Takwimu zaonesha kuna ongezeko kubwa la Wagonjwa wa kupooza

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mara baada ya kuelezwa kuwa Taasisi ya Mifupa (MOI), Dar es Salaam imekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa kupooza ndani yam waka mmoja imeelezwa kuwa moja ya sababu kubwa inayochangia hali hiyo ni aina ya maisha ambayo watu wanaishi kwa miaka ya hivi karibuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniphace amesema takwimu zilizopo ni kuwa idadi ya wagonjwa kwa kupooza kwa mwaka hospitalini hapo ni 120-150 wakati miaka ya nyuma idadi ilikuwa wagonjwa 70-80 kwa mwaka.

Dkt. Respicious Boniphace.jpg

Dkt. Respicious Boniphace

Anafafanua: “Asilimia kubwa chanzo ni magonjwa ya presha kutoka na mtindo wa maisha uliopo sasa kwa watu wengi, kubwa ikiwa ni mwili kutokuwa na mazoezi.

“Watu wengi sasa hivi wanatumia magari, bodaboda na aina nyingine za usafiri kila sehemu wanapokwenda hata kama kuna umbali mfupi, tofauti na ilivyokuwa zamani.

“Zamani watu walikuwa lazima watembee hata kwenda kwenye kituo cha daladala ilikuwa kawaida mtu kutembea kwa umbali fulani, lakini sasa hivi mtu anapanda boda kwenda kwenye kituo cha daladala hata kama hakuna umbali wa kiwango hicho.

“Hata watoto watoto wadogo nao hawapati muda wa kutembea, sehemu ndogo tu anatumia usafiri, wengine hawapati muda wa kuacheza na kuufanya mwili kuwa active.

“Hali hiyo ndiyo inachangia magonjwa mengi kama presha au sukari, sasa hivi kuna vijana wengi tu wa miaka 30-35 wanapata magonjwa ambayo zamani tulikuwa tunaona wanapata watu wazima kuanzia miaka 60 na kuendelea.

“Vyakula navyo vinachangia, mfano matumizi mengi ya nyama choma, unywaji wa pombe nyingi, sigara na matumizi ya shisha huku wakiwa hawafanyi mazoezi. Hiyo inaweza kusababisha mishipa ya damu kusinyaa na kuwa hatarini kupata stroke.”

Aidha, Dkt. Boniphace ametoa ushauri kwa kusema: “Niwaambie Wananchi kuwa kama haujisikii vizuri kama vile kichwa kinauma mara kwa mara, kuchokachoka, waende hospitali mapema kabla haijafikia levo mbaya.

“Wasiishie kununua dawa mtaani tu pasipokuwa na maelekezo ya daktari, waende hospitali wakafanyiwe vipimo na kubaini tatizo mapema kama lipo.

Pamoja na hivyo, amebainisha kuwa kawaida kwa siku wamekuwa wakitoa huduma kwa wagonjwa waliopooza 7 hadi 10.
 
Idadi ndogo sana na ukizingatia pia population imeongezeka na inaongezeka kila siku.
 
Idadi ndogo sana na ukizingatia pia population imeongezeka na inaongezeka kila siku.
Kumbuka kuwa hiyo ni Hospitali moja tu, siyo Mkoa Dar yote, sasa jiulize Dar kuna hospitali ngapi kubwa zinazopokea wagonjwa wenye changamoto hiyo, kisha jumlisha na wale wa mikoa mingine, then kwa mwaka unapata watu wangapi?
 
Nyama choma gani? Nadhani gari pendwa za abiria pale Dumila Kilosa hauna madhara.
 
kutakuwa ma matokeo mabaya sana siku za mbeleni, energy drinks zimefamywa kama maji ya kunywa,watu wanapiga mo energy au jembe mpaka tatu kwa siku
Halafu haohao wafanyabiashara wa hizo energy ndio haohao watachukua tenda za kuleta vifaa tiba vya kutibu tatizo walilolisababisha wao wenyewe
 
Back
Top Bottom