Kivumah
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,428
- 1,050
Leo katika Gazeti la Majira nimekutana na Repoti hii.
UMOJA wa Mataifa (UN), umeziweka nchi 48 katika kundi la nchi maskini duniani (LDCs), zikiwemo nchi 33 za Afrika, Asia (9), Pacific (5) na Caribbean (1).
Ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012 iliyotolewa na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) kutoka Geneva, nchini Uswisi, ilisema idadi ya watu waliohamia Ulaya kutoka nchi maskini sana (LDCs) iliongezeka.
Ongezeko hilo ni kutoka watu milioni 19 mwaka 2000 hadi milioni 27 mwaka 2010, sawa na asilimia 3.3 ya wakazi wote wa nchi hizo.
Kwa mujibu wa ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012, iliyotolewa na UNCTAD, ilisema nchi maskini sana duniani zinatoa asilimia moja ya wahamiaji duniani kote.
Imesema wahamiaji wanne kati ya watano kutoka LDCs, wanaishi katika nchi zinazoendelea (Kusini) na mmoja kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).
"Kiwango cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng'ambo kwenda katika nchi zao, kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011, kutoka dola bilioni 3.5 hadi bilioni 27.
"Mwaka 2011, kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada milioni 3.2 na kutoka Kenya milioni 2.5," ilisema taarifa hiyo.
Fedha zilizotumwa kwenda LDCs, zilikuwa mara mbili ya thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI).
Nchi maskini zilizotajwa ni Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic, Chad, Comoros, Congo (DRC), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Lesotho, Liberia, Madagascar na Malawi.
Nyingine ni Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo, Uganda, Tanzania, Zambia, Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste, Yemen, Caribbean, Haiti,
Kiribati, Samoa, Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu
My Take!
Hivi nchi hii tujiringanishe na Kenya tu ambao hawapo miongoni mwa nchi masikini walichotushinda ni nini kwa upande wa Rasilimali, Hapa naona viongozi waliopo madarakani wanacho cha kujibu kwa nini Tanzania kwa wingi wa Rasilimali tulizonazo bado ni Masikini, Hii ni aibu kubwa sana jamani.
=======================
Watu wameng'ngania takwimu za miaka 20 iliyopita .. Tanzania nchi ya tatu kwa umasikini Duniani mara Tanzania nchi ya kwanza kwa umasikini Duniani. Angalia Orodha ya Nchi masikini kutoka katika macho ya watu wanaoijua Dunia. Tanzania haimo kwanye orodha ya nchi 25 masikini zaidi Duniani.. Hii maana yake imependa sana katika miaka ya hivi karibuni kutoka nafasi ya 3 hadi nafasi ya 26! Aidha kwa kasi tuliyonayo tunaendelea kuzivuta nyuma nchi mbali mbali na kwenda juu zaidi. Aidha Tanzania inatajwa kuwa moja kati ya nchi 10 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi. Nchi Tajiri zaidi Duniani ni Qatar!
https://fbcdn-sphotos-e-a.akamaihd....0x720/1001011_545338152168858_129569371_n.jpg
======================
Nimejiuliza hili swali nimekosa jibu, kwanini jirani zetu hapa KENYA wameweza kutoka katika hili kundi lakini sisi TANZANIA tumeshindwa ilihali sisi tuna fursa nyingi kuliko wao?!!,
ZIKO WAPI NCHI MASKINI SANA DUNIANI?
Umoja wa Mataifa unaziweka nchi 48 kwenye kundi la Nchi Maskini Sana Duniani (LDCs). Mgawanyo wao ni kama ifuatavyo.
Africa (33): Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic, Chad, Comoros, Jamhuri ya KIdemnokrasia ya Kongo(DRC), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo, Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia;
Asia (9): Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste na Yemen;
Caribbean (1): Haiti;
Pacific (5): Kiribati, Samoa, Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu.
Mchoro 1 – Nchi 48 za kundi la LDCs
Imetolewa na UNCTAD
--
Kutengeneza list ya LDCs
List ya LDCs inapitiwa upya kila baada ya miaka mitatu na Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) la Umoja wa Mataifa, kufuatana na mapendekezo ya kamati ya Sera ya Maendeleo (CDP).
Katika mapitio ya hivi karibuni, Machi 2012, CDP ilitumia vigezo vifuatavyo:
1. Kigezo cha pato la kila mtu, kwa kufuata Pato la Jumla la Nchi (GNI) kwa kila kichwa (wastani wa miaka mitatu)
2. Kigezo cha raslimali watu ambacho kinatumia viashiria kama lishe, afya, kuandikishwa shuleni na kujua kusoma na kuandika
3. Kigezo cha mazingira hatarishi ya kiuchumi. Ambacho kinatumia viashiria kama mishtuko ya kiasili, mishtuko ya kibiashara, udogo na umbali.
source: haki ngowi blog