Tambua siri ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari

Nkingwamh

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
290
210
Wapendwa kwanza kabisa poleni na majukumu ya wiki zima. Kutokana na kichwa hapo juu.Nianze moja kwa moja kwa kuwapongeza madaktari wenye moyo wa huruma na wakujitolea kuelimisha jamii juu ya elimu ya ugonjwa huu hatari kwakua mengi yamekwishasemwa na madaktari humu,Mimi Leo sioni haja ya kueleza kisukari ni nini,kwani ninatambua wengi mnafahamu.

Sasa niende moja kwa moja kwenye sababisho la ugonjwa huu. Wapendwa mwili unavyouita ndivyo utavyoitika.Mwili umeumbwa kwa seli nyingi sana,na seli ndizo zinazoufanya mwili uweze kutekeleza majukumu yake mbalimbali ya kila siku.Naseli haziwezi kufanya kazi bila wewe muhusika kuulisha mwili wako wanga,wanga ndio chanzo kikubwa cha umeme mwilini.

(electrolytes).unapokula chakula cha wanga mwili huvunja wanga na kupata sukari aina ya monosakaridi yenye viwango vya namba hizi C6 H12 O6 ambayo molyekuli yake ni sawa na mwili unavyo hitaji.Sasa ikitokea mwili ukaulisha sukari yenye namba tofauti na hizo,kitachotokea hapo ni kwamba mwili utaangalia sukari ya akiba yenye namba hiyo ambayo iliohifadhiwa na mwili ndio itayotumika kuzalisha umeme.wakati ile ambayo yenye namba kubwa haitotumika hadi kwanza ivunjwe vunjwe iwe na namba C6 H12 O6.

Sukari yenye namba hiyo inapokutana na Sodiam chloride Pamoja na Patasiam ndio inatengeneza umeme wa mwili.Na umeme ukitengenezwa unakuja kutumiwa na mwili, kwa kuzalisha nguvu, na kuziendesha ogani mbalimbali mwilini kama vile ubongo moyo figo na tezi Mbalimbali ambazo zinahitaji umeme ili zifanye kazi. kadiri nguvu za mwili zinapozalishwa na tezi zinapoutumia umeme huu ndivyo sukari hii inavyopungua.na kadiri sukari inavyopungua ndivyo mwili unavyo hitaji sukari iingietena mwilini.

INAKUAJE UGONJWA UNATOKEA.

Wapendwa hapa naomba mtulize macho ili msome kwa umakini.kile kitendo cha kula vyakula vyenye sukari zenye namba mbili tofauti ( C6 H12 O6 na C12 H22 O11)ndicho kinachosababisha ugonjwa wa kisukari.Unapokula mchanganyiko huo,kinachotokea hapo ni kwamba sukari ilio na namba inayotakiwa na mwili ndio itayotumika na mwili,halafu ile ambayo namba yake ni kubwa itaachwa na kusubiri ivunjwevunjwe. Na kabla haijavunjwa wewe tayari ushakula chakula chenye sukari zenye namba zote mbili.

Kitachotokea tena ni kutumiwa sukari ile ambayo namba yake inayotakiwa, wakati ile ambayo yenye namba tofauti.itaisababisha ile ambayo iliokua ikivunjwa iachwe na kwenda kutupwa nje ya seli.kitendo hiki cha kutupwa sukari nje seli tena bila kuvunjwavunjwa husababisha seli kuziba, yaani hapo sukari ile ambayo haijavunjwa ikikaa juu ya tundu la seli sukari hiyo huwa gundi.

Gundi hiyo husababisha seli zishindwe kufungua matundu ili kutumia sukari sahihi.Kwa hiyo hapo hata ile sukari yenye namba sahihi haitotumika tena.Na hapo ndipo sukari inapoanza kukusanyika kwenye damu bila ya wewe kujua Na ikikusanyika kwenye damu.

Kongosho nalo linakua busy mda wote kutengeneza Homoni iitwayo insulin.ambayo kazi yake ni kuitoa sukari iliozidi.Pia kitendo hiki cha kongosho kua busy mda wote.husababisha kuchoka kongosho lenyewe na kushindwa kutoa homoni ambayo itaiondoa sukari iliozidi. Na kongosho likiwa limekufa sasa insulin inabidi itumike bandia.ambayo mgonjwa hupewa hospitali.hapo sasa mtu tunasema kisha kua mgonjwa wa kisukari na ni mteja wa insulin.

