Takwimu hii ni sahihi? - Idadi ya wapiga kura TZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takwimu hii ni sahihi? - Idadi ya wapiga kura TZ

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyambala, May 12, 2010.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  21.8m eligible voters registered, says NEC

  By Dominic Nkolimwa
  12th May 2010


  [​IMG] Surpasses target by .5m people

  The National Electoral Commission (NEC) has announced that it has surpassed the voter registration target for the forthcoming general election.

  The Deputy Secretary to the Commission, Dr Sisti Cariah said yesterday that about 21.8 million eligible voters have been registered to vote in the coming election.

  The commission said that it was targeting to register about 21.3 million.

  Dr. Cariah was speaking when the visiting chair of the United Nations Development group and UNDP Administrator, Helen Clark, visited the National Electoral Commission processing Centre in Dar es Salaam.

  He said that the number of registered voters was equal to 86 percent of the population of the eligible voters.

  Dr Cariah thanked UNDP for their support to the general election since being requested to do so in 2004, saying it has had a great significance on the process since 2005.

  He said NEC has improved its Information Technology (IT) as part of preparations for the forthcoming elections.

  He said almost all equipment is ready for the coming general elections, except for ballot papers.

  ….."Our objective is to conduct credible, free and fair general election in October this year" said Cariah.

  Giving her remarks, Clark said she was impressed with the seriousness of the activities that NEC was carrying out.

  She called on the Commission to emphasis civic education for the people, so that they all know the importance of participating in the election.

  She said in the training special groups should be given first priority so that they can fully participate in the process.

  Commission's Executive Director, Raja Karamu pledged that his office will make sure that the coming elections were free and fair.


  SOURCE: THE GUARDIAN

  Tukirudi nyuma kidogo, 2005.

  HEBU tujikumbushe matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Rais Kikwete alivuna kura 9,123,952, sawa na asilimia 80 ya kura zote zilizopigwa. Aliyefuata alikuwa Profesa Ibrahimu Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 1,327,125 sawa na asilimia 11.7.

  Wa tatu alikuwa Freeman Mbowe aliyepata jumla ya kura 668,756 ambazo ni sawa na asilimia 5.9, waliofuata baada ya hao walipata kura chini ya asilimia moja.


  Source: Tanzania Daima - Nov 26, 2008.


  Watanzania tupo wangapi vile?????????
   
 2. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mkubwa,issue hapa ni kuwa watu wengi hawajiandikishi katika daftari na wakijandikisha wengi wao hawajitokezi kupiga kura

  Hili ni tatizo kwa nchi nyingi afrika,na matokeo yake wanasiasa wanachaguliwa na watu wachache kwa maslahi ya wengi

  JE UMEJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU
   
 3. m

  miss annie Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watu tumejiandikisha tunataka hivyo vitambulisho vyao na sio kupiga kura,nani ana mda wa kupoteza kupigia kura mafisadi?? siku hizi kitambulisho cha mpiga kura dili kweli ,huwezi aminika mahali bila kuwa nacho....ila kura hatupigi unless ccm hawagombei.kwa hiyo hiyo figure hapo isikutishe sio wote wapiga kura,watu tuna malengo yetu binafsi......
   
 4. n

  nndondo JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Jamani, tuna tatizo kubwa sana sana sana kuliko tulivyotegemea, inakuwaje watu mnashindwa kutumia dakika moja kusoma wenzenu walichoandika kazi ni kukurupuka tu?

  How do we get into conversations kwa tabia hii ya uvivu wa kusoma na papara zinazoonyesha umbumbumbu wetu na hatuoni haya? This is very embarassing, hivi wachangiaje mmesoma swali na hoja anayoiweka hapa mwenzetu Nyambala? Inahusina vipi na waliyoweka wachangiaji? tatizo letu hatutulii soma between the line tunaulizwa kama hizi takwimu zinaaminika?

  Tuongee hilo sio swala la kutaka vitambulisho wala kujiandikisha kwenye daftari. Huu ndio uzembe unaoendeana na kuwa anonymous, tujirekebishe jamani tunawapa faida wanaosema kuwa ukitaka kumtoa mtanzania kwenye majadiliano mpatie habari kwa maandishi.

