Tambua vituo vitano vya treni vinavyovutia duniani

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,084
Habari ya mchana wanandugu, natumaini mnaendelea Vyema sana Pole zangu kwa wagonjwa. Kama ilivyo Kawaida yangu ni vyema kwangu kuwaletea makala mbalimbali zinazotuongezea ufahamu na udadisi wa namna Dunia yetu ilivyo.
Leo nitazungumzia masuala mazima kuhusu vituo vya treni au gari moshi duniani.
Nilipata wazo hili mara baada ya kuona design ya vituo vya treni yetu ya Tanzania pamoja na mazingira yake.
IMG_1183.jpg

nimechakata ubong na kujiuliza je katika sekta ya usafiri wa reli duniani; ni vituo gani vilivyo na hadhi ya nyota tano kubwa na ya kipekee.
Ni suala lisilopingika kuwa wenzetu wazungu kwenye bara la Amerika pamoja na Ulaya wamepata maendelo makubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo usafirishaji.
IMG_1155.jpg

Kituo cha treni nchini kwetu Tanzania.

IMG_1156.jpg

Kituo cha treni nchini Ufaransa.
NB: Sina nia mbaya yoyote ya kubeza maendeleo ya taifa langu kwa namna yoyote bali ni kuona tu namna gani sehemu zingine zina maendeleo kuzidi maendelo yetu.
Sekta ya usafirishaji haswa reli ni Moja kati ya sekta kubwa kwenye maendeleo Kwani mizigo na watu husafiri kutumia reli.
Pia ni wazi suala la mandhari na mazingira ya vituo huweza kuchochea watu kupendelea au kutokupendelea kusafiri kwa treni.
Hivyo basi leo nitakuletea vituo vitano duniani ambavyo kwa maoni yangu Ndio vituo vya treni vinavyovutia zaidi.
IMG_1157.jpg

Naomba nieleweke kuwa uzi huu sio kwa ajili ya kubeza maendeleo ya nchi yoyote.... Na hauna maoni ya kiitikadi ya chama chochote lengo ni kujifunza tu.

Namba 5. KITUO CHA TRENI CHA ATOCHA – MADRID, UHISPAINA:
IMG_1158.jpg

Hakika kwangu hichi kituo ndo namba tano kwa ubora, sio tu kwa sababu kina majengo mazuri lakini usanifu wa majengo yake umekifanya kiwe ni kituo kizuri nje mpaka ndani. Hii ni kazi safi kutoka kwa wanamichezo majengo wawili; Bwana Alberto de Palacio Elissagne pamoja na Bwana Gustave Eiffel.
Ndani ya kituo hiki kuna bustani ya miti zaidi ya elfu nne, mimea zaidi ya Mia tano, aina za samaki zaidi ya hamsini pamoja na maduka makubwa, migahawa bila kusahau sehemu ya kula bata usiku. Ni kituo chenye uzuri wa kipekee.
IMG_1159.jpg

Uingiapo ndani ya kituo hiki ni kama umeingia ndani ya kivutio cha asilia kwani wakati utakapokuwa unapiga misele kusubiria usafiri wako; unaweza kushangaa urembo na usanifu maridadi wa jengo hili linalopatikana ndani ya jiji la Madrid.
IMG_1160.jpg

Kwangu hiki ni kituo kinachovutia zaidi duniani; na kwa heshima nimekipa nafasi ya tano.

Namba 4. KITUO CHA TRENI CHA ANTWERP- ANTWERP, UBELIGIJI:
IMG_1161.jpg

Utundu na makeke ya wasanifu majengo ndo yamekifanya kituo hiki kiwe na unadhifu wa kiwango hiki. Ni kazi ya msanifu Louis Delacenserie ambaye alitengeza paa la kufunikia jumba hili huku akikusanya zaidi ya aina ishirini za marumaru na mawe kisha kutengeneza kioo kikubwa cha kuvutia chenye kuruhusu mwanga kuchomoza na kutoa rangi nzuri kwenye kila kona na pembe ya jengo.

IMG_1162.jpg

Katika purukushani za vita ya Pili ya dunia, jengo hili lilipata kuharibiwa na mabomu ya Ujerumani. Lakini lilifanyiwa marekebisho na kurudi kwenye hali yake ya mwanzoni.
Kituo hiki ni namba nne kwangu.
IMG_1163.jpg

Namba 3. KITUO CHA MTAKATIFU PANCRAS – LONDON, UINGEREZA:
IMG_1165.jpg

Kituo hiki cha Mtakatifu Pancras ni Kituo cha kimataifa cha Treni Kwani ndivyo kinachounganisha nchi mbalimbali za Bara la Ulaya. Mfano: Ufaransa, Ujerumani, Ureno na kadhalika. Kwa sasa kina zaidi ya Miaka Mia moja na hamsini na tatu. Na ni Moja kati ya alama jiji la New York.
IMG_1166.jpg

Humu ndani kunapatikana kila aina ya maduka ya bidhaa, kuna kumbi za starehe zaidi ya kumi zenye hadhi ya nyota tano.
IMG_1167.jpg

Namba 2. KITUO CHA AMSTERDAM CENTRAAL STATION – AMSTERDAM, UHOLANZI:
IMG_1172.jpg

Ni kituo kinachopatikana ndani ya jiji la Amsterdam mkabala na Makumbusho maarufu ya wadachi. Usanifu wa Bwana Pierre Cuyper ndo umeifanya Uholanzi kuwa na kituo cha treni nadhifu.
IMG_1175.jpg

Pia Kituo hiki kimepewa hadhi ya kuwa urithi wa taifa nchini Uholanzi.
IMG_1174.jpg

Namba 1. KITUO CHA TRENI CHA GRAND CENTRAL TERMINAL – NEW YORK MAREKANI (USA):
IMG_1176.jpg

Kwa Hakika orodha hii haitokamilika wala kuitendea haki kama sitoweka kituo hiki. Ni eneo la Sita kidunia kwa kuvutia watu na watalii.
IMG_1177.jpg

Ni jengo lililokamilika kutengeneza mnamo mwaka 1913. Lina kila huduma ya kijamii ambayo mtu anapaswa kupata.
IMG_1178.jpg

Hivi ni vituo vitano bora kwangu. Je Afrika hatuwezi kufikia hatua hizi kama wenzetu? Kidogo nchini Morocco.
Gare Casablanca Port, Morocco
IMG_1179.jpg

IMG_1180.jpg

Pamoja na Gare Marrakech, Morocco
IMG_1182.jpg

IMG_1181.jpg

Naomba kuwasilisha uzi.....
Kama kuna sehemu nimekosea; Naomba nirekebishwe .
Cc Damaso @Mshana_Jr
 
Attachments

  • IMG_1170.jpg
    IMG_1170.jpg
    74 KB · Views: 4
Sisi cha kwanza kabisa hatujui kutunza unakuta mtu kaandika katika ukuta akumbukwe fulani.

Pia fikiria mtu anaiba vioo vya madirishani yani sisi bado mno acha tuendelee tu hivyo hivyo.
 
Unachokisema ni ukweli na sahihi Kabsa mkuu. Hatuna utamaduni mzuri wa kutunza Mali Kabsa Waafrika
 
Habari ya mchana wanandugu, natumaini mnaendelea Vyema sana Pole zangu kwa wagonjwa. Kama ilivyo Kawaida yangu ni vyema kwangu kuwaletea makala mbalimbali zinazotuongezea ufahamu na udadisi wa namna Dunia yetu ilivyo.
Leo nitazungumzia masuala mazima kuhusu vituo vya treni au gari moshi duniani.
Nilipata wazo hili mara baada ya kuona design ya vituo vya treni yetu ya Tanzania pamoja na mazingira yake.
View attachment 1710956

nimechakata ubong na kujiuliza je katika sekta ya usafiri wa reli duniani; ni vituo gani vilivyo na hadhi ya nyota tano kubwa na ya kipekee.
Ni suala lisilopingika kuwa wenzetu wazungu kwenye bara la Amerika pamoja na Ulaya wamepata maendelo makubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo usafirishaji.
View attachment 1710860
Kituo cha treni nchini kwetu Tanzania.

View attachment 1710861
Kituo cha treni nchini Ufaransa.
NB: Sina nia mbaya yoyote ya kubeza maendeleo ya taifa langu kwa namna yoyote bali ni kuona tu namna gani sehemu zingine zina maendeleo kuzidi maendelo yetu.
Sekta ya usafirishaji haswa reli ni Moja kati ya sekta kubwa kwenye maendeleo Kwani mizigo na watu husafiri kutumia reli.
Pia ni wazi suala la mandhari na mazingira ya vituo huweza kuchochea watu kupendelea au kutokupendelea kusafiri kwa treni.
Hivyo basi leo nitakuletea vituo vitano duniani ambavyo kwa maoni yangu Ndio vituo vya treni vinavyovutia zaidi.
View attachment 1710865
Naomba nieleweke kuwa uzi huu sio kwa ajili ya kubeza maendeleo ya nchi yoyote.... Na hauna maoni ya kiitikadi ya chama chochote lengo ni kujifunza tu.

