Takwimu za Serikali zinaonyesha 6% tu ya Watanzania ndio wanaolipa kodi

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,320
Takwimu za serikali zinaonyesha Watanzania sasa wako ama wanakafiriwa kuwa Milioni 60.

Kwenye takwimu hizo, wazee ni Milioni 2 na ushee ila hawajafika Milioni 3. Wazee wa kuanzia umri wa miaka 61. Maximum ni Milioni 3.

Kwenye hizo takwimu ina maana nguvu kazi ni watu Milioni 57, yaani ambao umri wao haujafika miaka 61.

Kwenye hao watu milioni 57, tukiondoa watoto na wategemezi, kuanzia miaka 0 hadi miaka 21(ni mambo ya kushangaza kusikia mtu ana miaka 21 amekua categorized kama mtegemezi. Nadhani hii ni Tanzania tu Duniani). Wanakadiriwa kua milioni 25.

Kwa maana hiyo watagemezi wote, miaka 0 hadi 21 na zaidi ya miaka 60 wako milioni 28 ama nusu ya Watanzania.

Maa yake ni kua nguvu kazi ambayo inatwgemewa kama injini ya kuendesha hii nchi, kizazi chenye nguvu ni karibia Milioni 32. Kwenye hiyo nguvu kazi wanaolipa kodi Tanzania hawazidi milioni 4 kwenye database ya TRA.

Hao walipakodi 4M karibu nusu ni wafanyakazi wanaolipwa mshahara na nusu ni wafanya biashara.

Kwa watu milioni 60, wanaolipa kodi hawazidi milioni 4 maana yake hii nchi ina wategemezi milioni 56 sawa na 94% ya population. Hii ni hatari.

Lazima serikali itafute mbinu mpya na mbadala za kupanua wigo wa kulipa kodi na kupunguza hii gap ya dependants vinginevyo hii nchi haitaenda popote.
 
1- Serikali lazima itafute namna ya kukuza na kulea sekta binafsi. Hawa ndio walipa kodi.

Hakuna namna nyingine. Machinga ni namna tu watu wanapambana kuishi lakini siyo suluhisho.

2- Serikali ipunguze kufanya biashara yenyewe kwa yenyewe. Yaani kuchukua pesa mkono wa kushoto na kutia mkono wa kulia.

Ni ngumu sana serikali kupata faida, na hata hivyo hailipi.

Mashirika mengi ya serikali ni ULAJI tu wa wanasiasa.

Huwezi kutegemea watu 3M tu kati ya watu 60M ndio walipe kodi. Na kibaya zaidi kila mwaka unaongeza kiwango cha makusanyo kwa kuwaongezea ukubwa wa kodi watu wale wale badala ya kutafuta walipa kodi wapya.
 
1- Serikali lazima itafute namna ya kukuza na kulea sekta binafsi. Hawa ndio walipa kodi.

Hakuna namna nyingine. Machinga ni namna tu watu wanapambana kuishi lakini siyo suluhisho...
Uko sahihi kabisa.

Hii ya serikali kufanya biashara kwenye hata sekta zisizo za muhimu ni mambo ya ajabu sana.

Serikali ingejikita kwenye umeme, Reli, Maji, Ndege na shughuli nyingine za utoaji huduma kama hispitali lakini kazi nyingine zote zipewe private sector.

Kuna shida mingi kwenye private sector lakini serikali ingeendelea kuiimarisha hizo shida zingepungua sana.

Serikali ipambane kuboresha sector binafsi hasa ya ndani. Wafanyabishara wa ndani wawezeshwe. Sasa hivi kazi nyingi hasa za ujenzi zinafanywa na wachina. Wakandarasi wa ndani wanakua kama vibarua.
 
Kweli hili ni tatizo kubwa sana kwa nchi yetu na ndio maana niliwahi pendekeza hivi:

Mbona VAT kila mtu analipa? Au ile sio kodi?
VAT analipa kila mtu kweli lakini ili VAT iwe na manufaa ni lazima tuwe na mfumo imara wa makusanyo ya kielektroniki na utunzaji wa kumbukumbu za hesabu mzuri.

Watu wengi wanafanya biashara na wanakusanya VAT kwa niaba ya TRA lakini hawaziwasilishi TRA na TRA haina mfumo wa kujua ama kuzijua.
 
Takwimu za serikali zinaonyesha watanzania sasa wako ama wanakafiriwa kua Milioni 60.

