Takwimu: Watanzania maskini wafikia milioni 4.2

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Ripoti mpya iliyotolewa na Benki ya Dunia (WB) inaonyesha Watanzania milioni 4.2 wanaishi chini ya mstari wa umaskini kwa kupata Sh886 kwa siku.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa Watanzania hao ambao wanaishi mijini na vijijini, wanapata Sh26,000 kwa mwezi, ambayo ni sawa na Sh866 kwa siku.


Akizindua Toleo la Nne la Taarifa ya Hali ya Uchumi nchini jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa WB, Philippe Dongier alisema hali hiyo inatisha.


Dongier alisema mpango huo ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa nchi za Brazil na Mexico na kwamba, nchini umetekelezwa wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).


Mtaalamu wa Uchumi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi na Uganda, Jacques Morisset alisema asilimia 18.7 ya wananchi wanaoishi mijini ni maskini, huku vijijini wakichukua asilimia 71.2.


Aliongeza kuwa asilimia moja ya wakazi wa Dar es Salaam, ni maskini wa kupindukia.


Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu Kitengo cha Kuratibu Utendaji Ofisi ya Rais (PDB), Peniel Lyimo alisema siyo vyema kwa watu kujadili kama Tanzania inaweza kuondoa umaskini uliokithiri au la, badala yake waamini kwamba hali hiyo itakwisha nchini.


“Kwa namna ambavyo Serikali inatoa mchango mkubwa kwenye kilimo, hasa kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) umaskini uliopindukia utakwisha,” alisema Lyimo.

Naye Meneja wa Sera za Uchumi wa WB kwa nchi za Maziwa Makuu, Albert Zeufack alisema nchi nyingi zimeingia katika umaskini kutokana na tabia ya Serikali zao kupenda kukopa fedha nyingi hasa wakati wa uchaguzi mkuu kwenye nchi zao

Takwimu: Watanzania maskini wafikia milioni 4.2 | SHEBBY D BLOG

NB. Katika ripoti hii nimevutiwa na haya maneno ya hawa waliotoa comment zao nilipoweka BLUE inaonyesha mawazo ya MTANZANIA na huyu mwenzetu wa nje hapa ndipo utakapojua ni wapi nchi yetu inaelekea.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom