Tamaduni zetu zinasemaje, matendo haya ni sahihi kufanyika TZ?

Ukitaka kwenda na tamaduni halisi za kiafrika, mtoto wa kike anavaa kibwaya (kama cha Kipepe kile) halafu juu maziwa wazi. Sasa kama issue yako ni "kukaa uchi" tamaduni zetu zinaruhusu watoto wa kike kukaa "uchi" kuliko hawa.

Sema jingine.

Ona waswazi hawa wanaodumisha mila zao.

swazii.jpg
 
mkuu naona misimamo yako huwa wakati mwingine imekaa kikoloni hivi, you dont want to think nje ya box, na ukiambiwa unakuwa mkali coz umejifungia ndani ya box na funguo umetupa nje.

mbona haujajibu hoja mkuu? sijaona ulipojibu hoja btn the lines, au ukiwa nje ya box ndiyo inakuwa hivyo?

wapi nimebishana na nani kuonyesha ukali wangu? mbona naona unanizulia?
 
mkuu naona misimamo yako huwa wakati mwingine imekaa kikoloni hivi, you dont want to think nje ya box, na ukiambiwa unakuwa mkali coz umejifungia ndani ya box na funguo umetupa nje.


Biri wewe ndie uliyejifungia kwenye box na funguo kutupa nje. Maana ukijiulizwa swali hili je nguo hizo za nusu uchi zinaruhusika mahali pa heshima? Mfano bungeni, kanisani au maofisini? Jibu ni hapana, sasa jiulize ni kwa nini. Mwanamke anapojifunua maumbile yake mbele ya kadamnasi kuna jibu moja tu ama hayupo kwenye akili zake au amepagawa na pepo la ngono. Kujifunua kwa mwanamke kuna mahali pake napo ni faragha tana kwa mtu ambaye ni mmewe. Hata hivyo kuku kujipitisha juu ya majukwaa huku wanaume wenye uchu wakiwakodolea mimacho kama nyama nono ya buchani kunadhihirisha ninyi mmeumbwa kwa ajili ya wanaume na wala sii wanaume kwa ajili yenu. Sasa ule usawa mnaoutafuta mtaupata je? Kuna mavazi ya staha na pia kuna ya kikahaba. Ya kikahaba kwa sababu yamevaliwa wrong place kwa wrong person na kinyume chake sii ukahaba. Namna hii ya kuvaa nusu uchi sii tamaduni yetu waTz na tunajaribu kuwarudisha mabinti zetu ndani ya ufahamu wao waanachane na kuiga kila kitu hata kama kimetoka kwa shetani.
 
Ukitaka kwenda na tamaduni halisi za kiafrika, mtoto wa kike anavaa kibwaya (kama cha Kipepe kile) halafu juu maziwa wazi. Sasa kama issue yako ni "kukaa uchi" tamaduni zetu zinaruhusu watoto wa kike kukaa "uchi" kuliko hawa.

Sema jingine.

Ona waswazi hawa wanaodumisha mila zao.

swazii.jpg

Mbona yamesha tepwereka kiasi hicho ,Au ndio yamechezewa sana?
 
Hapa kinachosemwa ni nini?

1. Nguo zinawafanya kina dada wawe nusu uchi hivyo si za heshima?

2. Nguo zinawafanya kina dada wawe nusu uchi na si za utamaduni wetu?

Kwa sababu hivi ni vitu viwili tofauti. Na kama nilivyoonyesha hapo juu, notion ya kwamba nguo/mavazi ya asili ya kiafrika ni ya "heshima zaidi" kwa maana yanafunika zaidi si kweli.Nimeonyesha hapo juu kwamba sisi kiutamaduni tunaenda style za "The Gods Must Be Crazy" na wasichana wanaenda na vifua wazi.Mpaka miaka ya 50's 60's watu walikuwa kwenye mabasi wanakuja Dar mitaa ya Chalinze, Mkuranga, Mlandizi unaona watoto wa kike wenye umri wa kubalehe na wengine waliovunja ungo tayari wanatembea maziwa nje.

Sasa kama tunaongelea utamaduni, hawa mamiss naona wame cover zaidi ya utamaduni wetu.

Kama mnaongelea issue ya heshima, heshima inajikita katika misingi ya utamaduni.Sasa hii hehima mnayoiongelea heshima gani? Au mnaongelea heshima ya kimagharibi?

Maana angalieni, katika ku make an argument kwamba dada zetu wamekosa heshima na wanavaa kimagharibi sana na nusu uchi, mtakuwa mnaji expose utovu wa werevu wa utamaduni wenu.

Na in fact mtakuwa mnatuambia kwamba nyinyi mnaosema kina dada wanaiga umagharibi ndio mtakaokuwa mnaiga umagharibi, kwa kutaka watu wajifunike kwa kaniki mwili mzima, kaniki ambalo kiafrika hata hatukuwa na viwanda vya kulitengeneza.

The irony of it all!
 
Back
Top Bottom