Tamasha la Franco Luambo Luanzo Makiadi Grand Master( Grande Maitre) Dar es Salaam- Early 1970's

Attention na SIDA , baada ya franco kupimwa ufaransa akaelezwa anaukimwi na hatopona akatoa kibao cha tahadhari ya gonjwa baya ambalo baadae lilimchukua,
KIMPA KISANGAMENI pia ni ngoma nayoipenda sana hapo alihadithia watu wabaya waogopwe sana maana hawana huruma kabisa.
 
Franco alikufa kwa UKIMWI wakati huo ndio ugonjwa bado mpya
Uko sahihi.. ule Ukimwi ulikua mkali sana, siku chache kabla ya kifo chake Franco anapanda jukwaani kufanya show, amekaa kwenye kiti hata kusimama hawezi, anajaribu kupiga gitaa ya ule wimbo wa Chacun pour soi anahangaika sana Melody inakataa badae Inakubali ili sio Kama ile ya kawaida!
 
Attention na SIDA , baada ya franco kupimwa ufaransa akaelezwa anaukimwi na hatopona akatoa kibao cha tahadhari ya gonjwa baya ambalo baadae lilimchukua,
KIMPA KISANGAMENI pia ni ngoma nayoipenda sana hapo alihadithia watu wabaya waogopwe sana maana hawana huruma kabisa.
Ajabu ni kwamba baada ya kujua atakufa alitengeneza nyimbo nzuri sana, mfano wimbo Kama Sadou... Au Muongo na Murozi alioimba na Samagwana...

Kuna watu duniani Mungu kawaleta kwa Makusudi kabisa.
 
Ni kweli kwamba Luambo Makiyad Franco alimiliki ndege aina ya Boeing 737?
 
Hivi francoo na Tabuley Nani alianza mziki kati ya hawa wawili


Je pia walikuwa kund moja la TP OK JAZZ au kila mtu alikuwa na kundi lake Mgibeon

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mkuu iko hivi. Tabu Ley alizaliwa mwaka 1937, àlianza muziki wa bendi mwaka 1956 na bendi ya African Jazz. Bendi yenyewe ilia zishwa mwaka 1953. Mastaa wa bendi hiyo walikuwa Joseph Kabasele(Grand Kale), Tabu Ley, Dr Nico Kasanda(mpiga solo) ...kwa upande wa Franco Makiadi alizaliwa 1938, na àlianza kutoa wimbo wa Kwanza akiwa na miaka 13 wimbo uloitwa Bolingo na Ngai Beatrice (mpenzi wangu Beatrice)...akiwa na miaka 15 akawa anarekodi kwenye studio ya Loningisa. Mwaka 1956 yeye na rafiki zake akiwamo Alex Mosekiwa( mpuliza sax) walianzisha bendi. Walfanya kikao cha kuchagua jina wakiwa kwenye bar ya jamaa aitwaye Oscar Kashama. Baada ya masaa mengi mwenye bar akawashauri Waite bendi yao OK Jazz...! lakini miaka michache baadae wakabadili jina na kuita TP OK JAZZ. kuhusu kuwa bendi moja haijawahi kutokea! Lakini wamewahi kufanya kazi ya pamoja na kutoa album ya pamoja mwanzoni mwa miaka ya 80. nyimbo inaitwa Ngungi ni moja ya kazi walipiga kolabo pamoja. TP OK JAZZ katika uhai wa Franco walitoa albums 150! kwa ujumla Franco Ni mwanamuziki mkubwa kuliko Tabu Ley. Ingawa Tabu Ley alikuwa mwimbaji mzuri sana!
 
Bila shaka mkuu alimiliki ndege japo sina jina la aina aliyomiliki. Kwa sababu Franco alikuwa tajiri haswa. Katika miaka ya 1980 utajiri wake ulikadiliwa kuzidi dola za marekani milioni 3! Ni hatari mkuu. Jamaa tangu miaka ya 1970 alikuwa anawalipa wanamuziki kupitia benki siyo mambo ya pesa mkononi. Alikuwa na uzito wa karibu 140kg! Alikuwa anakula mbuzi mzima alone

Ni kweli kwamba Luambo Makiyad Franco alimiliki ndege aina ya Boeing 737?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom