi wao ni polygon kwa hali ya sasa watoto wazuri utaishia kuwaita shemeji na ukizifuma yule aliyekuvumilia utamuona km Mzee na jinsi mlivyo wanaume ukiwa vizuri kiuchumi basi hata kula utataka ule vilivyonona ni hayo tu
Wewe hupendi vilivyonona? Anyway sikupanga kuchangia wewe umenifanya kuchangai kipindi nikiwa sina kitu kuna wadada walionivutia Sana kila mmoja Kwa kipindi chake nilifanikiwa kuwa nao wakinisapoti Kwa kila kitu lakini ghafla nilipoa anza kupata neema ya kuwa na vijisenti mfukoni wakinipiga chini wote nakila kinipiga nao story nikijalibu kuwauliza ni kitu gani kulichofanya mpaka wakanipotezea hawana majibu nikauliza ushawai kuniona na mwanamke mwingine, au kuna baya lolote nililokufanyia,nimekuzarau,nimshindwa kukutimizia kitu ulichotaka,nimepunguza muda wakuonana na wewe au kuna baya lolote nimekufayia jibu ni hapana kiukweli nimeahindwa kujua nini wanawake mnataka.
 
Kiukweli mwanamke anaekupenda na kukuthamini ukiwa huna kitu hasa ktk hii hali ya vyuma kukaza nindio chaguo bora tatizo linakuja wewe unamuona kimuonekano hakuvutii sasa hapo ndo unapofeli.
Wakati mkipat mnawasahau wale mlioanz nao shidani
 
Back
Top Bottom