Tamaa ya ****** Makubwa Yamuua Msanii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamaa ya ****** Makubwa Yamuua Msanii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Msanii mmoja wa Hip Hop wa kike anayechipukia wa Uingereza amefariki dunia baada ya kujidunga sindano ya kuongeza makalio ili aweze kutamba kwenye anga za muziki kama kina Beyonce au Jennifer Lopez.
  Kwa wale dada zetu wanaotamani kuwa na makalio makubwa na kuamua kujidunga sindano za kuongeza makalio basi wajifunze kutokana na habari hii ya mrembo wa Uingereza aliyezaliwa Nigeria mwenye umri wa miaka 20, Claudia Aderotimi ambaye amefariki wiki hii baada ya kudungwa sindano za kuongeza makalio.

  Claudia alitamani kuwa na makalio makubwa ili yaweze kumuongezea jina kwenye anga ya muziki wa Hip-hop kama wanavyotamba kwa makalio yao Beyonce na Jennifer Lopez.

  Mbali ya usanii wa muziki Claudia alikuwa pia na ndoto ya kuwa msanii mkubwa wa maigizo na mcheza dansi kwenye video za muziki.

  Claudia aliamua kuongeza ukubwa wa makalio yake baada ya kutimuliwa kwenye dili la kudansi kwenye video ya msanii mmoja wa muziki nchini Uingereza.

  Taarifa zilisema kuwa Claudia alipata dili la kudansi kwenye video ya muziki, siku ya kwanza alienda akiwa amesunda nguo kwenye makalio yake ili kuyafanya makalio yake yaonekane makubwa.

  Siku hiyo alipokelewa vizuri na alitamba kwenye maandalizi ya video hiyo lakini alipogundulika kuwa alikuwa akiweka nguo kuyafanya makalio yake yaonekane makubwa alitimuliwa na kuambiwa asirudi tena.

  Ili kuzitimiza ndoto zake za muziki, Claudia alisafiri kutoka London hadi Philadelphia, Marekani ili aweze kudungwa sindano za kuongeza makalio ambazo zilimgharimu dola 2000.

  Claudia alidungwa sindano hizo ambazo zimepigwa marufuku nchini Marekani ndani ya hoteli moja mjini humo.

  Muda mfupi baada ya kudungwa sindano hizo, Claudia alilamika maumivu makali kifuani na alipowahishwa hospitali alifariki.

  Polisi nchini Marekani wanamtafuta daktari feki aliyemdunga Claudia sindano hizo huku wakiwa tayari wameishamtia mbaroni mwanamke anayedaiwa kulifanikisha dili la Claudia kusafiri kutoka Uingereza kwenda kwenye hoteli hiyo kuongeza makalio yake.

  "Tumemhoji mwanamke aliyekuwa akiwasiliana kwa email na Claudia kufanikisha Claudia kuja hapa", alisema msemaji wa polisi na kuongeza "Kwa sasa tunamtafuta daktari aliyemchoma sindano hizo".
   
 2. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  Sasa huyu tumuombee aende peponi au kwa moto wa milele?
   
 3. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hata ukimuombea huyu shetani hawezi kuacha t*k* liende peponi hivi hivi....hapa duniani tu mnaona mambo yake....je huko.
   
 4. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kufa pia ni njia amojawapo ya kutimiza mambo yako!
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  smh!!!is it a right decision?
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu shetani sasa hivi anapasha huko kwake!!!
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hayo ndiyo mambo ya kutaka kwenda na wakati.
   
 8. k

  kituro Senior Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kuokana na tabia za kupenda vitu ambavyo hatuna, pia kutamani kuwa na hali ambayo mungu hakutujaalia ndiyo inayotufikisha hapa! sasa ikiwa mambo ndiyo kama haya itakuwaje?

  kwa sasa mie napenda mjue kuwa shetani hana huruma na mwanadamu kwakuwa yeye hakumuumba hivyo hana uchungunae ndiyomana anatutesa apendavyo!
   
 9. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
   
 10. M

  Mwera JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu hashcool huyu ndio huyo bint aliekufa kwakudungwa sindanoya kuongeza makalio au vipi?mbona hakunamaelezo ktk hii picha?
   
 11. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  ndio mwenyewe huyo...
   
 12. M

  Mwera JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  asante sana mkuu pia nakupa hongera ktk post zako napia michango yako huwa nakukubalisana uko makini na hauna pumba,nakupa thanks kwa umakini wako ktk kutoa na kuchangia mada.
   
 13. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  this means a world to me mkuu...thanks
   
 14. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Huyu uwezekano mkubwa kafariki baada ya kupata aidha anaphylactic au anaphylactoid reaction ya hilo lisindano la kuvimbisha makalio.
   
 15. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  RIP Mrembo iwe fundisho kwamba uzuri ni gharama paundi 1,000 ni ndogo sana kwa kutaka urembo
   
 16. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Du wange muwahi kumdunga hydrocortisone inj pengine angepona!!
   
 17. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #17
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ni kweli maana kwa haraka hilo tayari ni kosa mbele ya mungu
   
 18. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mtu au mgonjwa akionyesha dalili za "allergic reaction hatarishi ya maisha", dawa nambari moja inatakiwa iwe ni Adrenaline (Epinephrine) ikifuatiwa kwa baadaye na Hydrocortisone pamoja na Chlormpheniramine. Hizi dawa mbili za mwisho zinachukua muda mrefu kuanza kufanya kazi ingawa zikishaanza kufanya kazi zina fanyakazi kwa muda mrefu. Lakini lifesaver ni adrenaline.

  Bila kusahau kingine muhimu kabisa ni ABC: A=Airway protection and maintanance(100% Oxygen). B=Breathing, mgonjwa apumulishwe kama hapumui. C=Circulation, mgonjwa alazwe chini na miguu yake inyanyuliwe juu ili damu iliyoko miguuni ihamie kwenye moyo na ubongo zaidi. Aongezewa na maji mwilini. Haya ni baadhi tu ya mambo machache.

  Wito: Hawa watu wanaofanya huduma za kudungadunga midawa ya mitako wajiandae au wawe na utaratibu wa kuwahudumia wateja wanapopatwa na allergic reactions. Na ili kunusuru maisha ya watu wafungiwe kabisa hizi shughuli zaovinginevyo watatumalizia vimwana vyetu.
   
 19. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli mkuu! Nchi zilizoendelea kama UK...huwa wanawapa watu wenye hizi severe allergy rxns sindano hizi wanakuwa wanatembea nazo muda wote!!!
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,463
  Trophy Points: 280
  kwani maombi ya watu ndio yanasaidia mtu aende peponi?? hata kidogo ndugu yangu matendo yako kabla ya kufa ndio yana determine kila kitu ukishakufa ni kwisha habari yako ndugu
   
Loading...