Takwimu za janga la mvua; mkuu wa mkoa kamdanganya rais kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takwimu za janga la mvua; mkuu wa mkoa kamdanganya rais kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mikael P Aweda, Dec 23, 2011.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Nimekuwa nikufuatilia kwa karibu habari za majanga mbali mbali ktk nchi yetu. Kila mara takwimu za serikali hutofautiana na wadau wengine kama wanahabari, taasisi za kiraia, wachunguzi binafsi nk. Kwanini?

  Leo gazeti la Mwananchi linaripoti kuwa idadi ya waliokufa ni 30, huku mkuu wa mkoa wa Dsm, M. Sadick jana alitoa ripoti yake kwa bosi wake kikwete akisema waliokufa ni watu 20 - tofauti ya watu 10. Hawa 10 serikali haiwajui kweli? Au imewakana kwa maslahi gani?

  Kumbu kumbu zinanipeleka mabomu ya mbagala ambako vyombo vya habari na serikali vilitofautiana kwa zaidi ya watu watu 10. Niliwahi kumpa lift askari wa Mbagala wa JWTZ wiki moja baada ya mlipuko ule, akaniambia askari wao waliokufa ni zaidi ya 10, serikali iliripoti 6 tu, naye anashangaa kama sisi wengine.

  Likaja sakata la gongo la Mboto, tofauti ni kubwa sana kati ya serikali na ukweli wenyewe. Kama sikosei Mwananchi nalo lilitoa tofauti kubwa ya takwimu za waliokufa ukilinganisha na takwimu za serikali. Tofauti ni zaidi ya watu 20. Kwa nini? Maisha ya watz yako rehani kwa maslahi ya nani?

  Kubwa kuliko zote meli ya Islanders, serikali ilisema wamekufa 200 na kitu, baadaye wabunge wa CUF pemba wakasema waliokufa wanazidi 1000. Mimi nilishiriki kipimajoto ya ITV kuhusu ajali ya Islanders na mmoja wa abiria aliyepona ktk ajali ile. Nilimsikiliza wakati wa kipindi na baada ya kipindi hicho. Nikagundua kuwa serikali yetu ni ya kisanii na waongo wa kutupwa. Wabunge wa CUF ni wakweli ktk hili. Uwongo wa nini?

  Kwanini kila mara serikali inawadanganya watz wazi wazi? Hii ni kwa faida ya nani? Nini madhara ya uwongo huu kwa watanzania? Serikali inayoweza kuwadanganya watz ktk mambo muhimu kama vifo, itasema kweli ktk ripoti zake za fedha na uchunguzi mbali mbali inazoziendesha? Tutakwenda na hali hii mpaka lini?
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Uratibu wa matukio hayo ya vifo hufanywa na Polisi, matatizo huanzia pale kutokana na ukusanyaji mbaya wa taarifa.
   
 3. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kashazoea kudanganywa yule , subiri uje uone atavyoropoka hivyo hivyo kwenye hotuba zake za mwisho wa mwezi, sijui bado zipo?
   
Loading...