Tamasha kabambe la Mafundi ujenzi na Wauza vifaa vya Ujenzi kufanyiaka Kawe Jumapili hii Banana Zoro na Inspector Babu watakuwepo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Wananchi wote wa Dar Es Salaam na Vitongoji vya jirani, Wanaalikwa kwenye tamasha la ujenzi litakalofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe tarehe 31 Mwezi huu wa Tatu 2018. N keshokutwa siku ya Jumapili.. Bonanza litaanza mapema sana. Mafundi ujenzi waliobobea wote na Wauza vifaa vya ujenzi wote watakuwepo na mabanda yao ya maonesho.
IMG-20190401-WA0038.jpg

Jacqueline Alex Mushi, mkurugenzi na mwanzilishi wa Ujenzi zone&Mafundi Connect, amesema Kampuni inahusika na kuunganisha watu wanaojenga na mafundi mabalimbali pamoja na Wauza vifaa vya ufundi.

Nia ya madhumuni ni kutaka kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi wajuane na kuweka mikakati katika shughuli za ujenzi zifanyike vipi ili wale Wauza vifaa vya ujenzi mafundi na wananchi wanaojenga, waweze kukutana na kubadilishana mawazo.

Hii Kampuni nimeanzisha kwasababu maswala ya ufundi yamevamiwa na makanjanja.

Kwa ufupi mwanzo wa hii Kampuni imeanza 2012 katika jukwaa la facebook. Mwanzilishi wake anasema yeye wakati anajenga alitapeliwa sana na mafundi, alikuwa hajui chochote, hajui wapi apate fundi, wala wapi anunue vifaa. Ndo maana akaanzisha ujenzi zone. Sasa jukwaaa lina mika saba na wanachama zaidi ya lami tatu

"Mafundi wamepata sehemu ya kujitangaza, na wauza vifaa pia. Sisi tumewaandilia mazingira mazuri kwa wanaojenga" kasema Jaq. Diaspora wengi wanatutegemea.. Kwani huwa wanawasiliana na sisi na kuwarahisishia maisha. Kwetu unaweza kupata mafundi waminifu na vifaa vya ujenzi pia.

Bonanza tumeamua kuitumia kama mbinu ya kujitambulisha na Wananchi Kama mnataka mafundi wazuri tunao, tuna mafundi wa fani 10. Mafundi bomba, mafundi umeme nk. Hivyo ni fursa kwao kuja kupata dondoo za ujenzi na maswala ya ghama za ujenzi.
IMG_20190329_111613_4.jpg

Tumeamua kuwa na mpira wa miguu siku ya bonanza. Timu nane zitachuana katika mfumo wa kutoana. Na mshindi tutampa zawadi na tutaiendeleza na kuiita ujenzi FC. Na tunataka iwe ngazi ya Kitaifa na kimataifa na iendelee hadi kwa vizazi vijavyo. Siku hiyo tutatengeneza na kuzindua timu zetu. Timu ya Vijana, wazee, veterani. Na Timu ya ujenzi zone itazinduliwa rasmi

Kutakuwa na maonesho. Kutakuwa na mabanda ya Mafundi na watakuwa wanapokea taarifa na kuelezea nini wanakifanya na kutoa ushauri kuhusu ujenzi, kutakuwepo Mabanda ya Wauza Vifaa vya ujenzi. Tuna mafundi 500 waliobobea ambao watashiriki, kwani tunao kwa miaka 7 sasa.

Kutakuwa na wadhamini ambao pia watakuwa na mabanda yao. Tutakuwa na tuzo ya mafundi bora kwa hizi fani 10 ambazo tunazo. Tutatoa tuzo za heshima kwao.

Kutakuwa na burdani. Inspector haruni babu atakuwepo. Pia Msanii mkongwe na mwanzilishi wa The B- Band, Banana Zorro atakuwepo na wengine wengi kutoa burdan

Hata mafundi wamejipanga katika kushiriki kucheza na kuimba. Tunawakaribisha sana Kawe.
IMG_20190329_105547_7.jpg

Inspector amesema ameona ni vyema kushiriki ili kuwawakilisha wasanii wenzake. Mimi nimeona fursa. Tunaweza pata connection nzuri hasa wale tunao jenga. Tutaweza kujua wapi vifaa bei nafuu. Sasa nina nyimbo mbili ambazo nimezitoa mpya na ntaziimba pale kawe.

MC Pambe pia atakuwepo.

Tumaini Mkojera mwakirishi wa wadhamini amewataka watu wengi kujitokeza.
 
Back
Top Bottom