SoC02 Tamaa na Wivu ni Adui Mkubwa Sana katika mafanikio ya mwanadamu

Stories of Change - 2022 Competition
Jun 3, 2022
13
13
WIVU NA TAMAA NI ADUI MKUBWA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

Tamaa ni nini Tamaa ni Hali ya uhitaji Uliopitiliza Juu ya Jambo Fulani au ni Hali ya uhitaji wa Ghafla juu ya jambo Fulani bila kuangalia kwa undani juu ya jambo Hilo. Wahenga wakaja wakasema "Tamaa ni Mbaya" wakaenda mbali zaidi wakasema "Tamaa mbele mauti nyuma". Kwani kila Tamaa ni Mbaya, hapana lakini Tamaa yoyote ile Yenye kuzidi kiwango basi lazima tu iwe mbaya.

Mtu akitamani kufanikiwa katika muziki kama Diamond Platnumz sio vibaya ila tu hiyoo Tamaa isiwe yakupitiliza kiwango maana inaweza kukupelekesha na ikakufanya ufanye jambo lolote lile ili tu ukidhi hiyo haja ya Tamaa na mwisho wa siku ukishindwa kwa nguvu zako utataka kulazimishwa na kujikuta unafanya mambo ambayo sio na mwisho unaishia umauti tu. Vijana wengi Sana siku hizi tumekuwa na Tamaa ya kupenda kufanikiwa kwa haraka Sana katika maisha yetu hasa katika UCHUMI pia Tamaa ya ngono imekuwa kubwa Sana mpaka kupelekea vijana wengi kupata magonjwa tu kama vile UKIMWI.

Vijana wengi tumekuwa tukitamani Sana kufanikiwa haraka Sana kiuchumi na inapotokea mtu anashindwa anaanza kufikilia dhana potofu juu ya utajiri. Na kujikuta wakienda kwa Waganga wa kienyeji ili waweze kupata utajiri wengine wamekuwa wamiishia kuwa wezi, wengine matapeli kuwa mashoga na vitu vingine vingi vya hovyo. Yafuatayo ni madhara yakuwa na Tamaa ya kupitiliza.

i. Msongo wa mawazo Binadamu mwenye Tamaa yakupitiliza Mara zote huwa na msongo mkubwa Sana wa mawazo hasa anapokuwa amekosea Fursa au kitu alichokitamani kwa mda mrefu mfano mkaka akikataliwa na mdada na kwa Tamaa ya kimwili huwa wanakuwa na hasira na msongo Wa mawazo wakupitiliza Sana Mara nyingne pia hupelekea hadi kujiua.

ii. Kukata Tamaa mapema, mtu mwenye Tamaa ya kupitiliza pindi anapoona mambo yake hayaendi kwa haraka kama yeye alivyotegemea huwa ni rahisi Sana kukata Tamaa mapema na mwisho wa siku anashindwa kufikia Lengo lake alilokuwa nalo na huenda angeenda nalo Polepole huenda lingemletea mafanikio mkubwa

iii. Kujihisi mwenye Gundu au Mkosi, Mtu mwenye Tamaa ya kupata kitu akitakacho kwa haraka huwa anajiona kama ni mtu mwenye gundu au asiyekuwa na Bahati pindi anapoona Lengo lake halitimiii.

iv. Kujihisi mungu amemsahau na mwisho wa siku kuishia kwa Waganga wa kienyeji tu, tunashauriwa tusiwe watu WA kuwa na Tamaa isiyopitiliza sababu Unaweza ukajikuta unamkufuru mungu na kuishia kupata laana tu.

v. Kujikuta Unafanya kazi za kujidhalilisha ili tu utimize Lengo,Vijana wengi siku hizi wameishia kwenye kuvuta Unga na madawa ya kulevya na kuwa watu wakufanya kazi za kushusha heshima yako kama vile kuwa mwizi Tapeli na wengine wanaenda mbali hata kuwa mashoga.

Hivyo Tamaa sio kitu cha kukiendekeza Sana unatakiwa kuwa tu na Tamaa ya kawaida ila tu isizidi uwezo wako.

