TAMASHA la XXL Dodoma lagubikwa na simanzi, umati wamyoshea mabango waziri!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo kile kipindi cha XXL kilichokuwa kinaruka moja kwa moja toka Dodoma kimegeuka majonzi baada ya mamia ya vijana kunyoosha mabango yaliyoandika FREE ROMA

Watanganzaji walilazimika kubadili interview na kumwambia naibu waziri habari utamaduni na michezo Antony Mavunde kwamba hawawezi kupuuzia mabango waziri aseme chochote.

Naibu waziri akasema anasikitishwa na kitendo hicho lakini ana taarifa kwamba jeshi la polisi litatoa taarifa punde. Baada ya hapo kwenye segment ya hot 3 at 3 zimepigwa nyimbo mbili za ROMA ambapo umati umepagawa na kupiga mayowe.

Pia soma: Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara
 
Sijui kwanini kadri muda unavyozidi kwenda ndio naona kuna ugumu wa hawa watu kupatikana wakiwa hai!
Kwasababu wakiachiwa watasema walikuwa wapi?
Na huyo mtekaji atakuwa anaona atachukuliwaje?
Na alimteka kwa lengo lipi?

Eeee Mungu saidia vijana hawa huko waliko wawe hai
 
Waacheni waendelee na viburi vyao watakiona cha moto 2020.
Kwa nini tusubiri hadi 2020 wakati tukijua kuwa ndio wenyewe walioshika mpini. Tuhamasishane na kupinga ukatili na unyanayasaji kadri tunavyoweza bila kuvunja sheria - mfano maandamano, wabunge bungeni wapige kelele hadi dunia nzima isikie kilio chetu. Sizonje ni mwoga sana kupita kiasi ndio maana anatumia hizi mbinu za Iddi Amin!
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo kile kipindi cha XXL kilichokuwa kinaruka moja kwa moja toka Dodoma kimegeuka majonzi baada ya mamia ya vijana kunyoosha mabango yaliyoandika FREE ROMA

Watanganzaji walilazimika kubadili interview na kumwambia naibu waziri habari utamaduni na michezo Antony Mavunde kwamba hawawezi kupuuzia mabango waziri aseme chochote.

Naibu waziri akasema anasikitishwa na kitendo hicho lakini ana taarifa kwamba jeshi la polisi litatoa taarifa punde. Baada ya hapo kwenye segment ya hot 3 at 3 zimepigwa nyimbo mbili za ROMA ambapo umati umepagawa na kupiga mayowe.
Uandishi gani huu uliokaa kibashite- bashite? Kwanza Antony Mavunde sio naibu waziri habari utamaduni na michezo.
 
Screenshot_2017-04-07-16-10-49.png
kwa ambao hamjaangalia .oneni wananchi walivyocharuka.
 
Back
Top Bottom