Tambua kila mtu anamatatizo usione anatabasamu usoni

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
TAMBUA KILA MTU ANA MATATIZO USIONE ANA TABASAMU USONI

Kuna wakati ambao unakuwa na matatizo mengi sana kwenye maisha yako na kufikiri kwamba kama ungekuwa kama mtu fulani huenda usingekuwa na matatizo.

Labda huna kazi, unafikiri kama ungekuwa na kazi kama watu unaowaona wana kazi basi maisha matatizo yako yangekwisha.

Labda wewe ni mfanyakazi wa kawaida na unafikiria kwamba kama ungekuwa boss basi matatizo yako yote yangeisha.

Au unafanya biashara na kuona biashara yako haiendi vizuri, unafikiria kama ungekuwa unafanya biashara wanazofanya wengine basi matatizo yako yangekwisha.

Unaweza kufikiria hivi utakavyo, lakini ukweli ni kwambaaa Kila mtu ana matatizo.
Unaweza kuona ukiwa na kazi hutakuwa na matatizo, lakini wafanyakazi wengi sana wana matatizo kuliko hata ambayo unayo wewe.

Unaweza kuona boss wako hana matatizo, ila ukweli ni kwamba anaweza kuwa na matatizo makubwa kuliko uliyonayo wewe.

Unaweza kuona biashara za wengine hazina matatizo kama unayopata wewe, ila ukipewa biashara hizo unaweza kukimbia kabisa. Kwa kuwa kila mtu ana matatizo kwa hiyo tufanyeje sasa?

Fanya hivi, acha kuangalia nani hana matatizo, acha kuangalia matatizo yako sana na anza kuangalia ni jinsi gani unaweza kuboresha maisha yako, ni jinsi gani unaweza kuyatyumia matatizo yako kuwa bora zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe, kwa maneno mengine ni kwamba, wakati wewe unataka kuwa kama yule, naye anataka kuwa kama wewe, mawazo yetu bi siri na usiposema hakuna atakayejua kwamba ungependa uwe yeye.
 
ni kweli kabisa, kama kila mtu angeamuwa ku express matatizo yake aliyeko nayo tungekimbiana.
 
Unaweza kuwa na matatizo ila huna shida na unaweza kuwa na shida ila ukawa huna matatizo
 
Last edited:
Ni kweli mi mwenyewe ukiniona usoni nina furaha sana lakini yaliyopo moyoni mola tu anajua
 
Okey...matatizo yana viwango.

Kuna matatizo ya kiafya..haya hayachagui tajiri au maskini na hatuchagui kuumwa sasa haya tusiyaweke hapa.

Lakini matatizo mengine yanatokana na maamuzi tuayoyafanya kila siku.

Mfano kukosa fedha huwezi mlaumu mtu kwa hili liko kwenye uwezo wako. ..wakati wewe Huna fedha wenzio wako bar wanazichezea so...shida nyingi ni our own creation
 
Okey...matatizo yana viwango.

Kuna matatizo ya kiafya..haya hayachagui tajiri au maskini na hatuchagui kuumwa sasa haya tusiyaweke hapa.

Lakini matatizo mengine yanatokana na maamuzi tuayoyafanya kila siku.

Mfano kukosa fedha huwezi mlaumu mtu kwa hili liko kwenye uwezo wako. ..wakati wewe Huna fedha wenzio wako bar wanazichezea so...shida nyingi ni our own creation
Well said brother..
 
Ahsante sana. Hata mtoa maada pia una matatizo yako mpaka kuandika matatizo ya wengine.
:)
 
Back
Top Bottom