Tamaduni Za Kipumbavu


Waridi

Waridi

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2008
Messages
1,027
Likes
2
Points
135
Waridi

Waridi

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2008
1,027 2 135
Watanzania wenzangu,napendekeza tuachane na kuadhimisha sikukuu ya wajinga.

Mjinga ni mtu asiyejua kusoma au kuandika au vyote viwili.Namna nzuri ya kuadhimisha siku yake basi ingekuwa ni kumsaidia aonokane na ujinga wake na pengine kumsaidia hapate kila ambacho kwa sababu ya ujinga alionao anakikosa,matharani kushindwa kupata taarifa muhimu zilizoko katika maandishi nk.
Cha kusikitisha eti duniani kuna sikukuu ya wajinga na inaadhimishwa kwa kudanganyana-kupeana habari za uongo-kupumbazana.
Kwangu mimi maadhimisho ya namna hiyo ni upumbavu.Heri basi siku hiyo ingeitwa sikukuu ya WAPUMBAVU,kwa maana ya kwamba ni siku ambayo waongo na wapumbavu wanapata fursa ya kusema uongo wao hadharani.

Najiuluza ni nini kisa cha watanzania kushabikia sikukuu hii,hadi hata vyombo vya habari vinaamua kuwauzia wanunuzi wa magazeti na wasikilizaji wao habari za uongo.
Maadhimisho haya ni upuuzi,tamaduni ya kuachana nayo.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,032
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,032 280
waridi nadhani tatizo liko kwenye sisi tuliotafsiri siku kuu ya "fools day" kuwa ni siku ya wajinga (ignorant). Sasa ingekuwa ni siku kuu ya wajinga basi suluhisho lako ni muhimu kwamba tunaelemishana, kwani ujinga hutoka; kwa bahati mbaya upumbavu hauotoki kwa elimu bali kwa mtu kuoneshwa upumbavu wake.
 

Forum statistics

Threads 1,237,260
Members 475,501
Posts 29,282,832