Kwenye takwimu hizo, wazee ni Milioni 2 na ushee ila hawajafika Milioni 3. Wazee wa kuanzia umri wa miaka 61. Maximum ni Milioni 3..
Ni kweli serikali ipanue walipa Kodi kwa kufanya ushawishi ningependekeza kuwepo walipa Kodi za uzalendo bila kujali amesajiliwa Kama mlipa Kodi kwa mfano mtu kwa hiyari yake akalipa sh 5000 kwa mwezi na kupewa Cheti Cha kumtambua kwa uzalendo kwa mwaka atakuja kachanga 60.000 na kupata tuzo wakipatikana walau 1,000,000 ni sh 60b na kupewa zawadi ya kutibiwa katika dispensari za serikali.

Pia kuwe na wa daraja la pili wao watachangia sh 10,000 kwa mwezi kwa mwaka sh 120,000 wakipatikana 1m watachangia ngia Kama 120b na apewe tuzo na spare ofa km ya kutibiwa kituo Cha afya daraja la Kwanza watachangia sh;20,000 kwa mwezi mwaka ni 240,000 apewe tuzo na ofa ya huduma ya matibabu hosptali ya wilaya nk polepole baada ya miaka kadhaa kutatokea ongezeko la walipa Kodi ya uzalendo na serikali nayo inapaswa kua na uzalendo Sio kwa wananchi ndiyo wawe wazalendo
 
Ni kweli serikali ipanue walipa Kodi kwa kufanya ushawishi ningependekeza kuwepo walipa Kodi za uzalendo bila kujali amesajiliwa Kama mlipa Kodi kwa mfano mtu kwa hiyari yake akalipa sh 5000 kwa mwezi na kupewa Cheti Cha kumtambua kwa uzalendo kwa mwaka atakuja kachanga 60.000 na kupata tuzo wakipatikana walau 1,000,000 ni sh 60b na kupewa zawadi ya kutibiwa katika dispensari za serikali pia kuwe na wa daraja la pili wao watachangia sh 10,000 kwa mwezi kwa mwaka sh 120,000 wakipatikana 1m watachangia ngia Kama 120b na apewe tuzo na spare ofa km ya kutibiwa kituo Cha afya daraja la Kwanza watachangia sh;20,000 kwa mwezi mwaka ni 240,000 apewe tuzo na ofa ya huduma ya matibabu hosptali ya wilaya nk polepole baada ya miaka kadhaa kutatokea ongezeko la walipa Kodi ya uzalendo na serikali nayo inapaswa kua na uzalendo Sio kwa wananchi ndiyo wawe wazalendo
Good idea.

Watanzania ni watu wa kujitolea sana. Muhimu ni serikali ihakikishe inapambana na ufisadi na kutenda haki ili watu wawe na moyo
 
Ni kweli serikali ipanue walipa Kodi kwa kufanya ushawishi ningependekeza kuwepo walipa Kodi za uzalendo bila kujali amesajiliwa Kama mlipa Kodi kwa mfano mtu kwa hiyari yake akalipa sh 5000 kwa mwezi na kupewa Cheti Cha kumtambua kwa uzalendo kwa mwaka atakuja kachanga 60.000 na kupata tuzo wakipatikana walau 1,000,000 ni sh 60b na kupewa zawadi ya kutibiwa katika dispensari za serikali.

Pia kuwe na wa daraja la pili wao watachangia sh 10,000 kwa mwezi kwa mwaka sh 120,000 wakipatikana 1m watachangia ngia Kama 120b na apewe tuzo na spare ofa km ya kutibiwa kituo Cha afya daraja la Kwanza watachangia sh;20,000 kwa mwezi mwaka ni 240,000 apewe tuzo na ofa ya huduma ya matibabu hosptali ya wilaya nk polepole baada ya miaka kadhaa kutatokea ongezeko la walipa Kodi ya uzalendo na serikali nayo inapaswa kua na uzalendo Sio kwa wananchi ndiyo wawe wazalendo
wazo zuri la kushirikisha kila mmoja alipe kodi, sasa wapiga meza kule mjengoni na serikal kazi kwao.
 
Takwimu za serikali zinaonyesha Watanzania sasa wako ama wanakafiriwa kuwa Milioni 60.

Kwenye takwimu hizo, wazee ni Milioni 2 na ushee ila hawajafika Milioni 3. Wazee wa kuanzia umri wa miaka 61. Maximum ni Milioni 3.

Kwenye hizo takwimu ina maana nguvu kazi ni watu Milioni 57, yaani ambao umri wao haujafika miaka 61.

Kwenye hao watu milioni 57, tukiondoa watoto na wategemezi, kuanzia miaka 0 hadi miaka 21(ni mambo ya kushangaza kusikia mtu ana miaka 21 amekua categorized kama mtegemezi. Nadhani hii ni Tanzania tu Duniani). Wanakadiriwa kua milioni 25.

