Tamasha la filamu za bara asia kuanza kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamasha la filamu za bara asia kuanza kesho

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, Mar 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG] TAMASHA kubwa la filamu za Bara la Asia linatarajiwa kuanza kesho katika Ukumbi wa World Cinema uliopo Mwenge jijini Dar na kumalizika Machi 25 mwaka huu.
  Katika tamasha hilo nchi zilizohakikisha kushiriki ni pamoja na India, Iran, China, Korea na Indonesia.
  Akizungumza na mtandao huu katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar, Balozi wa India hapa nchini, Ngulkham Gangte, alisema lengo la tamasha hilo hapa ni kutaka kuunganisha mahusiano ya kiutamaduni kati ya nchi za bara la Asia na Tanzania.
  [​IMG]
  Balozi wa India hapa nchini, Ngulkham Gangte akiwajuza wanahabari tamasha hilo. Kulia ni Afisa Utamaduni wa Ubalozi wa Iran, Saeed Omidi na kulia ni mmoja wa wadau kutoka bara la Asia.

  [​IMG]
  Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakipata burudani ya vinywaji baridi.

  [​IMG]
  Washiriki wengine wa hafla hiyo walionaswa na kamera yetu wakikata kiu.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Hivi sisi nasi tuna matamasha yetu ya filamu za kiafrika tunayoyafanya kwenye mabara mengine?
  Kama hatuna maonyesho yetu nje, tutarajie nini??
  Kufa kwa utamaduni kwa mwafrika ndio huku.
   
Loading...