Namba 5. KITUO CHA TRENI CHA ATOCHA – MADRID, UHISPAINA:
View attachment 1710867
Hakika kwangu hichi kituo ndo namba tano kwa ubora, sio tu kwa sababu kina majengo mazuri lakini usanifu wa majengo yake umekifanya kiwe ni kituo kizuri nje mpaka ndani. Hii ni kazi safi kutoka kwa wanamichezo majengo wawili; Bwana Alberto de Palacio Elissagne pamoja na Bwana Gustave Eiffel.
Ndani ya kituo hiki kuna bustani ya miti zaidi ya elfu nne, mimea zaidi ya Mia tano, aina za samaki zaidi ya hamsini pamoja na maduka makubwa, migahawa bila kusahau sehemu ya kula bata usiku. Ni kituo chenye uzuri wa kipekee.
View attachment 1710871
Uingiapo ndani ya kituo hiki ni kama umeingia ndani ya kivutio cha asilia kwani wakati utakapokuwa unapiga misele kusubiria usafiri wako; unaweza kushangaa urembo na usanifu maridadi wa jengo hili linalopatikana ndani ya jiji la Madrid.
View attachment 1710872
Kwangu hiki ni kituo kinachovutia zaidi duniani; na kwa heshima nimekipa nafasi ya tano.

Namba 4. KITUO CHA TRENI CHA ANTWERP- ANTWERP, UBELIGIJI:
View attachment 1710877

Utundu na makeke ya wasanifu majengo ndo yamekifanya kituo hiki kiwe na unadhifu wa kiwango hiki. Ni kazi ya msanifu Louis Delacenserie ambaye alitengeza paa la kufunikia jumba hili huku akikusanya zaidi ya aina ishirini za marumaru na mawe kisha kutengeneza kioo kikubwa cha kuvutia chenye kuruhusu mwanga kuchomoza na kutoa rangi nzuri kwenye kila kona na pembe ya jengo.

View attachment 1710884

Katika purukushani za vita ya Pili ya dunia, jengo hili lilipata kuharibiwa na mabomu ya Ujerumani. Lakini lilifanyiwa marekebisho na kurudi kwenye hali yake ya mwanzoni.
Kituo hiki ni namba nne kwangu.
View attachment 1710888

Namba 3. KITUO CHA MTAKATIFU PANCRAS – LONDON, UINGEREZA:
View attachment 1710893
Kituo hiki cha Mtakatifu Pancras ni Kituo cha kimataifa cha Treni Kwani ndivyo kinachounganisha nchi mbalimbali za Bara la Ulaya. Mfano: Ufaransa, Ujerumani, Ureno na kadhalika. Kwa sasa kina zaidi ya Miaka Mia moja na hamsini na tatu. Na ni Moja kati ya alama jiji la New York.
View attachment 1710898

Humu ndani kunapatikana kila aina ya maduka ya bidhaa, kuna kumbi za starehe zaidi ya kumi zenye hadhi ya nyota tano.
View attachment 1710900

Namba 2. KITUO CHA AMSTERDAM CENTRAAL STATION – AMSTERDAM, UHOLANZI:
View attachment 1710920

Ni kituo kinachopatikana ndani ya jiji la Amsterdam mkabala na Makumbusho maarufu ya wadachi. Usanifu wa Bwana Pierre Cuyper ndo umeifanya Uholanzi kuwa na kituo cha treni nadhifu.
View attachment 1710933

Pia Kituo hiki kimepewa hadhi ya kuwa urithi wa taifa nchini Uholanzi.
View attachment 1710938

Namba 1. KITUO CHA TRENI CHA GRAND CENTRAL TERMINAL – NEW YORK MAREKANI (USA):View attachment 1710941

Kwa Hakika orodha hii haitokamilika wala kuitendea haki kama sitoweka kituo hiki. Ni eneo la Sita kidunia kwa kuvutia watu na watalii.
View attachment 1710947

Ni jengo lililokamilika kutengeneza mnamo mwaka 1913. Lina kila huduma ya kijamii ambayo mtu anapaswa kupata.
View attachment 1710948

Hivi ni vituo vitano bora kwangu. Je Afrika hatuwezi kufikia hatua hizi kama wenzetu? Kidogo nchini Morocco.
Gare Casablanca Port, Morocco
View attachment 1710949
View attachment 1710950

Pamoja na Gare Marrakech, Morocco
View attachment 1710951
View attachment 1710952

Naomba kuwasilisha uzi.....
Kama kuna sehemu nimekosea; Naomba nirekebishwe .
Cc Damaso @Mshana_Jr
Saint Pancreas London Landmark ya New York!
 
Helsink railway station Finland
HELSINK CENTRAL RAILWAY STATION.jpg
HELSINK CENTRAL RAILWAY STATION.jpg
HELSINK CENTRAL RAILWAY STATION.jpg
 
Back
Top Bottom