Ninadhani kama vyama vya siasa viko makini ni rahisi kujua idadi kamili sababu kubwa ni kwamba vyama vingi vya uchaguzi vina mawakala katika sehemu za kupiga/kujiandikisha na lile daftari huwekwa wazi kwenye maeneo ya kura ili wapiga kura wa sehemu husika waweze kuthibitisha uhalali wa waliojiandikisha [katika sehemu husika] ninadhani ni suala la coordination tu na wakikuta hesabu zao na nec zimetofautiana basi inakuwa rahisi kushughulikiwa. lakini iwapo vyama vimelala basi idadi iliyotolewa na nec ndiyo inayotambulika.
Mkuu Abunuwas,
Wazo lako ni zuri. Tatizo ni kwamba kunakuwa na vituo hewa vingi ambavyo havisimamiwi na mawakala.Mawakala wanakuwa pia hewa, huko ndiko uchakachaji hufanyika. Na hapo ndio CCM inapojivunia kwamba watapatra %ge kubwa, kwani kama kura halali ni 10 million, basi hizo mtagawana vyama vyote, na wao wataongeza hizo dummy votes 9million. Hapo ndipo REDET wanapopatia vigezo vya kupika hizo data zao maana wana uhakika hao dummy voters ni wa CCM.