Tamasha la kijinsia

qeentar

Member
May 20, 2011
24
1
Mtandao wa kijinsia tanzania (TGNP)unaandaa semina ya demokrasia na maendeleo,ardhi,nguvukazi,na maisha endelevu litakalofanyika tarehe13 hadi 16 septemba mwaka huu jijini Dar es salaam

tamasha litalenga zaidi harakati za kijamii na wanawake walioko pembezoni kuhakikisha wanapata fursa sawa za kufikia na kumiliki rasilimali katika ngazi zote.

katika muktadha wa zahama ya fedha na uchumi duniani,inayojiri sasa,unyang,anyi wa rasilimali za Africa ambao unahusisha ardhi,maji,misitu,madini,mafuta,gesi ya asili,unaofanywa na makampuni ya kimataifa na serikali zao unatishia ustawi na riziki ya watu wengi hususan wanawake

mada za tamasha la jinsia zitalenga kwenye nyenzo za kupata haki na uchumi ili kufikia maisha endelevu.

changamoto kubwa inayomkabili mwanamke wa kawaida ni jinsi ardhi inavyomwathiri yeye,watoto na vizazi vijavyo.
itaendelea
 
Kwani hiyo ardhi na rasilimali za nchi kugaiwa wageni ama mafisadi wachache zinafanywa na hao wanakongamano ama serikali? Hapa kuna kila dalili ya kuzuga
.
 
Back
Top Bottom