Takwimu za tume ya uchaguzi sio sahihi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takwimu za tume ya uchaguzi sio sahihi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jatropha, Oct 28, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kwa muda mrefu sana yamekuwepo malalamiko kuwa Tanzania imefika hapa ilipo kutokana na wasomi kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo wa kutoa maoni na ushauri kwa mujibu wa taaluma hata kama havitawapendeza watawala. Hali hiyo imechangia kwa kiwango kikubwa Tanzania kuangukia mikononi mwa kikundo kidogo cha mafisadi.

  Hivi karibuni hali hiyo imeanza kubadilika baada ya wasomi kutambua umuhimu wa kuwa wazalendo zaidi katika masuala yanayohusu taifa hili.

  Mfano halisi ni maoni ya msomi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe aliyeamua kutoa maoni yake katika Gazeti la Mwanahalisi la Tarehe Okt 27- Nov 3 ,2010; kuhusu takwimu za idadi ya watu katika nchi mbali ikiwemo Tanzania ili kuunga mkono hoja yake kuwa Tanzania haiwezi kuwa na watu wenye sifa za kupiga kura wanaofikia Milioni 19.6 kama ambavyo Tume ya Uchaguzi imedai kuwa wamejiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

  Kwa mujibu wa msomi huyo nchi za duni ya Tatu zinakuwa na tabia ya "Pyramid Demographic" kwa watu wa nchi hizi wanakuwa na tabia ya kuoa wake wengi hivyo watoto wengi huzaliwa.

  Hivyo anadai kuwa Tanzania"s Demographic segments inaonyesha kuwa watu walioko katika kundi la umri wa siku moja hadi miaka 18 ni kati ya 65-70% ya watu wote. Hivyo wenye sifa ya kujiandikisha kupiga kura ni 35% ya watanzania Milioni 40, ambao idadi yao itafikia kama watu Milioni 14 tu. Kati ya hao anadai unawza kukuta wenye sifa za kuandikisha kupiga kura kutokana na sababu mbali mbali kama Milioni 12.5 tu. Ikiwa 75% yao ndio watajiandikisha utakuta watu wanaopaswa kuwa kwenye Daftari la Kudumu la Kupiga Kura ni watu Milioni 10.5 tu, na sio Milioni 19.6 kama Tume ilivyotangaza.

  Ndipo msomi huyo anatoa changamoto ya kuundwa kwa Tume kuchunguza kulikoni iwepo idadi kubwa ya wapiga kura kuliko idadi ya watu wanaostahili kuwa na sifa za kunadikishwa kupiga kiura hapa nchini.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  sasa kama tunabishania milioni 19.6, vipi kuhusu wapiga kura zaidi ya milioni 20 kama ilivyotolewa na NBS?
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani unajua nini, bongo tumefika mahali you can just choose not to trust anything. Hii takwimu maana ya ke basi ni population ya Tanzania is about 50 million!
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  tume ya uchaguzi inaongozwa na vile vibabu vilivyojichokea havina uchungu na nchi hii. Badala ya kuwezesha ukombozi kwa faida ya wajukuu zao, vinaongozwa na maslahi binafsi. kwa kweli inaudhi sana. ndiyo maana mimi binafsi nimekuwa nikiwapigia ndugu na jamaa zangu kuwahimiza kutoichagua ccm kwani watanzania hatutakuja kupata ukombozi wa kweli chini ya chama cha mafisadi. mimi ninaamini kabisa kwamba idadi ya wapiga kura imechakachuliwa kwa lengo mahsusi la kuibeba ccm. ole wenu ccm na mafisadi wake, mwisho wa yote hayo upo mlangoni kama si mwaka huu basi ni miaka michache ijayo wakati ambapo viongozi wote waliochakaza nchi yetu watakapofikishwa mbele ya mahakama kujibu mashtaka. sijui jk atakuwa wapi.
   
Loading...