Takwimu: Wanafunzi 78 wapoteza maisha kwa ajali za barabarani

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,224
1,676
wanafunzi.jpg

Wanafunzi jijini Dar es Salaam wakivuka barabara. PIcha ya Mtandaoni
Dar Es Salam. Jeshi la polisi nchini limesema wanafunzi 78 nchini wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabara huku 181 wakijeruhiwa katika kipindi cha mwaka 2015.

Hayo aliyasema leo na Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama barabarani kutoka Makao Makuu, Fortunatus Muslim wakati wa utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji alama za usalama barabarani.

Muslim alisema kati ya wanafunzi 78 waliofariki, wavulana walikuwa 40 na wasichana 38, huku majeruhi wakiwa 181 ambapo kati ya hao wavulana walikuwa 81 na wa kike 81.

"Maeneo hatarishi ambayo yanaongoza kwa kusababisha ajali za barabarani katika Jiji la Dar Es Salaam ni Lumumba, Mnazi mmoja, Mikumi, Mtambani, Boko, Bunju na Kongowe." Alisema Muslim.

Mashindano hayo ambayo yaliandaliwa na kampuni ya Puma Energy yalilenga kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi juu ya utumiaji wa alama za usalama barabarani.

"Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani limeendelea kutoa elimu kwa wanafunzi, madereva na Jamii kwa ujumla juu ya matumizi sahihi ya barabarani" aliongeza Muslim

Alisema wanafunzi walioshinda shindano la uchoraji wa alama za usalama barabarani ni Shaibu Abdalah kutoka shule ya msingi Gongo la mboto, Abdallah Hussein kutoka Osterybay na Christian Mathias kutoka Gongo la mboto.

Awali, Meneja wa kampuni ya Puma Enegy, Philippe Corsaletti alisema lengo la mashindano hayo ni kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusiana na matumizi sahihi ya barabarani.

Chanzo: Mwananchi
 
Duh inasikitisha! Kinachonishangaza ni hio wakiume 40, wa kike 38 waliokufa. Majeruhi wa kike 81 na wa kiume 81. 20 hawana jinsia?! Au mwandishi/mtoa takwimu akili yake ilikuwa ku balance wakike na kiume
 
Duh inasikitisha! Kinachonishangaza ni hio wakiume 40, wa kike 38 waliokufa. Majeruhi wa kike 81 na wa kiume 81. 20 hawana jinsia?! Au mwandishi/mtoa takwimu akili yake ilikuwa ku balance wakike na kiume
labda takwimu zimepikwa!!! unaweza kuta idadi halisi ni kubwa zaidi
 
Watoto lazima wathaminiwe na kulindwa kwa kila hali.

Pindi wanapotoka shule lazima kuwe na traffic warden watakaowavusha mda wa kutoka shule.

Ni tatizo kubwa kwetu na changamoto ni nyingi kwani kuna watoto wanakaa mbali na shule, lazima shule ziongezeke ili wa mbali wapate elimu karibu na makazi
 
Kwa kweli,wanafunzi wanapokwenda shule,katika kuvuka barabara,wanapata tabu sana,hasa kutokana na madereva wakorofi.
Nafikiri kungetolewa ruhusa kwa raia,kusaidia hii kazi ya kuvusha watoto,kama sheria inaruhusu.
Watu wengi,wahamasishwe kusaidia,kuvusha watoto maeneo ya barabara,maana watoto wakifuatana barabarani,mmoja akivuka mbio,mwingine bila kuangalia,na yeye huvuka barabara mbio,kumbe maskini gari au pikipiki imeshafika karibu,na kumgonga.
 
Back
Top Bottom