Tambi za kuku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tambi za kuku

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 8, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  TAMBI ni chakula ambacho kina mapishi mengi kama ilivyo kwa mchele. Unaweza kupika kwa kuaanga, kwa nazi, mafuta na wakati mwingine hata kuchemsha. Vivyo hivyo, katika matumizi yake, wakati mwingine hutumika kama mlo kamili na kuna wakati hutumika kama saladi na kutosheleza kabisa mahitaji ya mlaji.

  Katika mapishi ya leo, nitakuletea namna ya kuandaa tambi kwa ajili ya chakula cha mchana. Tambi hizi hupikwa kwa kuchanganywa na kuku. Mahitaji Tambi robo kilo Kuku asiye na mifupa nusu kilo Kitunguu kimoja Karoti moja Hoho moja Kotmir fungu moja Nyanya kubwa tatu Chumvi kiasi Bizari kijiko kimoja cha chai Mafuta ya alizeti vijiko vinne vya mezani Tangawizi iliyotangwa kijiko kimoja cha mezani Namna ya kupika Chukua maji kiasi cha lita moja, weka chumvi kiasi na kisha weka jikoni.

  Acha yachemke na kisha tumbukiza tambi ndani yake. Weka mafuta kiasi cha vijiko viwili vya chakula weka kwenye sufuria hiyo, ili kuzuia tambi zisigandiane. Acha zichemke hadi ziive na kisha ipua chuja maji na weka pembeni. Chukua mafuta vijiko viwili vilivyobaki na kisha weka kwenye sufuria na injika jikoni. Anza kwa kukaanga vitunguu maji na baadaye tangawizi, karoti, vitunguu maji, binzari halafu weka vipande vya kuku na endelea kukaanga. Fanya hivyo hadi kuku pamoja na viungo vyake vitakavyokuwa na rangi ya hudhurungi.

  Katia hoho huku ukiendelea kukaanga. Weka chumvi kiasi na kisha katia nyanya. Funika na acha ziive vizuri. Baada ya dakika kama tano hivi funua na angalia kama kuna maji ya kutosha kuivisha kuku. Kama yatakuwa yamekauka kabisa ongeza maji kidogo na acha nyama ya kuku iive kabisa. Baada ya kuiva katia majani ya kotmir na baada ya muda kidogo ipua na weka pembeni. Chukua tambi ulizoweka pembeni na changanya na rosti lako la kuku. Pakua na weka mezani tayari kwa kuliwa. Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya. Email maikube@yahoo.co.uk
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Dec 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu Hii kitu safi sana, nashauri ungeiweka hapa. Mapishi Club
   
Loading...