Takwimu: wabunge na madiwani msibweteke na data za taifa na UN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takwimu: wabunge na madiwani msibweteke na data za taifa na UN

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zing, Aug 14, 2011.

 1. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Wadau

  Siku chache zilizopita nilisoma thread ya mdau mmoja alieleza kukerwa na na wabunge wengi kuonekana ni wasemaji wa mkoa wa Dar Esalaam. Naam hii ni kero a inatuudhi wengi sijui kama hawa waheshimiwa wabunge madiwani mameyor na watendaji wengine wanafahamu hili.

  Japo hii si mada ya uzi huu nadhahi pia tunatakiwa tupate tawimu za idadi ya siku kwa mwaka ambazo wabunge wanakuwa majimboni......

  Anyway mimi nakwenda kwenye mada iliyonileta hapa

  Napenda kuongezea uchoozi kwa wawakilishi na watendaji wetu kujua je ni wangapi wana TAKWIMU zinahohusiania na maeneo au kazi wanazozoziwajibikia.

  Je una mbunge au Diwani yeyote anaweza kutupa takwimu hizi au zaidi ya hizi

  ELIMU

  • idadi ya shule za primary, sekonadry zilizomo kwenye maeneo yao? mahitaji halisi ya idadi ya walimu na wale waliopo. Ni wangapi wanajua Mwalimu mkuu wa shule ya primary na seondary anapokea mshahara wa shilingi ngapi kwa mwezi . Je wanajua Afisa walimu wa mkoa au wilaya anapata shiligi ngapi kwa mwezi. Ni
  • Ni asilimia ngapi au ni wastani wa watoto wangapi watoto wa jimboni au wilaya hawaendelei na elimu baada ya kumaliza darasa la saba?
  KILIMO BIDHAA, UZALISHAJI

  • Je ni wabunge au wetendaji wangapi wamefuatilia TAKWIMU za kilimo maaluma kwa jili ya mikoa na wilaya zao. Je kuna mbunge anajua jimbo au wilaya yake inatumia TON ngapi za chakula kwa mwaka. Je kuna mbunge anajua Wilaya, au jimbol ake linazalisha TON ngapi za chakula.
  • Au ni wangapi wanajua mahitaji ya bidhaa kama mafuta sukari, etc ya wilaya au mkoa kwa mwaka?
  KIPATO,UCHUMI NA AJIRA

  • Mara nyingi wabunge wengi na sisi binafsi tunareja takwimu zinazotolewa na UN lakini ni wangapi au ni study gani zimefanya kujua wastai o wa pato halisi la wakazi wa i wilaya na majimbo . Je kuna mbunge anajua GDP ya wilaya yake. Je kuna wbaunge wanjua 3 best paid employer katika jimbo lake au wilaya yake ni watu gani au wanafanya kazi gani.
  • Nia wangapi jimboni au wilayani wana formal employement? Ni watu wangapi wasiokuwa na kazi lakinini wanauwezo wa kufanya kazi ziwe ni za nguvu au akili. Kwa mwezi kuna ajira rasmi au zisozo ramsi ngapi ?
  Kwa weli kuna takwimu nyingi tunatakiwa kuzijua iwe ni afya, michezo, usafiri, maji, umeme . life expectancy, etc . Sio taiwmu za taifa tunatak tawimu za wilaya na mikoa.

  Kwa kweli takwimu ni kitu muhimu lakini inashangza wabunge wanabwteteka na kukariri takwimu za UN na taifa. Kitengo chetu cha takwimu taifa nacho kik hoi. Nadhani badala ya kuitwa kitengocha takwimu iitwe itengo cha Sensa ya watu . Maana kazi zao huwa ni za sena na zaidi ya hapo wanachukua zile za UN.

  Tukiwa na takwimu sahihi tutajua mafanikio na matatizo na tutakuwa na njia sahihi ya kutatua matatizo badala ya mambo ya bahati nasibu.

  napenda niskie wabunge wakitoa takwimu za majimbo au wilaya zao ziwe ni za mafanikio au matatizo.


   
Loading...