TALGWU mbona hamzungumzii madeni ya watumishi?

Dossa

Member
May 3, 2011
91
21
Guys,

CWT wako imara sana kutangaza mgogoro na serikali mpaka government inataka ikae nayo march 15 lakini TALGWU wamelala tu na kufuga matumbo hawatetei haki za watumishi wake as a result, madeni wataendelea kulipwa walimu tu kama vile watumushi ni walimu pekee, kama kwenye uchaguzi walumu tu, watumushi wengine tunaenda wapi?
 
Watapata wanachokitafuta? Nachelea maana mchawi wa mwalimu ni mwalimu!JPM na KM si ni walimu? tusubiri tuone!
 
yaani katika kitu kinachoniuma ni ile 2% ninayokatwa na TALGWU, yaani inaniuma sana. manake me sioni faida yake, mbaya zaidi wenzangu ambao hawajajiunga tulioajiriwa pamoja wananiona mjinga kukubali kuunganishwa.
nakumbuka mwenyekiti alisema ni lazima kujiunga akatuletea na ushahidi wa kesi za watumishi walizoshinda kama kielelezo cha kazi wanazofanya, lakini kuiukweli TALGWU ni chama cha mwisho kwa utendaji
 
UNGEFANYA UTAFITI MKUU VYAMA VYA WAFANYAKAZI HAVIPO KWA AJILI YA MASLAHI YA MFANYAKAZI.
 
TALGWU ni chama ambacho kinatetea masilahi ya watumishi wa serikali za mitaa na kinafanya kweli katika utete wake na sijawahi kusikia TALGWU imeshindwa kesi CMA au Mahakamani kwani kimeajiri makatibu wazuri na wengi wao wakiwa wanasheria waliobobea. Kwa mfano mwaka huu tangu uanze wametoa matamko makali zaidi ya matatu na maandamano juu yaliyofanyika mwezi januari mwaka huu kushinikiza mambo kadhaa yatekelezwi na srikali. Hayo matamko ninayo yote na kama kuna mtu ana uwezo wa kuyaweka hapa anipe simu yake yenye whatsap nimtumie.
Tatizo kubwa la wanachama wa TALGWU pia ndio watawala sehemu ya kazi kama vile maafisa watendaji wa mitaa, vijiji na kata , maafisa utumishi na wakuu wa idara kwa ujumla wakiwemu Wakurugenzi, kwa hiyo inapofika wakati wa maamuzi
magumu kunakuwa na mgongano wa kimaslahi .
 
TALGWU ni very hopeless! Tatizo kubwa ni kuwatumia watumishi wa umma kuwa ndio hao hao wafanyakazi wao, wanatakiwa kuajiri kama wanavyofanya waalimu na afya
 
TALGWU ni very hopeless! Tatizo kubwa ni kuwatumia watumishi wa umma kuwa ndio hao hao wafanyakazi wao, wanatakiwa kuajiri kama wanavyofanya waalimu na afya
Ushauri wako ni mzuri na Tayari chama kimeshaliona hilo na baadhi ya wilaya tayari wamepelekwa wafanyakazi waajiriwa.
 
TALGWU ni very hopeless! Tatizo kubwa ni kuwatumia watumishi wa umma kuwa ndio hao hao wafanyakazi wao, wanatakiwa kuajiri kama wanavyofanya waalimu na afya
Kivipi mkuu ni vizuri ukataja kasoro zake ili kama chama kikapata muda wa kujitazama kuhusu hizo kasoro.
 
Back
Top Bottom