Kwa maana hiyo watagemezi wote, miaka 0 hadi 21 na zaidi ya miaka 60 wako milioni 28 ama nusu ya Watanzania.

Maa yake ni kua nguvu kazi ambayo inatwgemewa kama injini ya kuendesha hii nchi, kizazi chenye nguvu ni karibia Milioni 32. Kwenye hiyo nguvu kazi wanaolipa kodi Tanzania hawazidi milioni 4 kwenye database ya TRA.

Hao walipakodi 4M karibu nusu ni wafanyakazi wanaolipwa mshahara na nusu ni wafanya biashara.

Kwa watu milioni 60, wanaolipa kodi hawazidi milioni 4 maana yake hii nchi ina wategemezi milioni 56 sawa na 94% ya population. Hii ni hatari.

Lazima serikali itafute mbinu mpya na mbadala za kupanua wigo wa kulipa kodi na kupunguza hii gap ya dependants vinginevyo hii nchi haitaenda popote.
Unapofanya interpretion ya takwimu uwe makini.
Unasema watanzania wengi hawalipi kodi, je ni kodi gani hiyo? Kuna aina nyingi za kodi. Kwanza karibia kila mtanzania ukiondoa watoto wadogo kabisa wanalipa kodi. Mtu anapinunua bidhaa au huduma anakuwa amelipa kodi tayari. Wakulima ambao ni zaidi ya nusu y a watanzania wote wanapouza mazao yao wanalipa kodi ingawa inaitwa jina la ushuru ( crop cess), kimsingi hi hutegemea wingi wa mazao anayouza mkulima na inafanana na ile kodi wanayolipa wafanyakazi (paye) maana base yake ni kipato kwa kuuza mazao. Kama ingekuwa hao wakulima wanalipa kwa kutumia TIN namba ungekuta wanaonekana katika database ya TRA lakini kinachoonekana ni quantity ya mazao. Kodi inatokana na kipato ndio sio idadi ya watu.
 
Sasa kama sera za maccm miaka yote hazina afya ya kuwanyanyua kipato cha watu unategemea nini?

Lakini kodi ya Indirect tax wanalipa kwa njia ya VAT
 
VAT analipa kila mtu kweli lakini ili VAT iwe na manufaa ni lazima tuwe na mfumo imara wa makusanyo ya kielektroniki na utunzaji wa kumbukumbu za hesabu mzuri.

Watu wengi wanafanya biashara na wanakusanya VAT kwa niaba ya TRA lakini hawaziwasilishi TRA na TRA haina mfumo wa kujua ama kuzijua.
Sasa hili ni la kumlsumu mwananchi au TRA?
 
Serikali inakusanya kodi kiduchu afu inajipa kazi ya kuwa mkandarasi na kodi halipi na pesa hizirudi kwenye mzunguko
 
Kodi ikusanyajwe bwasheee.

Mtu wa chini/Mkulima anategemea pembejeo, sukari, chumvi na mafuta kila siku yake iendayo kwa Mungu kimoja wapo hapo atanunua tu ukisikia vimepanda bei hesabu kodi inakusanywa na mkulima au mtu wa chini ambae anategemea mazao kulipa kodi lazima alipe kodi.

Mfano mkulima mwenye familia ya watu 10 hawezi nunua kuacha kununua mafuta hivyo vichwa kumi vitamgharimu ili kila mmoja ashibe hvyo kodi kila kichwa kitamuhusu na hio huanzia bandarini, mzigo ukiwa kwa boss na mpaka kusambazwa kwa mtumiaji wa mwisho huko kote kodi inakatwa.

Hao millioni nne hiyo ni category ambyo ipo na mambo yake hakuna asie lipa kodi lbd waongeze bdii kile knchoptkana kifike shm usika na kitumike vilivyo.
 
Takwimu za serikali zinaonyesha Watanzania sasa wako ama wanakafiriwa kuwa Milioni 60.

Kwenye takwimu hizo, wazee ni Milioni 2 na ushee ila hawajafika Milioni 3. Wazee wa kuanzia umri wa miaka 61. Maximum ni Milioni 3.

Kwenye hizo takwimu ina maana nguvu kazi ni watu Milioni 57, yaani ambao umri wao haujafika miaka 61.

Kwenye hao watu milioni 57, tukiondoa watoto na wategemezi, kuanzia miaka 0 hadi miaka 21(ni mambo ya kushangaza kusikia mtu ana miaka 21 amekua categorized kama mtegemezi. Nadhani hii ni Tanzania tu Duniani). Wanakadiriwa kua milioni 25.

Kwa maana hiyo watagemezi wote, miaka 0 hadi 21 na zaidi ya miaka 60 wako milioni 28 ama nusu ya Watanzania.