Pia tutambue kua ugonjwa unapoanza huanza kimya,na ikibainika mtu anatatizo basi huyo atakua ni mteja wa dawa za kupunguza sukari iliozidi kwenye damu.Lakini ikibainika kongosho limekufa hapo inabidi uwe mteja wa insulin.

UTAJUAJE KUA UMEKULA SUKARI NAMBA MBILI TOFAUTI.

Wapendwa ni kwamba chakula tunavyokula siku zote ni mpango au utaratibu tuliojiwekea.Tambua hili asubuhi unapoamka unakunywa chai yenye sukari, sukari hiyo iliowekwa kwenye kikombe cha chai ni Disakaridi yenye namba C12 H22 O11 ambayo ni kubwa. Na hapohapo unatafunia Viazi vitamu,ama wali.ambavyo hivi ni wanga.

Hapo vitavyoanza kutumia na mwili ni wali na viazi vitamu, chai itasubiria ivunjwe na kabla haija malizika kuvunjwa chakula cha mchana kimefika ambavyo Mara nyingi hua ni wanga ambayo ni Polisakaraid .ambavyo inaweza ikawa Ugali ama wali.Hapo ilechai uliokunywa mwanzo mwili itabidi usiangaike Nayo kuivunja hivyo itatupwa juu ya seli.

Tendo hilo likifanyike Mara miaka kadhaa jibu lake unafikiria litakua ni nini.majibu najua tunayo.Na kuna wakati mtu anakula maandazi au vitumbua hata kama asipokunywa chai ni lazima hapo kitachoanza kufanyiwa kazi ni ngano au mchele ile sukari iliowekwa humo itaachwa na itatupwa juu ya seli.Pia tukumbuke sukari inapokusanyika mwilini husababisha kuya shika mafuta mafuta mwilini na kuyakusanya hivyo kumfanyamtu kunenepa TIPWATIPWA na hilo nalo ni tatizo.

Wapendwa tufanye kinga kabla ya kutibu.mungu anasema watu Wangu wanaangamia kwa kukosa maalifa.sasa maarifa haya hapo tuyatumie tena bure.Maisha pasipo kuangamia kwa ukosefu wa maarifa inawezekana.
 
Toa mapendekezo ya namna ya kuzuia tatizo!
Ni kwamba tujitahidi kua wastaarabu wa kula vyakula.kama unakunywa chai yenye sukari ya kawaida,kunywa yenyewetu.Ama kama unakunywa chai yenye sukari ya kawaida ambatanisha na chakula chenye Protini.Ama unapokula chakula cha wanga ambatanisha na chakula cha Ptotini.Kutumia chakula cha wanga na chai kwa wakati mmoja kitachowahi kuvunjwa ni wanga,kisha sukari ilioko kwenye chai kuvunjwa taratibu.Pia tujitahidi kuilisha miili yetu sukari ambayo itaingia mojakwamoja katika utendaji kazi pasipo kuuchosha mwili kuvunjavunja kwa mda mrefu.
 
Kwa maelezo yako ina maana kwa asubuhi kunywa chai na vitafunwa mathalan chapati,maandazi,mkate_viazi ni kosa la kila cku ambalo tunalifanya kipi,ni salama ktk milo yetu
 
Kwa maelezo yako ina maana kwa asubuhi kunywa chai na vitafunwa mathalan chapati,maandazi,mkate_viazi ni kosa la kila cku ambalo tunalifanya kipi,ni salama ktk milo yetu
Mkuu salama ni kunywa chai pekee, kisha kukaa muda mrefu kama Massa mawili ama matatu ili sukari uliokula katika chai ivunjwe ndipo ule chapati na viazi.Maandazi hapo usile kwakua yanasukari ambayo sio sahihi, ama kama utaamua kula maandazi kula na ukae mda kama Masaa mawili ama matatu ili sukari uliokula katika maandazi ivunjwe, chapati na viazi hapo usile kwakua ukila utasababisha sukari ilioko kwenye maandazi kushindwa kuvunjwa.
 
Dawa ya Kisukari ni kupiga zoezi tu.
Mkuu kupiga zoezi ni kufanya seli za mwili zikutengenezee nguvu, na zinapotengeneza nguvu zinaitumia sukari hivyo uko sawa kabisa,ila kua na utaratibu katika Milo ni vizuri zaidi ili kupunguza mzigo wakazi katika kongosho
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom