Tamasha kubwa la Zinduka leo-Leaders

Mayolela

JF-Expert Member
Sep 21, 2009
384
6
Nimepata taarifa kuwa leo kuna tamasha kubwa sana la kampeni ya Zinduka kutokomeza Malaria.Na mkul uJMK atakuwa ndani ya nyumba,pa moja na burudani mbalimbali.Kweli kwani kwa sasa malaria ni ugonjwa hatari kulingana na Ukimwi,TB.
Hima wananchi hima tujitokeza kuzindua kampeni hii.
 
Hakuna jipya hapo zaidi ya Muungwana kwenda kujirusha na bongo flavour na kutia maneno mawili au matatu ya kampeni kwa vijana!
 
Nilifikiria ni Zinduka ya CUF. Anyway baada ya ARI MPYA.... Slogans kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2010 zinaanza kuibuka.
 
Hakuna jipya hapo zaidi ya Muungwana kwenda kujirusha na bongo flavour na kutia maneno mawili au matatu ya kampeni kwa vijana!
Kweli kabisa na wataoenda huko ni wale wanaochukuliwaga kura zao kwa upande wa kanga na fulana!!
 
Tunatokomeza malaria bilicanas? Au humo ndio kuna mbu wengi sana kuliko vijijini kwa kina bibi zetu?
 
Watanzania bwana tunatokomeza malaria kwa muziki. Vichekesho kwelikweli.
Kinachotakiwa ni kufyeka nyasi, kuzibua mifereji ili kuondoa mazalia ya mbu, kunyunyizia dawa ya kuua vului lui nk, sio kuelimisha namna ya kutumia chandarua, (hakuna asiyejua hilo) na kucheza disco,
 
Kinachotakiwa ni kufyeka nyasi, kuzibua mifereji ili kuondoa mazalia ya mbu, kunyunyizia dawa ya kuua vului lui nk, sio kuelimisha namna ya kutumia chandarua, (hakuna asiyejua hilo) na kucheza disco,

Kaitaba uko sawa kabisa, sasa hizi nyimbo hivi kweli mkazi wa kiburugwa, nyamuswa, ipinda etc ataelewa mantiki ya bongo flava kuhusu malaria? Nashindwa kabisa kuunganisha halafu nasikia kulikuwa na kiingilio shs 3000 mimi nadhani hao wenye hizo 3000 wangeongezewa 2000 na serikali ili kila mmoja anunue chandarua.

Kwa jinsi watu walivyojaa nadhani kidogo ingeleta sense lakini nyimbo mhh sidhani.

mwenye tathmini ya matumizi na mapato ya siku hiyo atupe ili tuone kama kulikuwa na mafanikio au la.
 
Jamani tusijidanganye. Vita dhidi ya malaria si rahisi, na ndo maana tunawatumia wasanii kufikisha ujumbe.

Ni rahisi sana tukiamua na kuwa serious na hilo.

Hivyo mradi wa wajapani wa malaria control project uliishia wapi?????????

Dawa bure, magari na pikipiki bure, wataalamu wa bure lakini bado mradi ukafa kifo cha mende sasa hii bongo flava itatokomeza malaria kweli ?????
 
Back
Top Bottom