  Hichi ndio nilichokiona hapa, tukosoane ili turekebishane sasa nyie ndio mngekua kwenye negotiation teams za mikataba si kungekua na tofauti na hii tunayoilalamikia?

  Nyambala anatupa angalizo kwamba tume imeanza ku doctor tangu base line, hakuna mwaka watanzania wamejiandikisha kwa idadi inayotangazwa na electoral commission wakati wanadia tayari mwaka huu watu wengi zaidi ya mwaka jana hawajajiandikisha.

  Tusome taarifa za tume kwa dar es salaam kwa mfano walishasema watu waliomba siku ziongezwe kwa sababu siku zilikua chache sana hivyo kuwanyima watu nafasi ya kupiga kura. Huko zanzibar tumesikia daftari la wapiga kura lilivyosababisha watu wengi zaidi ya miaka ya nyuma kushindwa kujiandikisha sasa hii overwehlming response imetoka wapi?

  Wana-cook ndio maana wana guts za kusema hawahitaji kura za civil service kwa wao kuendelea kuongozia nchi.
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  You are right Nndondo!
   
 6. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  http://www.nbs.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=97&Itemid=115 Source hii ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa Tanzania ina sema sensa ya mwaka 2002 Tanzania idadi ya watu ni 34millioni. Kwa kukisia mwaka 2010 tuweke idadi ya watu Tanzania 40 millioni ( ingawa sidhani tumefika hapo).

  Ofisi ya Takwimu ya Taifa Tanzania inasema idadi ya watoto toka umri zero mpaka miaka 14 ni asilimia 44.2% ya Watanzania wote http://www.nbs.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=97&Itemid=115 , hivyo watoto wa umri 0 mpaka umri miaka 14 tukipiga hesabu 40, 000, 000 x 44.2% inatupa watoto 17,680,000. Hivyo idadi ya vijana toka umri wa miaka 15 mpaka 17 tuwajumuishe kama wapiga kura wengine walio na umri wa zaidi ya miaka 18, mahesabu ni hivi ya wenye haki ya kupiga kura 40,000, 000 watoe watoto 17, 680, 000 tunapata wapiga kura 22,320,000.

  Tume imefanikiwa kuandikisha watu 21,800,000 hivyo kwa mahesabu yangu ya elimu ya sekondari Tume imefanikiwa kuandikisha asilimia 97.2 %( 21.8 mil gawa kwa 22.320 milioni) ya wapiga kura kuanzia umri wa miaka 15 ; Kumbuka source http://www.nbs.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=97&Itemid=115 .

  Tuendelee kudodosa changamoto ya mahesabu aliyoanzisha mtunga- 'thread"
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama kutakuwa na mizengwe wakati wa mchakato wa kampeni tusije kusikia waliojitokeza kupiga kura ni milioni 10 tu!
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Inakadiriwa kuwa watanzania wamefikia idadi ya milioni 40.3 in Tanzania Country Report pp. 34 (Economist Intelligence Unit, 2010) na 40.9 in Tanzania National Projections Vol. III in page 41 (NBS 2006).

  Kama 21.8 wamejiandikisha na wanaendelea kujiandikisha basi chini ya miaka 18 mpaka wakati wa uchaguzi ni 18.5. Lakini projection za NBS zinaonyesha chini ya miaka 18 ni milioni 22.2.

  Maswali sasa je projection sio sawa? Kama ni sawa basi wameandikisha na watoto hawa NEC. Kama ni sawa tena wamandikisha ghost voters? Je watoto wengi wamekufa kama milioni 4.2? Au watoto wanakuwa kwa kasi sana, miezi sita tu ana mwaka tayari?

  Usahihi wake una walakini!!
   
 9. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Wewe acha kuleta info bila kurejea kwanza, NEC wanasema

  Tumia mahesabu ya chuo kikuu halafu utuletee data hapa. Au toa hao wa miaka 16 - 17 mpaka Oktoba 2010 halafu utuambie umepata nini.
   
