Takwimu za Uchumi wa Mikoa hazina maana kama Mikoa haijitegemei

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,407
8,900
Sielewi hizi takwimu ya kipato cha Mikoa kinachotolewa zina lengo gani haswa, je ni kuonyesha Mkoa upi ni masikini zaidi ya mwingine au ni nini?

Na kama ndiyo je, tukishajua Mkoa fulani ni masikini then what ? Nini kinafwatia? Tunafanya nini sasa na hizo namba?

Kwangu mimi ingeleta maana kama Mikoa ingekuwa inajitegemea kwa maana ya kodi na matumizi mpaka uwekezaji hapo sasa ndiyo tungeweza kulinganisha na kushindanisha lkn sasa hivi Mikoa iliyo mbele kitakwimu haijafanya chochote isipokuwa tu Serikali imeamua kuwekeza huko basi, sasa mnlinganisha nini?

Yaani huwezi kusema Mkoa x uko mbele kwa sababu ya jitihada za Viongozi wa Mkoa kwa maana Viongozi wa Mkoa wanapata kila kitu ktk Serikali kuu.

Mkuu wa Mkoa hana room yoyote ya kubadilisha au kuboresha Mkoa wake, kila kitu kinatoka Wizarani Serikali kuu, hivyo takwimu hizo hazina maana yoyote labda kwa mfumo uliopo wazipeleka Serikalini ambao ndio wanaoamua wapi waendeleze wapi waache.
 
Back
Top Bottom