Maa yake ni kua nguvu kazi ambayo inatwgemewa kama injini ya kuendesha hii nchi, kizazi chenye nguvu ni karibia Milioni 32. Kwenye hiyo nguvu kazi wanaolipa kodi Tanzania hawazidi milioni 4 kwenye database ya TRA.

Hao walipakodi 4M karibu nusu ni wafanyakazi wanaolipwa mshahara na nusu ni wafanya biashara.

Kwa watu milioni 60, wanaolipa kodi hawazidi milioni 4 maana yake hii nchi ina wategemezi milioni 56 sawa na 94% ya population. Hii ni hatari.

Lazima serikali itafute mbinu mpya na mbadala za kupanua wigo wa kulipa kodi na kupunguza hii gap ya dependants vinginevyo hii nchi haitaenda popote.

Mimi sikusoma sana statistics kwa hiyo nimesoma haraka haraka tu data zako, na ningelipenda kwanza kukuuliza hivi hizi data zote ni official na hukutoa tafsiri yako? Nashangazwa kuwa sikuona mahali panaposema kati ya kizazi chenye nguvu ni wangapi wenye kazi,zinazohesabika kuwa ni kazi hasa sio za ubabaisho, wangapi hawana kazi na wangapi wanakazi za pesa ya mkononi kwenda mdomoni kama vile mvuvi na muuza maziwa au samaki kwa baskeli.

Kadhalika kwa nini unashangaa kuona kuwa Tanzania mtu mwenye miaka 21 bado anaitwa mtegemezi, ilhali takriban percentage kubwa sana ya vijana hao bado wako nyumbani kwa wazazi wao na wanajulikana kama "kula kwa mama, kuvaa kwa baba"? Hadi pale mfumo wa maisha Tanzania utakapobadilika na kumpa kijana wa miaka 21 means za kujituma au kujipatia ajira za kweli sio za kubabaisha kama boda boda, uber n.k. mtoto wa miaka 21 bado atabaki kutegemea kula kwa mama na kununuliwa nguo na viatu na baba.
 
Takwimu za serikali zinaonyesha Watanzania sasa wako ama wanakafiriwa kuwa Milioni 60.

Kwenye takwimu hizo, wazee ni Milioni 2 na ushee ila hawajafika Milioni 3. Wazee wa kuanzia umri wa miaka 61. Maximum ni Milioni 3.

Kwenye hizo takwimu ina maana nguvu kazi ni watu Milioni 57, yaani ambao umri wao haujafika miaka 61.

Kwenye hao watu milioni 57, tukiondoa watoto na wategemezi, kuanzia miaka 0 hadi miaka 21(ni mambo ya kushangaza kusikia mtu ana miaka 21 amekua categorized kama mtegemezi. Nadhani hii ni Tanzania tu Duniani). Wanakadiriwa kua milioni 25.

Kwa maana hiyo watagemezi wote, miaka 0 hadi 21 na zaidi ya miaka 60 wako milioni 28 ama nusu ya Watanzania.

Maa yake ni kua nguvu kazi ambayo inatwgemewa kama injini ya kuendesha hii nchi, kizazi chenye nguvu ni karibia Milioni 32. Kwenye hiyo nguvu kazi wanaolipa kodi Tanzania hawazidi milioni 4 kwenye database ya TRA.

Hao walipakodi 4M karibu nusu ni wafanyakazi wanaolipwa mshahara na nusu ni wafanya biashara.

Kwa watu milioni 60, wanaolipa kodi hawazidi milioni 4 maana yake hii nchi ina wategemezi milioni 56 sawa na 94% ya population. Hii ni hatari.

Lazima serikali itafute mbinu mpya na mbadala za kupanua wigo wa kulipa kodi na kupunguza hii gap ya dependants vinginevyo hii nchi haitaenda popote.

TRA wanataka hao 6% ndio wababe zigo zima la 60mil people. Haiwezekani. Tutafute namna kila mtu alipe kodi
 
Ukiuwa sekta binafsi kwann usipate hio asilimia 6.Yaani utengeneze matatizo ya kuua uchumi the utegemee kukusanya zaidi,ni lzm uwe mporaji pesa za watu Ili mambo yaende
 
Ukisikia tafiti uchwara ndio hizi. VAT inalipwa na kila mtu! Tena inakusanywa kwa mtoa huduma / mzalishaji, yeye anaongeza tu bei ya mwisho kwa mteja.

Kila vocha, kila unit ya umeme, kila lita ya mafuta, kila bia, kila sigara na bidhaa nahuduma nyingine, kuna kodi ya 18% inayoliopwa na mlaji / mtumia huduma.
 
Back
Top Bottom