 10. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanawayu,
  Hayo maandishi yako mekundu ktk orginal posting yangu nime-edit isomeke kuanzia umri wa miaka 15(na siyo 16). Hapa mie ni mdadisi asiye statistician hizo figures za The Economist/Takwimu-NBS-Tz/NEC-Tz pia ni za kufanyiwa udadisi, maana 'wataalamu' pia hufanya 'madudu' na kuchomekea mambo kwa ajili ya faida zao.
   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Labda sijakuelewa, nina maanisha umri wa kuanza kupiga kura kwa Tanzania ni miaka 18. Sasa hao wa miaka 15 mpaka 17 wanahusika vipi na upigaji kura kuchagua viongozi wa nchi?
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Source: Demographics of Tanzania, Data of FAO, year 2005 ;
   
 13. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  CIA nao wamesema nusu ya watanzania ni watoto. Source: Rai 13 - 19 May 2010.
   
 14. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nndondo ungefrem mawazo yako ukayapaka mafuta ukayaweka hadharani yanafaa sana.

  Yaani ki ukweli hiyo idadi hata mimi imenipa shaka washaiba tayari hawa wakware! Haiwezekani watu wajitokeze wachache halafu wao waseme watu wamevunja record. Mimi nazani tunakoelekea siko. Wewe subiri uone wakishinda pasina haki.

  Haki ya nani misaada itakatwa nasi tutalia nakusaga meno tusubiri tuone. Si mnajua nchi yetu inategemea wahisani asilimia zaidi ya 60???
   
 15. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Naongezea linki ya posti yako mkuu ili wasomaji na wachangiaji wawaze kufuatilia linki mbalimbali na kutoa michango yao kuhusu takwimu
  http://newhabari.co.tz/index.php?option=com_content&view=category&layout=blog&id=38&Itemid=107 nukuu toka gazeti la Rai kutoka CIA:

  ''Kwa kuwa na watu wengi wenye umri wa chini ya miaka 15, ina maana kwamba sehemu kubwa ya raia wa Tanzania inategemea kupatiwa mahitaji muhimu kutoka kundi dogo la wananchi wake, na hivyo kusababisha matatizo makubwa katika uzalishaji wa chakula na upatikanaji wa huduma nyingine muhimu. .........''
   
 16. M

  MJM JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Wakati tunajadili pia tukumbuke kwamba wao walijiwekea malengo (targets) ya kuandikisha wapiga kura 21.3M na wameandikisha 21.8M hivyo kweli wamevuka lengo. Kwa nini waliweka malengo ya 21.3M ni suala ambalo mpaka wakupe base yao otherwise tutapoteza muda mwingi kujadili tusipate jibu. Ukisema 21.3 ni kidogo watakuambia waliweka allowance kwaajili ya defaulters ukisema ni wengi pia kuna tatizo kwa sababu nikiangalia takwimu za wachangiaji tayari zinatofautiana kwa substantial amount.

  Masuala ya kujiuliza ni je watu wote wanaotakiwa kuandikishwa wameandikishwa? Hakuna walioandikishwa mara mbili? Kuhusu wapiga kura watu wengi huwa hawajitokezi kupiga kura na hii ni changamoto kubwa sana kwa watanzania.
   
 17. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2010
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  nikiangalia uchambuzi wa takwimu mbalimbali zilizotelewa kwenye hii thread, ina maanisha NEC imeandikisha wapiga kura zaidi ya asilimia 95, jambo ambalo linatia shaka, tz kama nchi iliyo nyuma kimaendeleo ina vikwazo vingi vinavyo sababisha tusifikie hiyo asilimia
   
 18. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ninadhani kama vyama vya siasa viko makini ni rahisi kujua idadi kamili sababu kubwa ni kwamba vyama vingi vya uchaguzi vina mawakala katika sehemu za kupiga/kujiandikisha na lile daftari huwekwa wazi kwenye maeneo ya kura ili wapiga kura wa sehemu husika waweze kuthibitisha uhalali wa waliojiandikisha [katika sehemu husika] ninadhani ni suala la coordination tu na wakikuta hesabu zao na nec zimetofautiana basi inakuwa rahisi kushughulikiwa.

  Lakini iwapo vyama vimelala basi idadi iliyotolewa na nec ndiyo inayotambulika.
   
 19. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Naona sasa uttata wa hii takwimu sasa umeibuka tena!!!!!!!!!!!!!!
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  siku zimebaki chache sana... Nini kifanyike?
   
Loading...