Tambua uwepo wa dhahabu katika eneo lako

The_Geo

New Member
Jan 6, 2017
1
2
Habari wakuu,

Nikiwa natambua kuna watu ambao wana maeneo yao ambayo pengine wameambiwa kwamba yana uwezekano wa kuwa na dhahabu au wanahisi tu kwamba kuna dhahabu. Hapa nitaelezea viashiria baadhi ambavyo vinaweza kukujulisha kama eneo lako linaweza kuwa na dhahabu au la.

Kwanza tutambue kuwa utafutaji wa dhahabu unapitia mchakato mkubwa ambao unatumia jopo la wataalam(wajiolojia) na vifaa vya kisasa hadi kukamilika. Kifupi hupitia ramani za kijiolojia,jiofizikia, jiokemia pamoja na hatua ya uchimbaji(drilling) ambayo hiyo hutoa uhakika wa taarifa za awali.

Maelezo haya yatakuongezea uhakika wa uwepo wa dhahabu katika eneo lako kabla ya kumwona mjiolojia. Na hivi ndivyo viashiria awali,

  1. Eneo kuwa na rangi tofauti na maeneo yanayolizunguka.
Mara nyingi dhahabu huambatana na vimiminika vizito vya moto(hydrothermal fluids) kutoka chini sana ya dunia. Vimiminika hivi ndivyo hubeba dhahabu hadi sehemu ya karibu na dunia pamoja na madini mengine mfano:shaba. Ujio huu huathiri hali ya asili ya eneo hilo hivyo tabaka la juu la eneo hubadilika.

2.Miamba inayozunguka eneo hilo kuwa na mikanda/michirizi mingi meupe-silica (Quartz veins).
Dhahabu huambatana na madini ya silika (quartz) wakati wa mtengenezo ambayo huonekana kama mikanda/michirizi meupe katika miamba ya eneo lako.

3.Miamba ya juu katika eneo lako kutengeneza (weathering) rangi ya kutu ya njano au nyekundu.=Gossan formation
Hii hutokana na madini ya sulfide ya chuma(pyrite) ambayo huambatana na dhahabu wakati wa mtengenezo(auriferous ferrogenous sulfide). Madini haya yakiwa juu ya uso wa dunia huchuja(leaching) na kuruhusu sulfide iende chini ya ardhi na kubakisha madini chuma ambayo kwa sababu ya kiwango kikubwa cha oksijeni juu ya ardhi, hupata kutu ambayo hutengenezeka katika miamba. Kutu hii ikizidi mwamba huweza kuwa mlaini sana kiasi cha kumeguka kwa mkono.

Kwa leo tujifunze hivi, mda mwingine nkipata ntaelezea zaidi kuhusu dhahabu na madini mengine. Nimeambatanisha picha baadhi kwa uelewa mzuri.

Angalizo: Sio kila kiashiria nilichokiandika hapa lazima kionekane katika eneo lako, dhahabu hutegemea jinsi ilivyotengenezeka. ukiona huelewi vizuri, muone Mjiolojia kwa msaada zaidi
 
Attachments

  • quatz vein.jpg
    quatz vein.jpg
    10.2 KB · Views: 529
  • rusted basalt -0003.jpeg
    rusted basalt -0003.jpeg
    15.2 KB · Views: 569
  • the _Geo.jpg
    the _Geo.jpg
    10.5 KB · Views: 560
watu wa kanda ya ziwa wasogee hapa faster, sisi wa kaskazini hatunaga mazahabu
 
Habari wakuu,

Nikiwa natambua kuna watu ambao wana maeneo yao ambayo pengine wameambiwa kwamba yana uwezekano wa kuwa na dhahabu au wanahisi tu kwamba kuna dhahabu. Hapa nitaelezea viashiria baadhi ambavyo vinaweza kukujulisha kama eneo lako linaweza kuwa na dhahabu au la.

Kwanza tutambue kuwa utafutaji wa dhahabu unapitia mchakato mkubwa ambao unatumia jopo la wataalam(wajiolojia) na vifaa vya kisasa hadi kukamilika. Kifupi hupitia ramani za kijiolojia,jiofizikia, jiokemia pamoja na hatua ya uchimbaji(drilling) ambayo hiyo hutoa uhakika wa taarifa za awali.

Maelezo haya yatakuongezea uhakika wa uwepo wa dhahabu katika eneo lako kabla ya kumwona mjiolojia. Na hivi ndivyo viashiria awali,

  1. Eneo kuwa na rangi tofauti na maeneo yanayolizunguka.
Mara nyingi dhahabu huambatana na vimiminika vizito vya moto(hydrothermal fluids) kutoka chini sana ya dunia. Vimiminika hivi ndivyo hubeba dhahabu hadi sehemu ya karibu na dunia pamoja na madini mengine mfano:shaba. Ujio huu huathiri hali ya asili ya eneo hilo hivyo tabaka la juu la eneo hubadilika.

2.Miamba inayozunguka eneo hilo kuwa na mikanda/michirizi mingi meupe-silica (Quartz veins).
Dhahabu huambatana na madini ya silika (quartz) wakati wa mtengenezo ambayo huonekana kama mikanda/michirizi meupe katika miamba ya eneo lako.

3.Miamba ya juu katika eneo lako kutengeneza (weathering) rangi ya kutu ya njano au nyekundu.=Gossan formation
Hii hutokana na madini ya sulfide ya chuma(pyrite) ambayo huambatana na dhahabu wakati wa mtengenezo(auriferous ferrogenous sulfide). Madini haya yakiwa juu ya uso wa dunia huchuja(leaching) na kuruhusu sulfide iende chini ya ardhi na kubakisha madini chuma ambayo kwa sababu ya kiwango kikubwa cha oksijeni juu ya ardhi, hupata kutu ambayo hutengenezeka katika miamba. Kutu hii ikizidi mwamba huweza kuwa mlaini sana kiasi cha kumeguka kwa mkono.

Kwa leo tujifunze hivi, mda mwingine nkipata ntaelezea zaidi kuhusu dhahabu na madini mengine. Nimeambatanisha picha baadhi kwa uelewa mzuri.

Angalizo: Sio kila kiashiria nilichokiandika hapa lazima kionekane katika eneo lako, dhahabu hutegemea jinsi ilivyotengenezeka. ukiona huelewi vizuri, muone Mjiolojia kwa msaada zaidi
Je mawe ya aina hii ni viashiria vya madini aina gani mkuu?
 
Hiyo ni ya elimu ya kukariri ya darasani sisi huku kijijini nikagundua dhahabu kirahisi bila hayo yote uliyoyataja, njoo huku upate elimu ya kiasili
 
Back
Top Bottom