Taliban Kuvikata Vidole Vya Watu Wote Watakaopiga Kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taliban Kuvikata Vidole Vya Watu Wote Watakaopiga Kura

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Aug 17, 2009.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,996
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Abdullah Abdullah, mpinzani wa Karzai katika kiti cha urais
  Wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan wametishia kuvikata vidole vya watu wote watakaoshiriki kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika wiki ijayo.Katika kampeni ya Taliban kushawishi watu kugomea uchaguzi mkuu utakaofanyika alhamisi ijayo, Taliban wametangaza adhabu kali kwa watu wote watakaoshiriki zoezi la kupiga kura nchini humo.

  Mmoja wa makamanda wa Taliban alitangaza kwenye jimbo la Zabul nchini humo kuwa Taliban watavikata vidole vya watu wote watakaonekana vidole vyao vina wino usiofutika wa kupigia kura.

  Hadi sasa Taliban wameendelea kuupiga vita uchaguzi wa urais utakaofanyika alhamisi wiki ijayo na kuifanya serikali na majeshi ya kigeni nchini humo yasijue nini Taliban wanapanga kufanya baada ya hapo.

  Vitisho vya Taliban kwa watu watakaoshiriki kupiga kura vilianza wiki iliyopita pamoja na majeshi ya kigeni kusisitiza kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa kwa amani.

  Katika kuonyesha vitisho zaidi vya Taliban, zikiwa zimebakia siku tano kabla ya uchaguzi jengo la umoja wa mataifa nchini Afghanistan lililopo mita mia mbili kutoka ikulu ya Afghanistan lilipuliwa kwa bomu na kupelekea vifo vya watu 7.

  Mbunge mmoja na watu wengine 91 walijeruhiwa katika shambulio hilo lilitokea kwenye mlango mkuu wa jengo hilo la umoja wa mataifa.


  chanzo:- Nifahamishe.com
   
 2. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Hii nia ya kukata watu vidole nayo inalenga kuhimiza mafundisho ya dini? Au ni nia ya kutaka kuona wanarudi madarakani? Wanaowakata vidole ni kina nani?Sio watakuwa hao ndugu zao waliochoshwa na vita visivyoisha? Kazi kwelikweli.
   
Loading...