Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
Wajumbe wa Taliban wanakutana na maafisa wa nchi za magharibi nchini Norway kwa ajili ya mazungumzo ya kwanza Ulaya tangu kundi hilo lichukue udhibiti wa nchi ya Afghanstan.
Mazungumzo hayo, yaliyopangwa kufanyika kwa muda wa siku tatu, yatakijita katika suala la haki za binadamu pamoja na mzozo wa kibinadamu katika nchi hiyo.
Umoja wa Mataifa unasema 95% ya Waafghanstan hawana chakula cha kutosha.
Maandamano kadhaa yamefanyika Ulaya huku wakosoaji wakidai kuwa Taliban haipaswi kuzawadiwa kwa mazungumzo.
Jumapili, wajumbe wa Taliban walikutana na wanaharakati wa haki za binadamu lakini maelezo ya mazungumzo hayo bado hayajafichuliwa.
Leo Jumatatu inasemekana kuwa siku muhimu ya mazungumzo baina ya wajumbe wa Taliban na maafisa wa magharib. Kikundi hicho kimepanga kuomba kupata mabilioni yake ya dola yaliyofujwa katika benki za Marekani.
Afghanistan imeshuhudia ukosefu wa ajira na mfumuko wa bei za bidhaa, huku thamani yasarafu yake ikiporomoka na benki zimeweka ukomo wa kiasi cha pesa ambazo zinaweza kutolewa kwenye akaunti ya benki.