Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,188
- 10,668
Kwa mujibu wa takwimu za utawala wa Kizayuni wa Israel kuna watoto 437 Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala huo.
Idara ya jela za utawala haramu wa Israel imekiri kupitia takwimu rasmi ilizotoa kuwa hadi mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu, watoto 437 Wapalestina wameendelea kushikiliwa kwenye jela za utawala huo. 329 kati yao wana umri kati ya miaka 16 hadi 18, watano wana umri chini ya miaka 14 na watoto wengine 10 wamewekwa kizuizini bila ya kufunguliwa mashtaka wala kubainishiwa makosa na mashtaka yanayowakabili.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unakiuka pia haki za watoto hao walioko kizuizini ikiwemo kuwatia nguvuni wakati wa usiku, kuwatesa kimwili na kiakili, kuwasaili bila ya kuwepo yeyote kati ya wazazi wao, kuwashinikiza wakiri makosa, kutowapatia msaada wa mawakili wakati wakiwa kizuizini na kuendesha kesi zao katika mahakama za kijeshi za utawala huo ghasibu.
Jumuiya ya Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala wa Kizayuni ilitangaza hapo kabla kuwa Wapalestina wapatao 6,830 walitiwa nguvuni katika mwaka uliopita wa 2015. Hivi sasa kuna zaidi ya Wapalestina elfu saba ambao wanaishi katika hali na mazingira mabaya kwenye jela za kuogofya za utawala haramu wa Israel.
Kushadidi utiwaji nguvuni wa Wapalestina hususan watoto na vijana wadogo kumezusha malalamiko na lawama kimataifa. Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti likiwatuhumu askari wa utawala wa Kizayuni kuwa wanaamiliana vibaya na watoto wa Kipalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala huo.
Human Rights Watch limebainisha kuwa askari wa Israel wanatumia mbinu za kinyama katika kuamiliana na kuwasaili watoto wa Kipalestina, na kwamba hatua hizo zisizo za kibinadamu zimesababisha madhara ya kiroho na kiakili kwa watoto hao.
Kwa mujibu wa shirika hilo la kutetea haki za binadamu, tangu ilipoanza Intifadha ya Quds hadi sasa, utiaji nguvuni watoto wa Kipalestina umeongezeka kwa asilimia 150.
Zaidi ya Wapalestina 200 wameuawa shahidi tangu mwezi Oktoba mwaka jana hadi sasa, na maelfu ya wengine wamejeruhiwa au kutiwa nguvuni. Vijana wadogo na watoto ni miongoni mwa waliouawa na kujeruhiwa katika ukandamizaji unaoendelea kufanywa na askari wa utawala dhalimu wa Kizayuni.
Kutokana na hali hiyo harakati ya kimataifa ya kutetea haki za watoto imeripoti kuwa watoto 45 Wapalestina wameuliwa shahidi katika Intifadha mpya ya Quds na kusisitiza kuwa inasikitisha kuona kwamba ufyatuaji risasi wa askari wa Kizayuni kuwalenga watoto hao, sasa limekuwa jambo la mazowea na la kawaida.
Vitendo vya ukatili ambavyo utawala wa Kizayuni unawafanyia watoto wa Kipalestina vinakinzana na sheria za kimataifa hususan kifungu cha 16 cha Mkataba wa Haki za Watoto.
Kifungu hicho kimepiga marufuku kuwafanyia ukatili watoto. Ukweli ni kwamba ukiukaji wa haki za watoto wa Kipalestina unaofanywa na utawala haramu wa Israel hauna kikomo; na utawala huo ghsibu unaendeleza jinai zake dhidi ya watoto hao kwa jeuri na kiburi mbele ya macho ya walimwengu bila kujali kufuatiliwa na jumuiya za kimataifa.
Umoja wa Mataifa umeendelea kuchukua misimamo legevu katika kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni. Kitambo nyuma Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alikataa kuitikia miito na vilio vya walimwengu vya kumtaka auweke utawala haramu wa Israel kwenye orodha ya tawala zinazokiuka haki za watoto wadogo, hatua ambayo imezidi kuupa fursa utawala huo dhalimu ya kuendeleza jinai zake bila ya hofu yoyote.
Takwimu za watoto wa Kipalestina walioko kwenye jela za Israel na radiamali za kimataifa