Tamaa ya Madaraka iliyovuka mipaka anayoiongelea Kikwete ni ipi?

kibunda

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
403
52
Wana JF,

Jana Mkulu alipokuwa anaongea na sisi aliibua tahadhari kwa wananchi wa Igunga kutotumiwa na Wanasiasa kufanikisha maslahi binafsi na tamaa ya madaraka iliyovuka mipaka. Nimekuwa najiuliza, hao ni wanasiasa gani? Je, alikuwa akiwasema Magamba au Magwanda? Na kwamba, mipaka ya tamaa ya madaraka ni ipi ili yeye apime tamaa iliyovuka mipaka? Je, mipaka ni zile juhudu za chama kung'ang'ania madaraka hata kwa gilba, wizi na kuchakachua?
 
katika sifa nadra alizonazo jk ambayo hata wanaomkosoa walikuwa wakiikubali ni uvumilivu na kuonekana muungwana. sijui imekuwaje sasa ameanza kukosa sifa hizo na pengine wanaomshauri wanampeleka kubaya. katika hotuba yake ya mwsho wa mwez anawaita wapinzan wake wanye tamaa ya madaraka. hii si kaul inayotarajiwa kwa kiongoz kama yeye. alikuwa anatarajia nn ulipotangazwa uchaguz igunga. au alitaka vyama vinine visishrik ndiyo aone kwamba hawana tamaa ya madaraka
 
Naona ni kama kauli za kukata tamaa hivi. Ni kweli ameishiwa na uvumilivu. Anaona joto linazidi kupanda.
 
Anaongelea wanasiasa wahuni kama wa cdm ambao wapo tayari kuingia ikulu hata kwa kumwaga damu kama walivyoleta mungiki igunga!
 
Yule jamaa rarely knows what he is talking!
Angalia anavyokuwa anaropoka mambo yanayo backfire mbay.
....list ya wauza unga
.....viongozi wa dini ni wauza unga
.....sihitaji kura za wafanyakazi
.....kuna udini
yote haya anayaongea kama amerekodia hivi!!
 
mwenye tamaa ya madaraka ni yeye aliyetumia mbinu chafu tangu mchakato wa ndani ya chama 1995-2005 na kwenye uchaguzi mkuu wa 2010. Leo anapata wapi uwezo wa kuwaita wenzie wanatamaa iliyozidi au kijembe kwa magamba wenzie maana wanatumia njia isiyo sahihi
 
Iron finger, ukiangalia siasa zetu na kuchambua vizuri utangudua ni nani aliye na tamaa ilivyovuka mipaka kati ya CDM na CCM? Ni kweli CDM wanatumia gia kubwa. Lakini ifahamike kuwa kwa gilba na ubabe wa CCM chama bila kuwa Ngangari hawawezi kupata kitu. CCM bila kutokwa damu hawaachii madaraka. Watafanya kila ufisadi. Si unaona hata kule Zanzibar, wamesalimu Amri tu baada ya CUF kuamua kumwaga damu.

Anaongelea wanasiasa wahuni kama wa cdm ambao wapo tayari kuingia ikulu hata kwa kumwaga damu kama walivyoleta mungiki igunga!
 
Naona kifo cha ccm kinakaribia.
Mungu ailaze roho ya ccm, mahali pa ajabu.
 
Na ndiyo maana ukiangalia matendo yake na kauli zake unaweza kupata unafiki mkubwa.

mwenye tamaa ya madaraka ni yeye aliyetumia mbinu chafu tangu mchakato wa ndani ya chama 1995-2005 na kwenye uchaguzi mkuu wa 2010. Leo anapata wapi uwezo wa kuwaita wenzie wanatamaa iliyozidi au kijembe kwa magamba wenzie maana wanatumia njia isiyo sahihi
 
jaman hata mimi nilimshanga sana uenda ajajua mpaka saizi watanzania wa sasa siyo wale wa zamani
 
Anafikiri TZ ya leo ndiyo ile ya mwaka 1961. Lakini nashangaa leo ujasiri wa kufoka amepata wapi? Hatujasahau ile hotuba ya mwaka mpya pale Mkulu alipoongea kinyonge dhidi ya maandamano kama vile mtu anaomba kazi. Lakini ni katika hotuba hiyo ndipo aliposurrender suala la katiba kwamba serikali imekubali iandikwe upya.

jaman hata mimi nilimshanga sana uenda ajajua mpaka saizi watanzania wa sasa siyo wale wa zamani
 
Yule jamaa rarely knows what he is talking!
Angalia anavyokuwa anaropoka mambo yanayo backfire mbay.
....list ya wauza unga
.....viongozi wa dini ni wauza unga
.....sihitaji kura za wafanyakazi
.....kuna udini
yote haya anayaongea kama amerekodia hivi!!

nina mashaka na uwezo wako wa kufikiri na kutafakari.fanya utafiti kabla ya kuja hapa mkuu...
 
Back
Top Bottom