TAKWIMU: Idadi ya Kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji nchini Tanzania

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,480
2,000
Mnamo Oktoba mwaka 2014, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ilitangaza ongezeko la idadi ya kata, vijiji, mitaa na vitongoji nchini vilivyotumika kwa ajili ya uchaguzi serikali za mitaa.

Ongezeko hilo lilidaiwa kufanywa kwa kuzingatia idadi ya watu kuongezeka kwa kasi na kupanuka kwa maeneo baada ya watu kujisajili.

Kata kwa nchi nzima ziliongezwa kutoka 2,802 mwaka 2009 hadi 3,337, vijiji vikaongezeka kutoka 11,795 hadi 12,423 na mitaa ilitoka 2,995 hadi 3,741 huku vitongoji vikiongezeka kutoka 60,359 hadi 64,616.

Tutarajie ongezeko zaidi 2019 kabla ya uchaguzi?
 
CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
1,971

Hivyo jumla ya vijiji na mitaa kwa Tanzania nzima ni 16,164.
Ikiwa CCM na Magufuli wanataka kutimiza ahadi yao ya kutoa milioni 50 kila kijiji/mtaa; watahitaji jumla ya bilioni 808.2

=idadi ya vijiji/mitaa X 50,000,000.
=16,164 X 50,000,000.
=808,200,000,000.

Najua mpaka sasa 2018 huenda kuna ongezeko la vijiji kutoka mwaka 2014. Hivyo Magufuli atahitaji kama trilioni 1 kutimiza azma hii.

Je, atazitoa? au ndio hizi zinatolewa kupitia elimu bure/bila malipo?

Tusubiri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom