Tamaa ya viongozi inaipasua nchi vipande vipande. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamaa ya viongozi inaipasua nchi vipande vipande.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PISTO LERO, Oct 13, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Na yasema haya kwa uchungu na kwa uangalifu mkubwa kwasababu naipenda nchi yangu , Niwazi sasa hivi nchi inaendeshwa kwa mashindano kwa viongozi kutaka kujaribu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ili badae wajisifie kuwa wao ndiyo walio fanya bila kujali mathara ya baadae kwani viyu vingi vinafanywa kwa kulipuliwa ilimradi tu wapata sifa,lakini naomba kutoa tahathari .tanzania iko hatarini kupasuka vipande vipande na sidhani kama kuna kiongozi analiona hilo. NITATOA MIFANO MICHACHE NA UFAFANUZI KADIRI YA UWEZO WANGU. Mwaka 1995: katika uchaguzi mkuu Nchi ilipita katika misukosuko mikubwa kutokana na siasa ya vyama vingi kuwa ndiyo kwanza inapata kasi,tulishuhuia vituko vya kila aina lakini kwa kudra za mungu tulipita salama.na hapa ikumbukwe busara za mwalimu zilitumika sana tunamshukuru kwahilo kwasababu alikuwepo. Mwaka 2000: hali haikuwa mbaya sana kama hapo nyuma hii ni kutokana na wananchi kuanza kuelimika juu ya siasa ya vyama vingi,hivyo uchaguzi huo ulipita kwa utulivu wa hali ya juu japo kulikuwa na makovu kidogo. Hii ilikuwa ni kwa bara, visiwani wakati huo walishapata joto ya kisiasa na hii ni kutokana na wenzetu kuwa na uhuru mkubwa wa kuzungumzia maswala nyeti yanayoihusu zanzibar. Tofauti na bara ambapo ilikuwa ni marufuku kuihoji serikali Raisi alikuwa ni mmbabe,tabia hii ilipelekea watanzania wengi kuiogopa serikali na kuwa na nizamu ya woga,ila viongozi walijitahidi kufanya kazi ipasavyo na uchumi wa nchi kuimarika pamoja na sarafu kuwa na thamani. Kitendo hicho tu kiliwafanya watanzania kutulia na kuwa na matumaini kwani serikali ilifanya mambo kwa ufasaha na maendeleo kiasi kuonekana. MWAKA 2000: kijana uchaguzi haukuwa mgumu kabisaaaaaa ikizingatiwa kuwa MH.Kikwete alikubalika sana haswa na vijana pamoja na akina mama kwasababu moja tu.tulikuwa na imani nae kuwa atatufikisha tunapopataka matokeo yakawa sivyo tulivyo tarajia wengi,tukaanza kushuhudia matumizi makubwa ya pesa za walipa kodi,uchumi ukaanza kuporomoka,pesa ikaanza kushuka thamani kwa kasi ya ajabu,imani ya wananchi ikatoweka ghafla kwa serikali,tukaanza kujutia uamuzi wetu. MWAKA 2005: Mh.kikwete akaponea chupuchupu akashinda kwa kura chache sana tofauti na ilivyo tarajiwa na wengi.lakini je?swaligumu la kujiuliza ni mbinu gani zilitumika? Na je,ni makovu gani yaliyo achwa wakati wa kampeni?hapa ndipo tunapotakiwa kupajadili kwa kina kuelekea kupata katiba mpya. Gari letu linauwezo wa kubeba tani 10 dereva akisaidiana na utingo,kwatamaa zao na sifa zilizopitiliza na kwasababu wanazozijua wao,wanalazimisha garihili kubeba tani 20. Tujiulize kwanini wanangÂ’angÂ’ania kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja?! Madereva wengine si wanakuja? Kwanini hawataki kubeba mzigo saiz yao?ili wafike kwa wakati na kwa usalama zaidi? MTANZANIA HEBU JENGA PICHA HII. Tunataka katibampya Wakati huo kunaudini wa hatari unaofukuta Wengine koti la muungano limesha wabana hivyo wanataka kulivua. Wakati hatujapata ufumbuzi wa hayo uchaguzi mkuu huoooooo. Jiulize nini kitatokea kama siyo nchi kupasuka vipande vipande
   
 2. mtumishidc

  mtumishidc JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 488
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  lengo la ccm ni nchi kugawanyika vipande vipande ili iweze kuendelea kuitawala. kwao wao nchi ikibaki imara ndio kiama cha ccm maana wanachi watasimika chama mbadala haraka na kwa sababu hiyo ndio maana wameamua kutumia mbinu chafu ili waigawe nchi vipandevipande na waendelee kuitawala. Baadhi ya mbinu hizi
  1) udini
  2) kudhoofisha mfumo wa elimu tanzania na kuwanyima mazingira bora ya wananchi kuelimika
  3) kuiruhusu zanzibar ijione ni Taifa na nchi Kamili
  4) ucheleweshwaji wa katiba mpya na bora( % za kupata katiba mpya inayokidhi viwango kabla ya uchaguzi 2015 ni chini 50%).
  hakika ni jukumu letu kutafakari na kuiamsha jamii!
   
Loading...