WIVU
Winu ni kumuonea mtu kijicho, kutotaka mwingine apate, au kufanikiwa kwa sababu wewe hujafanikiwa kama yeye alivyofanikiwa. Katika maisha ya mwanadamu kila mtu anarafiki yake na Mara nyingi marafiki zetu wa karibu huwa wanakuwa na wivu na sisi lakini sio Mara zote kwamba rafiki zetu wanaweza kuwa na wivu na sisi ingawa ni Mara nyingi watu wanaotuonea wivu ni watu WA karibu Sana na sisi. Ndio maana wahenga wakasema "ADUI Hatoki mbali". Mtu mwenye wivu ni Sawa tu na adui wa mafanikio yako.

Watu wengi tumekuwa na wivu wa kuona kwa nini fulani anapata Zaid yangu Leo nataka nikufunze namna na jinsi ya kuwa mtu ambaye Hana wivu.

i. Jiamini
Mtu yeyote yule ambaye anajiamini katika yeye na anaamini kwamba kama yeye hajapata Leo basi hata kesho inakuja huyu mtu hata iweje hawezi kuwa na wivu juu ya mafanikio ya mtu mwingine kwa sababu na yeye anaamini kuwa atafanikiwa tu. Hivo unashauriwa kujiamini ili usiwe mtu mwenye wivu

ii. Jifunze kwa waliofanikiwa Ukiwa na Tabia ya kupenda kujifunza kwa watu ambao wamefanikiwa katika jambo gila I huenda na wewe ndio unafanya hivo hivoo ni lazima upende kuomba ushauri kwa wao waliofanikiwa Zaidi yako na utoe roho ya wivu ili na wewe uweze kufanikiwa kama wao na lazima wivu utakuisha tu.

iii. Kuwa Mkweli, Ukiwa mtu ambaye huongei uongo juu ya swala Fulani ni lazima ufanikiwe Tena ukiwa mwepesi kusema jinsi unavyojisikia juu ya wenzako kufanikiwa kwao inakuwa rahisi Sana kwako kufanikiwa sababu msema ukweli ni Mpenzi wa mungu na mungu anaweza kukubaliki zaidi hata yao

iv. Mwamini Mungu, mwanadamu yeyote yule ambaye anamwamini mungu ni ngum sana kuwa na Tabia ya wivu kirahisi rahisi kwa maana mtu anamwamini mungu anaamini kuwa kama yeye hajafanikiwa sasa basi hata badae atafanikiwa tu na hata weza kuwa na wivuwa mafanikio ya mtu yeyote yule.

v. Tambua mapungufu yako mapema na uyatendeee kazi kwa kuyaboresha ili kesho uwe bora Zaidi ya Leo Mtu mwenye wivu Mara nyingi ni mtu ambaye hayajui mapungufu yake ndio maana anakuwa haoni yeye akifanikiwa na watu wake wa karibu wanafanikiwa hiyoo inamfanya kuwa na wivu lakini mtu akiamua kuyajua mapungufu yake na kuyaboresha kamwe huyu mtu hawezi kuwa na wivu.

Hivyo Jamani naombeni tusiwe na wivu kwa sababu wivu unatukosesha na vitu Vingi vizuri na kupelekea kuwa kosa watu muhimuu katika maisha yetu Ili kuwa mtu ambaye Hana wivu inabidi uyazingatie mambo hayo ambayo nmeyasema hapo juu.

Mwisho Tamaa na Wivu ni vitu vibaya Sana na ni vitu ambavyo vinaenda sambamba Sana na ukiitaka ufanikiwe basi ni lazima uviache hivi vitu haraka iwezekanavyo ili kukufanya uwe bora na mtu mwenye mafanikio zaidi. Tamaa na wivu ni adui mkubwa Sana katika mafanikio ya mwanadamu yeyote yule. Hivo basi tuache Tamaa na wivu ili tufanikiwe.
Mimi ni Davis Abely Nziku (DNA)

Contact ;0755386540
;0628488781
Mkazi wa Kigamboni Mjimwema
 
Back
Top Bottom